PostGE2025 Tuwe Mabalozi Wa Amani Hatutaki Kuwa Wakimbizi Wa Nchi Yetu Wenyewe

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Ertugrul Bey

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2020
Posts
14,705
Reaction score
30,041
file_0000000055ec71fd87ea5b2484893222 (1).png

My people,​

Si kila anayetaka amani kwasasa hajaumizwa na yale yaliyotokea 29 Oct na yanayoendelea sasa hivi ikiwemo utekaji

Natambua kwa baadhi yenu mnaweza kumuona kila mtaka amani na mpinga harakati za fujo ni adui wa Taifa hili,ukweli ni kwamba kila mpenda amani na mpingaji fujo ni mzalendo namba moja wa Taifa hili utake usitake.

Tanzania haijawahi kukosa amani kwa kipindi kirefu sana,hivyo hutukujua neema ya amani mpaka pale tulipo ipoteza 29 Oct 2025, baada ya kukaa nyumbani kwa siku kadhaa tulionja amani ina faida gani,laiti ile lock down ingedumu kwa wiki moja zaidi hali ingekuwa mbaya sana

Tukubali ukweli kwamba huwezi kuangusha Serikali kwa maandamano yasiyo na kichwa wala miguu,ni mtu asiye tafakari na kuwazua mambo anaweza kuamini hayo

Kitendo cha 9 December watu kutoandamana si kwakuwa ulinzi ulikuwa mkali ila kwasababu wengi wetu tulishaona umuhimu wa amani,hivyo hatukuwa tayar kuumwa mara mbili katika shimo moja,hivyo ndivyo watu werevu wanavyokuwa

Mwisho,guys tuna nchi moja tu na ardhi moja nayo ni Tanzania,tusihadaike na hawa wanaharakati ambao huenda wana nia nzuri lakini njia wanayotumia kuliendea jambo sio sahihi

Wengi wao wapo nje ya Tanzania wana hifadhi za kisiasa,je wewe kikinuka hapa utakwenda kupata hifadhi wapi?

Umeshaiwazia familia yako na ndugu zako?

Amani ni jambo la msingi sana hivyo tusiipoteze,tujifunze kutoka nchi nyingine jinsi wanavvyoitafuta amani,amani ndio uhai na tunu ya taifa hili

Hakuna amani hakuna Tanzania

Binafsi nitakuwa balozi wa amani mpaka tar 31 Dec nikipost mantra ya :

Mwananchi kuilinda Tanzania ni jukumu lako

epuka kuichoma nchi yako

Mungu ibariki Afrika na Mungu ibariki Tanzania

Ni hayo tu!
 
Tupate haki kwanza hatutaki amani ya kinafiki
Toka lini ulaghai kwenye chaguzi, utekaji na mauaji, ufisadi, nepotism katika Taifa vikazaa amani

Amani ni muhimu zaidi
Lakini tukomeshe uhuni unaoondosha amani yetu
Naipenda Tanganyika, naipenda haki ambayo itanipa amani
 
Mimi siwezi poteza muda kuombea amani wakati muondoa amani yupo ikulu,huyo ndo aombee amanHatujamalizana naye,asijidanganye

Samia muuaji
Mkipanga maandamano yasiyo ya amani watu wanakosa amani

Mkitulia amani inarudi kwa watu so hapo nani anaondoa amani ya watu unavyoona?
 
View attachment 3513801

My people,​

Si kila anayetaka amani kwasasa hajaumizwa na yale yaliyotokea 29 Oct na yanayoendelea sasa hivi ikiwemo utekaji

Natambua kwa baadhi yenu mnaweza kumuona kila mtaka amani na mpinga harakati za fujo ni adui wa Taifa hili,ukweli ni kwamba kila mpenda amani na mpingaji fujo ni mzalendo namba moja wa Taifa hili utake usitake.

