Tuwatambue wenye kutaka kutuaminisha kuwa tu waoga

Tuwatambue wenye kutaka kutuaminisha kuwa tu waoga

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Uzalendo ni pamoja na kuyaweka wazi yanayotukera katika nchi bila kujali yanafanywa na nani.

Ndugu zetu pale kijitonyama, wasiojulikana, waziri Masauni hadi mama Samia tuvumiliane tu. Uzalendo kwanza.

Tuwatambue wanaohaha kutusambaratisha kama Taifa

Kuna maswali ya msingi kwa awaye yote mwenye kutaka kushadadia ulaghai huu kuwa watanzania ni waoga.

"Hivi, kwenye waoga hao na waliokwenda kumpokea Lissu au kusimama naye imara muda wote ikiwamo pale Kiluvya nao wamo?"

Vipi wale waliochanga mamia kwa mamilioni ya shilingi ndani ya masaa tu, ili kuwanusuru wakiwamo kina Bulaya? Nao ni katika waoga hao?

Nakadhalika nakadhalika. Mifano iko mingi mno!

Atudanganye nani?

Upinzani - walio waoga (cowards) si Wafuasi

Habari ndiyo hiyo.

Ikumbukwe:

"In the course of war, fear and terror are often used as weapons to distort the opponent's decision-making or break the opponent's will."
 
Aina ya mchango unaotolewa ili kuyafikia mabadiliko haufanani, kuna mchango unaofanywa na mtu hata akiwa amejifungia chumbani [mf.kumsaidia Lissu gharama za matibabu].

Mchango mwingine ni lazima mtu aende kuutolea field, huu nao upo wa aina mbili;

- Kuna ule wa kwenda field bila kutishwa na jeshi la polisi [mf.kumpokea Lissu akitokea Ubelgiji kwa matibabu].

- Pia ule wa kwenda field huku ukitishwa na jeshi la polisi [kuandamana kudai haki].

Huo mchango wa kwenda field huku ukitishwa na jeshi la polisi ndio Mbowe anauzungumzia, na mwenye mfano mzuri hapo ni Lissu alivyowahi kusema kama akiibiwa kura atawambia wafuasi wake waandamane, hakuna aliyethubutu kwa kuogopa kuvunjwa miguu na afande Sirro.

Hapa naona adui yetu namba moja ni mind zetu, uoga wetu unaanzia kwenye mind zetu kabla hatujafikiria kwenda mbali na kuwalaumu wengine, kwa hili sioni sababu ya kubishana, na mtu kusema ukweli asionekane adui kwani mifano ipo kuthibitisha uoga wetu.
 
Aina ya mchango unaotolewa ili kuyafikia mabadiliko haufanani, kuna mchango unaofanywa na mtu hata akiwa amejifungia chumbani [mf.kumsaidia Lissu gharama za matibabu].

Na mchango mwingine ni lazima mtu aende kuutolea field, huu nao umetofautiana, kuna ule wa kwenda field bila kutishwa na jeshi la polisi [mf.kumpokea Lissu akitokea Ubelgiji kwa matibabu], na ule wa kwenda field huku ukitishwa na jeshi la polisi [kuandamana kudai haki].

Huo mchango wa kwenda field huku ukitishwa na jeshi la polisi ndio Mbowe anauzungumzia, na mwenye mfano mzuri hapo ni Lissu alivyowahi kusema akiibiwa kura atawambia wafuasi wake waandamane, hakuna aliyethubutu kwa kuogopa kuvunjwa miguu na afande Mambosasa.

Hapa naona adui yetu namba moja ni mind zetu, uoga wetu unaanzia kwenye mind zetu kabla hatujafikiria kwenda mbali na hapo, kwa hili sioni sababu ya kubishana.

Pana jambo hapa ni muhimu kuliweka sawa. Kwenda kumpokea Lissu na kusimama naye imara muda wote wa kampeni likiwamo la Kiluvya hayana tofauti na kumwagika barabarani huku kutakakotukomboa.

Tunataka haki? Hatutaki tozo? Tukutane Tahrir.

Ifahamike kulikuwa na vitisho vya kufa mtu kwenye kwenda kumpokea Lissu na hata kwa Lissu mwenyewe kuja. Ikumbukwe pia mwenye lake jambo hapo alikuwa mwendazake mwenyewe, Sirro na genge lao la wasiojulikana wakati huo wakiwa kwenye ubora wao vilivyo.

Huoni pana haja ya kuyaangalia yote haya kutambua tofauti ilipo ili kuona kamili tunakwama wapi?

Ninakazia:

Upinzani - walio waoga (cowards) si Wafuasi
 
Pana jambo hapa ni muhimu kuliweka sawa. Kwenda kumpokea Lissu na kusimama naye imara muda wote wa kampeni likiwamo la Kiluvya hayana tofauti na kumwagika barabarani huku kutakakotukomboa.

