Tuwasaidie waliofukuzwa UDSM

Tuwasaidie waliofukuzwa UDSM

MESAYA

Member
Joined
Jan 4, 2012
Posts
55
Reaction score
52
Ndugu mtanzania kuna hawa wanafunzi wapatao 48 waliofukuzwa UDSM na kufungiwa Bank Account zao na pia kuondolewa kwenye hosteli za chuo walipokuwa wanaishi, mpaka leo wameshindwa kurudi majumbani kwao kwasababu:


  1. Wana kesi inayowakabili mahakamani ambayo ilifunguliwa na jamhuri juu yao kutokana na mgomo wa tarehe 11/11/2011.
  2. Wanategemea kufungua kesi mahakamani kukishataki chuo kwa hatua iliyochukuliwa juu yao

Kutokana na haya wanafunzi hawa wanalazimika kukaa hapa mjini bila kazi, ajira, biashara yoyote na allowance ya aina yoyote, hivyo basi nawasihi wanajamiiforum tuwasaidie vijana hawa ili waweze kumudu maisha ya hapa mjini ukichukulia ukweli kwamba wengi wanatoka kwenye familia masikini. Njia pekee ambayo itawafanyanya vijana hawa waendelee kukaa mjini wakishughulikia mambo yao ni kuwapatia kazi ambayo iawapa angalao kipato cha kuwawezesha kulipa kodi ya pango na chakula. Wengi wao ni mwaka wa tatu na wa pili na pia wapo mwaka wa kwanza. Professional zao ni tofauti ila wapo waalimu, accountants, finance na linguistic. Jamani tukumbuke kundi hili lina wanaume na kina dada ambao kwa kweli wakikosa pesa kidogo wanaweza kujiingiza kwenye maisha hatarishi kwao.

Tumia e.mail hii kuwasilisha mchango wako au nafasi ya kazi: ismail.mesaya@yahoo.com
 
peleka habari hii kwenye jukwaa la habari mchanganyiko mkuu,humu si mahali pake
 
Sioni mantiki ya suala lako, walivyokuwa wanafanya fujo hawakuwa wanajua madhara yake, let them pay for what they did. Najua wengi mtachukizwa na maneno haya ila binafsi naungana mkono kabisa na hatua ya kuwafukuza chuo na wachukuliwe hatua kali za kinidhamu.

Tumechoka fujo kila siku hata kwa mambo ambayo hayakuwa yanahitaji kuleta fujo, hayo ndio madhara ya kufanya mambo kwa kutaka kusifiwa na watu mwisho wa siku unabaki peke yako unaanza kutapatapa.
 
Wengi wetu tumepita vyuoni. Uaanaharakati ukizidi sana ndo matatizo yake hayo. Wape pole hawa wasomi wetu. walivyoandamana walikuwa wengi. Kafara wanatolewa wachache.
 
Kwanini UDSM tu? Mbona kuna vyuo vingi tumeshasoma habari zao kuwa wamefukuzwa! Na hao wasaidiwe vipi? Labda uanzishwe mfuko wa kusaidia wanafunzi wanaofukuzwa vyuo kutokana na migomo.
 
Pole mkuu,kua front liner kwenye migomo ni mbaya sana ila cha msingi wasikate tamaa maisha sio shule tu kama shule wamefukuzwa wajikite kitaani zaidi na watatoka tu,kusaidiwa kujikimu sio issue sana,waingie mtaani wapige kazi yeyote huku wakitafuta michongo mikubwa,wape pole sana ndo maisha hayo chuo sio sehemu ya kujifanya mjuaji ni pakupita tu hapo wengi humu tumepita hapo UDSm na tushagoma na tukafukuwa hadi mkandala akapita hall two kuangalia kama kuna watu wamebaki si mchezo
 
peleka habari hii kwenye jukwaa la habari mchanganyiko mkuu,humu si mahali pake

hawasi wanachuo? si jukwaa la elimu? kama huna la kushauri, pita kimya kimya. Naamini JF kuna wadau wwengi ambao wengine ni waajiri na wanaweza kuwapa japo tempo work. Pamoja na kuandika e-mail kwa wenye moyo, private sms ni nzuri zaidi
 
hawasi wanachuo? si jukwaa la elimu? kama huna la kushauri, pita kimya kimya. Naamini JF kuna wadau wwengi ambao wengine ni waajiri na wanaweza kuwapa japo tempo work. Pamoja na kuandika e-mail kwa wenye moyo, private sms ni nzuri zaidi

kwa kuwa hao walikuwa wakipewa loan na bodi ya mikopo basi hao ni watoto wa vigogo kwa mujib wa wale wanaharakati walokuwa wakisema mikopo imekuwa iktolewa kwa watoto wa vigogo so hakuna mtoto wa mlalahoi aloathirika basi tuwapotezee tu!
 
Wanafunzi wa sasa waoga sana yani me ningekuwa mwanafunzi leo ningelipua makazi ya mkandara hapo,na kuna kipindi ticha flani hapo alikua ananizingua na nilipanga nilipue utawala sema tulienda nae sawa,hawa washenzi dawa yao ni kulipua yani mnashindwa kujioganaiz wanafunzi hata wa5 mkanunua guruneti na kulipua utawala? Kama mbwai mbwai tu hii nchi mbele haitotawalika biliv dat I'm tellin y'all buddiez
 
Kwanini UDSM tu? Mbona kuna vyuo vingi tumeshasoma habari zao kuwa wamefukuzwa! Na hao wasaidiwe vipi? Labda uanzishwe mfuko wa kusaidia wanafunzi wanaofukuzwa vyuo kutokana na migomo.
nilisoma udsm nakwambia kuna wanahakati mandazi pale alafu kila kunji ikikalipia paper lol.........
 
Back
Top Bottom