Tafakari yetu
JF-Expert Member
- Apr 19, 2021
- 1,505
- 4,427
Rais wa JMT, Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan
Waziri wa kilimo, Mhe. Hussein Bashe
na wengine wanaohusika
Ninawapongeza sana viongozi wangu kwa kuwekea mkazo kilimo kiasi cha kilimo kuonekana ni ajira kwa vijana. Mipango na mikakati ya wizara ya kilimo inayobuniwa chini ya waziri Bashe inatoa matumaini kwa vijana kuona kilimo ni fursa. Mpango wa Building a Better Tommorow (BBT) utatengeneza fursa kwa vijana wengi.
Ninaamini kilimo sasa kinatoa kutoa fursa ya mpango wa lishe mashuleni kutekelezwa kwa matokeo makubwa. Kwa kuwa sasa kilimo kinafanyiwa maboresho na mapinduzi makubwa ni muda muafaka maboresho hayo yakasaidie mpango wa lishe na upatikanaji wa chakula mashuleni kupitia nguvu kazi ya wafungwa.
Wafungwa watumike katika kilimo kikubwa. Kwa kuwa ni nguvu kazi itakayotumika bila gharama kubwa itasaidia mpango huu kuwa na matokeo mazuri. Pia, wafungwa wakihusishwa na mpango huu itakuwa ni njia ya kuwajengea uwezo na ujuzi wa kufanya kilimo cha kisasa itakawafaa baada ya mafunzo yao.
Ni matumaini yangu mapendekezo haya yatafika kwa viongozi husika na kuangalia namna ya kuutekeleza kwa namna yoyote inayofaa.