Tunataka haki? Hatutaki tozo? Tukutane Tahrir.

Ifahamike kulikuwa na vitisho vya kufa mtu kwenye kwenda kumpokea Lissu na hata kwa Lissu mwenyewe kuja. Ikumbukwe pia mwenye lake jambo hapo alikuwa mwendazake mwenyewe, Sirro na genge lao la wasiojulikana wakati huo wakiwa kwenye ubora wao vilivyo.

Huoni pana haja ya kuyaangalia yote haya kutambua tofauti ilipo?

Ninakazia:

Upinzani - walio waoga (cowards) si Wafuasi
Ni mara nyingi watu wamejitokeza kuandamana wakapigwa na polisi, mfano kilichotokea kule Arusha wakati ule wa Dr. Slaa, waandamanaji walipigwa na polisi wakaumizwa.

Hapa sio suala la kuwatambua wanaotuaminisha sisi ni waoga kama ulivyoandika, ukweli ni kwamba, matendo ya polisi kwa waandamanaji kama mfano hapo juu, yakiambatana na kauli za vitisho za polisi kwa waandamanaji, ndio chanzo cha watu kuchagua wapi wakaandamane na wapi wasiende.
 
Unachokosea ni kuwaunganisha watanzania..... sema haupo kwenye waoga........

Watz tuache unafiq.... wapinzania wameumia sana kwa ajili yetu, wakapaza sauti tukawaona maboya kuna kina wewe brazaj labda mlitoka ila ukweli ni kwamba WATANZANIA TULIWASALITI WALIOTUTETEA.

LIPA TOZO MKUU brazaj
 
Lisu mwemyewe ni mwoga kama kunguru!

We mtu unakimbiliaje ubelgiji kisa kitisho cha kwenye simu?
 
Ni mara nyingi watu wamejitokeza kuandamana wakapigwa na polisi, mfano kilichotokea kule Arusha wakati ule wa Dr. Slaa, waandamanaji walipigwa na polisi wakaumizwa.

Hapa sio suala la kuwatambua wanaotuaminisha sisi ni waoga kama ulivyoandika, ukweli ni kwamba, matendo ya polisi kwa waandamanaji kama mfano hapo juu, yakiambatana na kauli za vitisho za polisi kwa waandamanaji, ndio chanzo cha watu kuchagua wapi wakaandamane na wapi wasiende.

Ifahamike vitendo vya kutumia nguvu na polisi hivyo vinajulikana, vipo na vitaendelea kuwepo. Awaye yote kama anadhani kuna siku havitakuwapo ajue anajidanganya.

Kwenye kumpokea Lissu na kote alikopita kauli zao hazikuwahi kuwa nyepesi hata kidogo. Ikumbukwe polisi hufanya yao kulingana idadi ya watu waliopo kwenye shughuli. Inapokuwa ndogo mno lakini si wakati umati ni wa kutosha.

Hatupaswi kuaminishwa kuwa tu waoga. Hizo ni propaganda za kujaribu kuona idadi kubwa ya kutosha haijitokezi mabarabarani.

Utayari wetu kuyajaza magereza yao pomoni kutatukomboa.

Wanapenda mno kwa gharama yoyote ukweli huu tusiuishi.
 
"Nilikuwa nimezungukwa na watu waliokuwa wakiniambia ukweli nilipokosea, pia walikuwa na uwezo wa kuhoji usahihi wa maoni au mawazo yangu kuhusu dhana yoyote ile.
Unapokosea halafu watu unaowaamini hawawezi kukuambia ukweli na unataka kuzungukwa na watu wanaokusifia tu ni hatari sana". By Barack Obama
 
unachokosea ni kuwaunganisha watanzania..... sema haupo kwenye waoga........

Watz tuache unafiq.... wapinzania wameumia sana kwa ajili yetu, wakapaza sauti tukawaona maboya kuna kina wewe brazaj labda mlitoka ila ukweli ni kwamba WATANZANIA TULIWASALITI WALIOTUTETEA.

LIPA TOZO MKUU brazaj

Ni vyema kuacha kuwasemea watanzania wala kumsemea awaye yote kuwa kasalitiwa. Labda kama unasema wewe umesalitiwa.

Upinzani - walio waoga (cowards) si Wafuasi

Nimewaona watu kwenye harakati hizi wapambanaji kweli kweli. Wanaweza kuwa hata determined kuliko wowote tunaowaongelea humu hadharani.

Ninakazia: wavumao baharini papa, lakini wengi wengine wapo.

Hapa ndipo ambapo si sahihi awaye yote kudhania kasalitiwa. Na adhaniaye hivyo ni heri akaachia ngazi mwenyewe vinginevyo huyo ni sahihi kumfurusha kwa sababu (hadi leo) nathubutu kusema, hatufai.
 
