SoC01 Tuwatambue watoto wa nje ya ndoa kwani ni damu zetu na tujitahidi kuwa waminifu katika ndoa zetu na mahusiano yetu

SoC01 Tuwatambue watoto wa nje ya ndoa kwani ni damu zetu na tujitahidi kuwa waminifu katika ndoa zetu na mahusiano yetu

Stories of Change - 2021 Competition
Joined
Aug 1, 2021
Posts
6
Reaction score
2
Nakusalimu kwa sauti kubwa ukapate kunisikia sikioni mwako,sina ukamilifu wa kutosha ila moyo unaniuma sana kuhusiana na ghazabu wanazozipata watoto wa nje ya ndoa

Mtoto wa nje ndoa ni yupi?

“Aliyezaliwa kabla ya baba na mama hawajaoana,alizaliwa bila ndoa na baadaye mzazi mmoja akaoa ama kuolewa kwingne ,aliyezaliwa wakati ndoa iko hai kwa baba ama mwanamke mwingne “.

Hivyo tunaona mtoto wa nje ya ndoa ni mtoto aliyezaliwa kabla ya baba na mama kuoana kisha mzazi mmoja akamuwa kuoa mwanamke mwengne nje nayule aliyezaa naye au mtoto aliyezaliwa wakati ndoa iko hai kwa baba ama mwanamke mwengne.

Sababu kubwa ya kuongezeka kwa watoto wa nje ni kutokana na mahusiano ya kimapenzi yanayozuka bila umakini au ukweli ndani ya wahusika (mwanaume na mwanamke)hii husababisha kuzaliwa kwa watoto wengi wa nje ya ndoa ambao hujakupata shida kutokana na malezi mabovu ama yasiyotosheleza kwa asilimia kubwa.Hata hao wanawake wanaozalishwa na kuachwa(single mother) huwa hadhi yao hushuka kwakiasi Fulani katika jamii zetu,haijalishi unauwezo wa kifedha kumlea mtoto au laa.

Ifike kipindi tutumie akili zetu kwa ueledi wa kutosha ili hisia isiweze kutawala ktk maisha yetu kwani wanawake na wanaume wengi hupenda kutawaliwa na hisia kuliko akili kiasi kwamba hata kwenye mamuzi magumu hutumia hisia badala ya akili.Mfano Mtu unafahamu fikra una mke wako wa ndoa ama umeolewa na unamume lakini bado unaruhusu hisia za mapenzi kwa wanawake nje ya ndoa,hili ni aibu kubwa sana kwani huongeza watoto wa nje ya ndoa mitaani na wazazi wa familia moja na kuleta migogoro katika familia.

Watoto wa nje wanapata shida sana na kuathirika kisakolojia hasa pale wanapohisi kukataliwa au kutokutambulika katika familia fulani ambayo baba yake ndiyo mmiliki wa familia hiyo.Wakati mwingne wanafikiri kwanini walizaliwa kukutana na ghazabu hizi.

Pia inakuwa ngumu sana kupata ushrikiano wa kutosha kwa ndugu zake wanaochangia baba kwani inafika hatua wanaonekana kama maadui na wezi na ngumu kuopa ushrikiano wa dhati.

Hivyo ni mama au baba anapaswa kulaumiwa kwa ongezeko la watoto wa nje…? tukisema tujadili hili suala hapa, hatutamaliza leo kwani kila mmoja atamtupia lawama mwenzake kuwa ndio chanzo cha haya yote na kutupiana maneno machafu na kubomoa badala ya kujenga.

Hitimisho,nafahamu kuna sababu nyingi sana za kutokea watoto wa nje ya ndoa,ila pendekezo langu wazazi wahusika yatupasa kuwatambua watoto wetu wa nje ya ndoa.

Pia kuzitafuta damu zetu na kuwahudumia kwa hekima kubwa sana na kuakikisha wanapata kutambulishwa katika familia zetu na kuakikisha uasama ama chukia kwa ndugu zake unatolewa kwa kuwaelimisha kuwa na umoja na upendo.

Pia Mwanamke na Mwanaume popote pale tuhakikishe tunaingia katika mahusiano yenye kesho nje (bright future) na kuzaa au kuwa na watoto baada ya ndoa ili kuepuka kuongezeka kwa wimbi la watoto wa nje ya ndoa na kutunza familia zao kwa hekima kubwa na kumtanguliza Mungu mbele kulingana na Imani zao.

Kila mmoja awajibike kwa nafasi yake ili kutengneza taifa lenye usawa na haki kwa maendele ya nchi yetu na mataifa kwa ujumla.

download.jpg


download (1).jpg
 
Upvote 1
Hii ni mada Pana sana lakini yenye umuhimu mkubwa katika maisha yetu Kila Leo.
Mtoto ni kiumbe ambaye Mungu amemuumba. Naye anayo haki ya kuishi katika amani na furaha kama ambavyo wazazi hao walikuwa nayo kipindi wanashughulika kumtengeneza.

Makosa ya watu wawili hayatakiwi kuharibu future ya mtoto. If you are responsible you shouldn't have ejaculated to the so you call "evil bitch" in the first place. Na if you are smart "you shouldn't have opened your legs" in the first place.
Ok ni kosa. Let's accept and move to the next stage. Mtoto apate haki yake..alelewe vizuri. Maisha yaendelee. Tukikosea tusiongeze makosa. Tujitahidi kujisafisha kwa msaada wa Mungu wetu.

Ndani ya ndoa:
Tumekutana watu tofauti. Ile tofauti ndiyo itakayotukamilisha. Hatuna namna Bali kuyabeba madhaifu na kusonga mbele. Mkikubaliana kuendelea na maisha yenu na watoto wakapata malezi Bora kwa usawa basi inakuwa heri.
Sasa nyinyi mkiruhusu external pressures ziwahunt kama maex, wazazi, ndugu, marafiki..mtabomoa nyumba yenu.

Tukubali Hali ilivyo. Tuendeleze libeneke la maisha. Hakunaga Cha mtoto wa nje wala wa ndani. Mtoto ni mtoto tu. Kama watakula, watalala na kusoma basi ni vyema tayari. Maneno yakianza kuinuka na mkayasikiliza tena yasiyo na tija hakika..ndoa mapema tu inasepa zake.

Msaada wetu uko katika BWANA MUNGU. Tuitafute hekima kwake plus upendo ujae kwa wingi katika mioyo yetu. Hatutakaa kuhesabiana mabaya. Tuzidi kujifunza upendo jamani..
#anywaysmadangumuhiiembunitulienisikilizewahenga.#
 
Wanaume ndo chanzo kikuu
Mtu haridhiki na mkewe anachovya tu nje

Si uoe wake wengi ss km we shababi kweli?!

Wanawake by nature hawakatai watoto
 
Back
Top Bottom