Tanzania haijawahi kukosa amani kwa kipindi kirefu sana,hivyo hutukujua neema ya amani mpaka pale tulipo ipoteza 29 Oct 2025, baada ya kukaa nyumbani kwa siku kadhaa tulionja amani ina faida gani,laiti ile lock down ingedumu kwa wiki moja zaidi hali ingekuwa mbaya sana

Tukubali ukweli kwamba huwezi kuangusha Serikali kwa maandamano yasiyo na kichwa wala miguu,ni mtu asiye tafakari na kuwazua mambo anaweza kuamini hayo

Kitendo cha 9 December watu kutoandamana si kwakuwa ulinzi ulikuwa mkali ila kwasababu wengi wetu tulishaona umuhimu wa amani,hivyo hatukuwa tayar kuumwa mara mbili katika shimo moja,hivyo ndivyo watu werevu wanavyokuwa

Mwisho,guys tuna nchi moja tu na ardhi moja nayo ni Tanzania,tusihadaike na hawa wanaharakati ambao huenda wana nia nzuri lakini njia wanayotumia kuliendea jambo sio sahihi

Wengi wao wapo nje ya Tanzania wana hifadhi za kisiasa,je wewe kikinuka hapa utakwenda kupata hifadhi wapi?

Umeshaiwazia familia yako na ndugu zako?

Amani ni jambo la msingi sana hivyo tusiipoteze,tujifunze kutoka nchi nyingine jinsi wanavvyoitafuta amani,amani ndio uhai na tunu ya taifa hili

Hakuna amani hakuna Tanzania

Binafsi nitakuwa balozi wa amani mpaka tar 31 Dec nikipost mantra ya :

Mwananchi kuilinda Tanzania ni jukumu lako

epuka kuichoma nchi yako

Mungu inabariki Afrika na Mungu ibariki Tanzania

Ni hayo tu!
Huu ndio uzi bora mwezi huu.
 
Samuya anaongoza nchi kwa mtutu wa bunduki, % kubwa ya wananchi hawamtaki!.
Bila ulinzi mkali jana maandamano yangeweka historia kwa wingi wa watu tz!.
 
Mkipanga maandamano yasiyo ya amani watu wanakosa amani

Mkitulia amani inarudi kwa watu so hapo nani anaondoa amani ya watu unavyoona?
Amani haipo,nishakuambia huo uchawa wako uko ukingoni, na kwa taarifa yako Samia hatoboi 2026 ,huo ndo ukomo wake wa kuitawala Tanganyika.

Kaa una jiandaa kisaikolojia ,utajua kufa kiholo
 
Hakuna amani katikati ya ulaghai kwenye chaguzi, utekaji na mauaji, ufisadi na nepotism
serikali iwajibike kutoa haki, amani automatic itakuwapo
 
Samuya anaongoza nchi kwa mtutu wa bunduki, % kubwa ya wananchi hawamtaki!.
Bila ulinzi mkali jana maandamano yangeweka historia kwa wingi wa watu tz!.
Hata tarehe 29 ulinzi mkali ulikuwepo lakini mlitoka na yote kwa kuwa hamkujua mtaenda kukutana na nguvu ipi? Nyie mlikariri itakuwa kama Kenya tu watatumia mabomu ya machozi na maji ya kuwasha ndo maana mkapaka dawa za meno machoni

Huku mkitembea na slogan ya Kinjeketile Mange jeshi lipo pamoja na sisi

Mkawaponza ndugu zetu wakauliwa hii dhambi mtaibeba milele

Haya ya tarehe 9 raia wamepata somo na akili zao zimeanza kufunguka mdogo mdogo kwa kuwa aware kwenye hizi issues
 
Hakuna amani katikati ya ulaghai kwenye chaguzi, utekaji na mauaji, ufisadi na nepotism
serikali iwajibike kutoa haki, amani automatic itakuwapo
Kama hamuwapi mda wa kuwajibika watawajibika vipi sasa??
 
Amani haipo,nishakuambia huo uchawa wako uko ukingoni, na kwa taarifa yako Samia hatoboi 2026 ,huo ndo ukomo wake wa kuitawala Tanganyika.

