benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,533
- 3,187
Nikiwa kama mdau na mfuatiliaji mkubwa wa sanaa hapa nchini, nimesikiliza kwa umakini, malalamiko au shutuma zinazotolewa na msanii Ruby, kwa kituo cha Redio cha Clouds FM, tamasha la Fiesta pamoja na uongozi wa THT; mimi namkubali sana Ruby kama msanii, mwaka mmoja uliopita nilimpigania aimbe kwenye harusi ya ndugu yangu, bahati mbaya sana harusini sababu za kinidhamu zilinivua mapenzi yangu kwake.
Ni mfuatiliaji sana wa Bongo flava na wasanii wake, na nimeona niandike mtazamo wangu kwasababu kituo cha Clouds hakijazungumza lolote mpaka sasa ili tuweze kujua nini hasa kimetokea kati ya pande hizo mbili, ambazo hadi siku moja kabla ya tamasha la Fiesta lilizozinduliwa Mwanza wiki iliyopita hali ilikuwa shwari,
Kwa hulka yetu ya kibinadamu, siku zote tumekuwa wepesi kupokea malalamiko ya upande mmoja na kufikia uamuzi kuwa hayo yanayolalamikiwa ndio hasa hali halisi bila kutafuta upande wa pili unachosema,
Kuna msemo mmoja maarufu usemao, ‘Kila stori ina pande tatu, pande ya mlalamikiwa, pande ya mlalamikaji na ukweli'
Kwa sababu pande ya mlalamikiwa haijaamuua kuzungumza, mimi kama mdau, nikajaribu kuwaza kimyakimya, na nikaona nijaribu kuweka hapa mawazo yangu, ili yatusaidie kupata labda ufafanuzi wa jambo hili kidogo,
Kwa mujibu wa akaunti ya Ruby ya Instagram, Ruby alisajiliwa kuwa msanii wa kufanya show na Fiesta, wiki moja kabla ya show ya Fiesta Mwanza, na pia siku ya jumatatu tarehe 15 akapost akiwa kweye rehearsal ya Fiesta pale Escape 1, swali ni je, hilo swala la maslahi alilifikiria Alhamisi usiku? Siku moja kabla ya show ya Mwanza?
Baadhi ya wasanii waliosajiliwa Fiesta niliozungumza nao, wanasema mwaka huu wamelipwa kupitia akaunti zao binafsi za benki au za mameneja wao wengine angalau siku 5 kabla ya show.
Meneja wa Ruby, Salehe Gadau inasemekana kuwa Clouds ilimuingizia kwenye akaunti yake jumla ya shilingi milioni saba na nusu (7,500,000/-), kama advance ya malipo ya show tano za Ruby, ambapo kwa nafasi yake kama Super Nyota alitakiwa kufanya show zote za Fiesta ambazo kiujumla angeingiza jumla ya shilingi million 22.5 kwa show 15, ambacho kwangu sio haba kabisa ila tunatofautiana kweli…..inawezekana kweli hicho ni kipato kidogo kwa Ruby.
Nimejaribu kuwaza sijapata jibu, lakini nadhani ni kitu cha kujiuliza, inakuwaje Ruby aliwapa Clouds akaunti ya meneja wake waweke hela, wakati hajakubaliana nao kuhusu maslahi? Na mbona alikuwa na muda mwingi wa kukataa kushiriki Fiesta kama maslahi ni tatizo, imekuwaje ikawa dakika za mwisho?
Lakini je, kama tatizo ni maslahi kweli, najiuliza kwani kuna wangapi wameshindwa kuelewana kwenye biashara, mbona hatuoni wanaenda kwenye vyombo vya habari?? Au ni kutafuta kiki?
Kama kweli THT walikuwa na nia ya kumkandamiza Ruby kama anavyosema mbona nilisikia story ya jinsi Uongozi wake kupitia Gadau walivyohaha kuificha story ya kuwekwa ndani Oysterbay Polisi. Taarifa za chini ya carpet zinasema, miezi miwili iliyopita Ruby alifunguliwa kesi kwenye kituo cha polisi Oysterbay ya kufungua account feki ya Instagram na kumtukana matusi ya nguoni msanii mwenzake aliyekuwa nae THT.
Taarifa za ndani zinathibitisha kuwa hasira kubwa ya Ruby ni kutaka kuwa yeye awe ndo lulu pekee kwa Boss wake wa zamani, na kuongezeka kwa wasanii wengine kumekuwa ni chachu ya matusi kwa hao wengine kila siku hadi kusimamishwa kwenda kituoni hapo kutokana na kutwa kuchafua hali ya hewa pale. Je inawezekana ana ugomvi binafsi na wasanii wengine kama unavyoonekana kwenye video alizorekodiwa akiwatukana matusi ya nguoni na ndio imesababisha ajitoe kwenye Fiesta?
Inasemekana pia kuwa usumbufu mkubwa aliwapa Fela wa Yamoto na msanii Wakazi kwenye recording ya video zao kwenye nyimbo walizomshirikisha….hali inayozua maswali kuliko majibu, kuna tatizo na Ruby au kuna tatizo na wasanii dhidi ya Ruby; hebu tujiulize…..mara ya mwisho nilisikia Fela, Boss wa Yamoto, anasema mimi ukweli nayazuia maneno yangu kwasababu ya Boss Ruge ila ukweli kabisa usinitajie Ruby…… hili tatizo la maslahi alianza nalo mapema au ndo asili yake, kupita kila mahali na kuharibu.
La mwisho kwa leo, huyu dada namkubali sana ana kipaji cha hali ya juu sana na nimeseme hivyo toka mwanzo. Uwezo wake wa kuimba ni mkubwa sana lakini siku zote ili uwe msanii mahiri, uimbaji ni sehemu moja tu ya mengine mengi; bado kuna umahiri wa kuandika, kuishi kwa nidhamu na mengineyo. Leo Ruby ambaye hajawahi kuandika hata mstari mmoja wa nyimbo, anazunguka kila mahali na kulalamikia ubaya wa THT na uongozi wake wa zamani,
Je ataendelea kutumia nyimbo alizotungiwa na uongozi wake wa zamani? Kwa maana nyimbo zote za Ruby kuanzia Na Yule, Forever, Sijutii zimeandikwa (mashairi na melody) na boss wake wa zamani akishirikiana na manguli wa THT, Barnaba na Amini, je Ruby yuko pia tayari kuzikana hizo nyimbo kwani zimetungwa na ‘wanyonyaji'?
Nikijaribu kurudi nyuma miaka kadhaa kidogo, nakumbuka Chidi Benz wakati wa kuanza alifanya bure Fiesta nzima kwa kuomba nafasi. Diamond na Jux kwenye show ya Fiesta Viwanja vya Posta walipanda kama wasanii wachanga wa kutafuta nafasi ya kuonekana. Kwahiyo, sio ajabu kwa wasanii kuomba nafasi ya kujulikana kupitia majukwaa kama Fiesta na mengine.
Inawezekana Ruby ni ‘mkubwa' kwa mtazamo wake…ila kwa mtazamo wangu bado alikuwa anahitaji sana kukua na platform ya Fiesta ingemsaidia kufikia walipofikia wale anaowatazama kwa admiration kama Lady Jaydee ambaye alisimama kwa jeuri na kuweza kukomaa baada ya album ya 5 chini ya Smooth Vibes….sasa huyu hana hata album moja misingi yake ya kusimama ni ipi!!
Ila kwasababu ni suala la maslahi, na maslahi ni yake mwenyewe naona nisiseme sana. Hayo maswali mawili matatu….yatatupa cha kutafakari kwa siku ya leo.