Ni kweli mkuu sisi watanganyika ni waoga sana na hakuna mtu mwenye guts za kupinga jambo lolote likafanikiwa.

Hapo Zanzibar tu ambao tumeungana nao wanatuzidi kwenye kudai haki zao.

Sisi hapa taabu tupu.

Mafuta juu. Kimya.

Tozo kila mahali. Kimya.

Kuongezeka kwa bei kwenye kila bidhaa na huduma. Kimya.

Umeme kukatika katika kila mara. Kimya.

Hakuna anayechukua hatua yeyote kuwafahamisha watawala kuwa wanachokifanya sio sahihi.
 
Ifahamike vitendo vya kutumia nguvu na polisi hivyo vinajulikana, vipo na vitaendelea kuwepo. Awaye yote kama anadhani kuna siku havitakuwapo ajue anajidanganya.

Kwenye kumpokea Lissu na kote alikopita kauli zao hazikuwahi kuwa nyepesi hata kidogo. Ikumbukwe polisi hufanya yao kulingana idadi ya watu waliopo kwenye shughuli. Inapokuwa ndogo mno lakini si wakati umati ni wa kutosha.

Hatupaswi kuaminishwa kuwa tu waoga. Hizo ni propaganda za kujaribu kuona idadi kubwa ya kutosha haijitokezi mabarabarani.

Utayari wetu kuyajaza magereza yao pomoni kutatukomboa.

Wanapenda mno kwa gharama yoyote ukweli huu tusiuishi.
Naona hatua ya kwanza kufikia malengo ni kukubali udhaifu na kuanza kuufanyia kazi, lakini kuendelea kukataa udhaifu wako ni kujichelewesha zaidi kuyafikia malengo.
 
Naona hatua ya kwanza kufikia malengo ni kukubali udhaifu na kuanza kuufanyia kazi, lakini kuendelea kukataa udhaifu wako ni kujichelewesha zaidi kuyafikia malengo.

Njia ya mafanikio makubwa waitumiayo watesi wetu ni kutuaminisha kuwa tu waoga au tu wanyonge.

Hatua ya kwanza ya kujikomboa iko katika kuyakataa hayo kwa vitendo.

Siwaoni waoga hapa:

Wala siwaoni hapa:

Machinga wanapotoa Somo, Makamanda tunakwama Wapi?

NB: "In the course of war, fear and terror are often used as weapons to distort the opponent's decision-making or break the opponent's will."
 
"Nilikuwa nimezungukwa na watu waliokuwa wakiniambia ukweli nilipokosea, pia walikuwa na uwezo wa kuhoji usahihi wa maoni au mawazo yangu kuhusu dhana yoyote ile.
Unapokosea halafu watu unaowaamini hawawezi kukuambia ukweli na unataka kuzungukwa na watu wanaokusifia tu ni hatari sana". By Barack Obama

Hili ndilo ambalo viongozi wetu wanapaswa kuliona na kulizingatia. Eeh Mola wetu utujalie kuyaona na kuyakumbatia hata tusiyoyapenda kibinafsi.
 
Waoga wengine hawa hapa mpaka wana shindwa kukisimamia wanacho kiamini na walicho kitaamka.
images (57).jpeg
images (56).jpeg
 
Ni kweli mkuu sisi watanganyika ni waoga sana na hakuna mtu mwenye guts za kupinga jambo lolote likafanikiwa.

Hapo Zanzibar tu ambao tumeungana nao wanatuzidi kwenye kudai haki zao.

Sisi hapa taabu tupu.

Mafuta juu. Kimya.

Tozo kila mahali. Kimya.

Kuongezeka kwa bei kwenye kila bidhaa na huduma. Kimya.

Umeme kukatika katika kila mara. Kimya.

Hakuna anayechukua hatua yeyote kuwafahamisha watawala kuwa wanachokifanya sio sahihi.

Si kuwa adui yetu anatumia woga kama silaha yake muhimu?

"In the course of war, fear and terror are often used as weapons to distort the opponent's decision-making or break the opponent's will."

Wewe uko upande upi hapo mkuu?
 
Kumpokea Lisu airport ndio Ujasiri?

Ulipaona hapa:

"Nakadhalika nakadhalika. Mifano iko mingi mno!"

Mbinu yenu hii imeshindwa. Tafuteni nyingine:

"In the course of war, fear and terror are often used as weapons to distort the opponent's decision-making or break the opponent's will."
 
Lisu mwemyewe ni mwoga kama kunguru!

We mtu unakimbiliaje ubelgiji kisa kitisho cha kwenye simu?

Zile risasi zilitoka kwenye sms za simu? Kutokuwa muoga hakumaanishi ukabaliane na risasi huku ukiwa na ilani ya uchaguzi mkononi, mwenzako ana AK47.
 
Back
Top Bottom