Kaa una jiandaa kisaikolojia ,utajua kufa kiholo
Mungu akipanga atoboe atatoboa tu though mi sio fan wake

Pia asipotoboa sawa tu kwa sababu sifaidiki na chochote directly kutoka kwake
 
Kama hamuwapi mda wa kuwajibika watawajibika vipi sasa??
Yaani tuwape muda wa kuacha kuteka na kuuwa holela, tuwape muda wa kuacha kuiba kura na kuhujumu uchaguzi, tuwape muda wa kuacha ufisadi na upendeleo.
Hivi kweli wewe unaamini watu waliopiga kura wanafika milion 32+ na Samia akapata kura 31 m?
 
View attachment 3513801

My people,​

Si kila anayetaka amani kwasasa hajaumizwa na yale yaliyotokea 29 Oct na yanayoendelea sasa hivi ikiwemo utekaji

Natambua kwa baadhi yenu mnaweza kumuona kila mtaka amani na mpinga harakati za fujo ni adui wa Taifa hili,ukweli ni kwamba kila mpenda amani na mpingaji fujo ni mzalendo namba moja wa Taifa hili utake usitake.

Tanzania haijawahi kukosa amani kwa kipindi kirefu sana,hivyo hutukujua neema ya amani mpaka pale tulipo ipoteza 29 Oct 2025, baada ya kukaa nyumbani kwa siku kadhaa tulionja amani ina faida gani,laiti ile lock down ingedumu kwa wiki moja zaidi hali ingekuwa mbaya sana

Tukubali ukweli kwamba huwezi kuangusha Serikali kwa maandamano yasiyo na kichwa wala miguu,ni mtu asiye tafakari na kuwazua mambo anaweza kuamini hayo

Kitendo cha 9 December watu kutoandamana si kwakuwa ulinzi ulikuwa mkali ila kwasababu wengi wetu tulishaona umuhimu wa amani,hivyo hatukuwa tayar kuumwa mara mbili katika shimo moja,hivyo ndivyo watu werevu wanavyokuwa

Mwisho,guys tuna nchi moja tu na ardhi moja nayo ni Tanzania,tusihadaike na hawa wanaharakati ambao huenda wana nia nzuri lakini njia wanayotumia kuliendea jambo sio sahihi

Wengi wao wapo nje ya Tanzania wana hifadhi za kisiasa,je wewe kikinuka hapa utakwenda kupata hifadhi wapi?

Umeshaiwazia familia yako na ndugu zako?

Amani ni jambo la msingi sana hivyo tusiipoteze,tujifunze kutoka nchi nyingine jinsi wanavvyoitafuta amani,amani ndio uhai na tunu ya taifa hili

Hakuna amani hakuna Tanzania

Binafsi nitakuwa balozi wa amani mpaka tar 31 Dec nikipost mantra ya :

Mwananchi kuilinda Tanzania ni jukumu lako

epuka kuichoma nchi yako

Mungu ibariki Afrika na Mungu ibariki Tanzania

Ni hayo tu!
So haki haina umuhimu? Kama hakuna haki hiyo hamani ni ya upande mmoja
 
Hizi propaganda za kuwa na amani tukificha maovu ni ujinga
Hatupingi kufichua maovu,tufichue lakini huku tukitafuta namna bora ya kuyaendea mambo
Tuipe muda serikali wanasema usiku wa deni haukawii, Serikali ina deni la kuwapa watanzania katiba

Tujipe muda
 
Wewe si ndo ulinifuata na kunitisha eti utaniua kwa kuhamasisha maandamano
Active Boqin Refiner celix Reviser

Huyu mtu anajaribu kunichafua na nadhani mmeona wenyewe nawaomba sana wakuu awaoneshe huo ujumbe niliomtisha hapa

Sijawahi kuwa na conversation nae sehemu yoyote ile hii tabia mkiiacha itatuletea tabu kwa sababu kuna watu wengi najuana nao nje ya hapa mnadhani watanifikiriaje?

Naomba akishindwa kuleta uthibitisho mumpige BAN ili kukomesha tabia hii
Maxence Melo
Wand
 
Back
Top Bottom