Tuwaze na Kuchambua haya Kuhusu Rubby

Tuwaze na Kuchambua haya Kuhusu Rubby

Simtetei Ruby ila naheshimu sana sana sana maamuzi yake.

Maswali ninayo jiuliza hapa.
1 Ruby ana vi nyimbo vi 3 tu na eti waandaaji walimpa mkataba wa milioni 22,
vp kwa weusi? chege temba madii na blue?
basi fiestar inalipa sana.

2 Wakowapi ma supar nyota wa misimu iliyopira? hivi msodoki alikuwepo kwenye show ya mwanza? kama hakuwepo ni kwa nini?

3 kumbe ukiwa ndani ya THT unakuwa na menejar wako nnje ya tht?(naomba kujuzwa)

yuko wapi mwasiti? Linah Amin barnaba boy dito mataluma.na wengine wengi tu walioamua kutafuta ugar wao nje ya clouds? Ni kwa nini msanii anaye amua kutoka nje ya tht huwa anasuswa na clouds?

ninacho amini mimi fiesta haina maslai sema tu msanii anapewa dulsa yakupiga show kwenye tamasha kubwa.
Nilikiwepo mwanza msodoki alikuwepo na akaamsha sana. Kumbukumbu zangu zinaonyesha washindi wa Super Nyota toka imeanzishwa ni RayVanny au RayMond wenyewe mnamuita kutoka wasafi babyyy akafuata YoungKiller au Msodoki pia kuna binti mmoja nimemsahau jina ila alitambatamba alafu ndiyo akafuata Ruby.

Super nyota wametisha kwa kuibua vipaji
 
Hii story imepikwa sidhani kama kuna ukweli
 
napenda jinsi kalivyoimba kwenye nivumilie. ila kila nikikaona mawazo ya wahadzabe na wasandawe hunijia.
 
Nyimbo na matangazo aliyofanya clouds... yanapigwa kama kawaida... sijui ni kiki kama ile ya Baraka na Blue...

hujasimulia alikataaje kuja kwenye hyo harusi
 
Kwanza jambo hili wadau wa Burudani tuna lipapatikia tuu paso kufahamu ukweli wowote kuhusu jambo hili.
Kosa alilo lifanya huyu Binti ni kwamba "Kwa nini alikubali kutia wino kama hali ilikua ndio hivyo?". Kwa hapa Rubby ana makosa maana yeye kwa miguu yake alikwenda na kwa mikono yake akakubaliana na Clouds Media kwa ajili ya Jambo hili.

Zaidi ya yote kabla ya Masilahu kuzua kizai-zai(According to Her) ni kwamba Rubby angepaswa kuzunguka Fiesta mikoa yote 15 kama ZAWADI ambayo aliahidiwa pindi alipo ibuka mshindi wa Fiesta super Nyota 2014(Swali kwa Mrembo huyu: Je na hili ni la Kimasahi?)

Kuna Jambo ambalo bado wasanii wa kike hapa Bongo iwe ni wa Bongo Movie, Dance, ama Music bado hawajalifahamu ama hawajui lina waathiri kivipi! Unapo itwa Nyota haimaanishi kwamba wewe ndio wewe katika hicho kilicho kufanya ukawa star, Kuna walio wahi kuwa Nyuta kabla yako na ndio maana leo hii wewe ni Nyota maana teyari msingi wa wewe kuwa Nyota ilikwisha wekwa na Nyota hao.

Huyu binti kwa wano fahamu sanaa hasa kwa upande Muziki watakuambia kwamba "Rubby bado ni mchanga mno ana hitaji kufanyia kipaji chake zoezi🙂D😀😀😀😀 wabongo bhana!) ila kwa kua ameonekana kuwa na kipaji hicho na akapewa nafasi yakukionyesha, basi leo tunamsikia kwenye Medias mbali mbali(shukrani kwa Clouds na THT).

Kwa yeye kuwa na migogoro ya hapa na pale kati yake na wasanii ama viongozi wake, ni kawaida tuu kama binadamu wa kawaida maana migogoro ni sehemu ya Masha ila Je inamjenga ama inaharibia? Kwangu mimi naona kwamba Huyu Binti anajiharibia tena Vibaya mno(Mtazamo wangu🙄🙄) maana Mtoto hawezi kupigana na Baba na mama yake eti kisa anapinga kula nyumbani (i.e THT na Clouds Media).

Ajifunze tuu maana nadhani UTOTO unamsubua kidogo. Haoni ni wangapi waliwahi kuja hapa Bongo wakitokea huko huko THT na wakafanikiwa kuwateka mashabiki ila walipotelea pasipo julikana! na Kumuacha COMANDO J-DEE, Yuko wapi Recho mamaaa Kizungu zungu jicho la kungu kiuno cha Nyigu😀😀😀! Yuko wapi bint Almasi a.k.a Mwasiti? Yuko wapi Maunda Alzahir Zoro binti mwenye sauti na sura nzura kama Jini?

My take:
Kwa sasa Clouds ndio wanao onekana kuisimamia Burudani hapa bongo na kwa namna jinsi Bongo flava ilivyo, bila media support HUTOKI kirahisi walahi hata ukiwa na Talent gani. Hili swala linazungumzika, wakae na watafute kanamna aisee na wamuonyeshe huyu Binti venye vile mambo inavyo takiwa kuwaga.

Mapeeenzi hayana mwenyeeeeweeeee......... unawezaza penda kijana au..........
 
mnapenda wenzenu wanavyo nyonya,unajua clouds wanaingiza sh ngap,kupitia hao wasanii,msipende kulaumu uamuzi wa mtu,

Nitajie wasanii wasiofanya kazi na "mnyonyaji" Clouds ambao wana-make pesa yakueleweka kuliko wanaonyonywa na Clouds.
 
tatizo lako unajifanya una huruma, utafikiri kwamba akikosa kufanya shoo na clouds BHAS ATAKUJA KUWA MZIGO KWAKO,KUMUHUDIA,RUBY ANA MAISHA YAKE NA MIPANGO YAKE,hauwezi kumlaumu kwa uamuzi wake,na wala haukusaidii chochote,wala haukupunguzi chochote,angalia shida zako,
 
Tatizo ukizinguana na Clouds wanahakikisha wanakuwekea vikwazo vingi kiasi kwamba hadi wasanii wenzako wanaofanya kazi na Clouds wanakukwepa kufanya nao collabo.

Kabla ya kuchokoza siafu hakikisha una nyasi kavu wahenga walinena.

Je Ruby anazo nyasi kavu?
 
Amejitambua muache aende mwanaume maneno mengi au mwanaume WA Dar ??


dah huyu mwanaume wa dar kabisa yaani katumia masaa kadhaa kuiandika hii habari ya kiki wakati angekuwa mkoani angepiga hata matuta sita ya viazi kwa muda aliotumia
 
Back
Top Bottom