Kwanza jambo hili wadau wa Burudani tuna lipapatikia tuu paso kufahamu ukweli wowote kuhusu jambo hili.
Kosa alilo lifanya huyu Binti ni kwamba "Kwa nini alikubali kutia wino kama hali ilikua ndio hivyo?". Kwa hapa Rubby ana makosa maana yeye kwa miguu yake alikwenda na kwa mikono yake akakubaliana na Clouds Media kwa ajili ya Jambo hili.
Zaidi ya yote kabla ya Masilahu kuzua kizai-zai(According to Her) ni kwamba Rubby angepaswa kuzunguka Fiesta mikoa yote 15 kama ZAWADI ambayo aliahidiwa pindi alipo ibuka mshindi wa Fiesta super Nyota 2014(Swali kwa Mrembo huyu: Je na hili ni la Kimasahi?)
Kuna Jambo ambalo bado wasanii wa kike hapa Bongo iwe ni wa Bongo Movie, Dance, ama Music bado hawajalifahamu ama hawajui lina waathiri kivipi! Unapo itwa Nyota haimaanishi kwamba wewe ndio wewe katika hicho kilicho kufanya ukawa star, Kuna walio wahi kuwa Nyuta kabla yako na ndio maana leo hii wewe ni Nyota maana teyari msingi wa wewe kuwa Nyota ilikwisha wekwa na Nyota hao.
Huyu binti kwa wano fahamu sanaa hasa kwa upande Muziki watakuambia kwamba "Rubby bado ni mchanga mno ana hitaji kufanyia kipaji chake zoeziπDππππ wabongo bhana!) ila kwa kua ameonekana kuwa na kipaji hicho na akapewa nafasi yakukionyesha, basi leo tunamsikia kwenye Medias mbali mbali(shukrani kwa Clouds na THT).
Kwa yeye kuwa na migogoro ya hapa na pale kati yake na wasanii ama viongozi wake, ni kawaida tuu kama binadamu wa kawaida maana migogoro ni sehemu ya Masha ila Je inamjenga ama inaharibia? Kwangu mimi naona kwamba Huyu Binti anajiharibia tena Vibaya mno(Mtazamo wanguππ) maana Mtoto hawezi kupigana na Baba na mama yake eti kisa anapinga kula nyumbani (i.e THT na Clouds Media).
Ajifunze tuu maana nadhani UTOTO unamsubua kidogo. Haoni ni wangapi waliwahi kuja hapa Bongo wakitokea huko huko THT na wakafanikiwa kuwateka mashabiki ila walipotelea pasipo julikana! na Kumuacha COMANDO J-DEE, Yuko wapi Recho mamaaa Kizungu zungu jicho la kungu kiuno cha Nyiguπππ! Yuko wapi bint Almasi a.k.a Mwasiti? Yuko wapi Maunda Alzahir Zoro binti mwenye sauti na sura nzura kama Jini?
My take:
Kwa sasa Clouds ndio wanao onekana kuisimamia Burudani hapa bongo na kwa namna jinsi Bongo flava ilivyo, bila media support HUTOKI kirahisi walahi hata ukiwa na Talent gani. Hili swala linazungumzika, wakae na watafute kanamna aisee na wamuonyeshe huyu Binti venye vile mambo inavyo takiwa kuwaga.
Mapeeenzi hayana mwenyeeeeweeeee......... unawezaza penda kijana au..........