Tuwe makini kuhusu wanaotoa mawazo ya Serikali ya Tanganyika, tutaletewa kiini macho kutuhadaa tu

Kama taifa kuna mambo yanatudharirisha sana. Huu mjadala kunapotokea pande mbili zinabishana , lazima anayeufuatilia atajiuliza sana kuhusu utimamu wa akili wa upande mwingine hadi kuwa na mfumo wa aina hii na bado unakuta wanaona ni sawa na wengine wanatetea.

Kuna haja ya kufanyika ustaarabu ili angalau kupunguziana kudharirika.

Nyakati zinabadilika, lazima pia ifanyike namna mifumo ibadilike.

Nikionacho mimi, huko tuendapo msijeshangaa Serikali ya tatu ikarudishwa lakini ikawa na hadhi ya Teritory tu huku wananchi wake wakiruhusuwa kuteuliwa na kugombea nafasi za Jamhuri lakini ikawekwa sheria ya kutoruhusu wananchi hao kushiriki kupuga kura ya kuchagua viongozi wa Jamhuri.

Huku wale walio chini ya serikali nyingine ndiyo wakiwa na mamlaka hayo ya kupiga kura kuchagua viongozi wa Jamhuri.

Mtu anaweza kuona haiwezekani, lakini kama tuna aina hii ya Jamhuri kwanini hili lingine lisiwezekane?

Nawaza maana waheshimiwa nakutana nao sana na ndo wanawapa kina Manara waseme nini

Maandiko yangu yazingatiwe yaweza fufuliwa thread hii mwaka hata 2050

Nitaweka video ya hawa vilaza later

Britanicca
Dah 2050 ni parefu. Kina adriz Al-mukheef Jagina ina Malaria 2 Dogo The Icebreaker sijdah zao zitakuwa zimeshaoza makaburini wakisubiria kwa hamu bila matumaini kubadilika na kuwa miarabu.
 
Kama taifa kuna mambo yanatudharirisha sana. Huu mjadala kunapotokea pande mbili zinabishana , lazima anayeufuatilia atajiuliza sana kuhusu utimamu wa akili wa upande mwingine hadi kuwa na mfumo wa aina hii na bado unakuta wanaona ni sawa na wengine wanatetea.

Kuna haja ya kufanyika ustaarabu ili angalau kupunguziana kudharirika.

Nyakati zinabadilika, lazima pia ifanyike namna mifumo ibadilike.

Nikionacho mimi, huko tuendapo msijeshangaa Serikali ya tatu ikarudishwa lakini ikawa na hadhi ya Teritory tu huku wananchi wake wakiruhusuwa kuteuliwa na kugombea nafasi za Jamhuri lakini ikawekwa sheria ya kutoruhusu wananchi hao kushiriki kupuga kura ya kuchagua viongozi wa Jamhuri.

Huku wale walio chini ya serikali nyingine ndiyo wakiwa na mamlaka hayo ya kupiga kura kuchagua viongozi wa Jamhuri.

Mtu anaweza kuona haiwezekani, lakini kama tuna aina hii ya Jamhuri kwanini hili lingine lisiwezekane?

Nawaza maana waheshimiwa nakutana nao sana na ndo wanawapa kina Manara waseme nini

Maandiko yangu yazingatiwe yaweza fufuliwa thread hii mwaka hata 2050

Nitaweka video ya hawa vilaza later

Britanicca
Hoja yako ni ipi hasa.
Umetumia maneno meeengiii, lakini hoja haionekani.

Kwamba serikali ya Tanganyika iwepo ya maonyesho tu; ikiwa kivuli cha hiyo ya Tanzania; wakati serikali ya Zanzibar ikiendelea kuwa na hadhi kubwa hata kuizidi hiyo ya Tanzania?

Assumption yako (zenu) na hao wanaCCM wenzio ndiyo hiyo, mkidhani waTanzania wataendelea kuwavumilia milele.
Itakusaidia sana ukianza kujizoesha maisha bila ya CCM Tanzania.; kwsa maana hilo ndilo litakalofuata.

"Ili Tanzania Ipone, ni lazima CCM ife"

Ukweli huu hamtaki kuukubali, lakini itawabidi tu, maana hakuna namna nyingine.
 
Kwa mfano, ili kulikamilisha hilo wakajiteulia Mkuu wa idara ya usalama Mzanzibar, Mkuu wa majeshi Mzanzibar, IGP Mzanzibar, Jaji Mkuu Mzanzibar na watu wengine muhimu wenye vinasaba na Zanzibar. Tutapinga?
Nimesoma mtiririko wa mawazo yako hadi nilipofikia hii mistari miwili nikajiuliza kama kuna tofauti yoyote na sasa kuhusu hao wakuu uliowataja!

Ninachosema hapa ni kwamba haijalishi chochote kuhusu hao wakuu wanatokea upande gani.
Tena inawezekana hao wa kutokea Zanzibar wakawa nafuu ya hawa waliopo sasa.
 
Ujumbe wako hautafika 2050 ni hapo mwaka 2027 tutakapoanza kutafuta mchakato wa kuandika Katiba mpya ndio yataibuka maana CCM hawajawahi kuwa na akili wanaona wanarekebisha kumbe bado wanakosea. Nchi iwe na rais mmoja, makamu wawili mmoja Tanganyika na mwingine Zanzibar (nafasi ya urais wa zanzibar ifutwe) na Waziri mkuu mmoja tu au Rais mmoja (CinC & Head of State) na Waziri Mkuu wawili wawe (Head of Government) alafu kila nchi ibakie na serikali zake hawa mawaziri wakuu watafanya kazi kama Head of Government ambapo kiuhalisia bado itakuwa Serikali 3. Pia ianzishwe tume ya pamoja ya fedha, makubaliano ya Muungano yapitie na yaandikwe upya na yatakelezwe kikamilifu hatutaki raia wa Zanzibar kuajiriwa Tanganyika kama DC, RC, DAS wala RAS .
 
"Ili Tanzania Ipone, ni lazima CCM ife"

Ukweli huu hamtaki kuukubali, lakini itawabidi tu, maana hakuna namna nyinyingine
I couldn't agree more!!

Unajua mahali hawa viongozi wa juu wa chama walipotufikisha kwa maslahi yao binafsi (UHUNI na ULAFI), hakuna namna bora na yenye baraka, zaidi ya kifo cha CCM.

Hii itafanya watu kutumia akili zao vizuri, nina amini kabisa hata huko ccm wapo watu wenye bongo zenye kuchaji mno sema WAHUNI wameteka nyara chama, hawataki watu wahoji au kuleta mawazo mbadala wa wao wanavyotaka.

Baada ya hapo najua tutakaa chini na kuamua mustakabali wa huu Muungano. Kiukweli huu wa sasa ni aibu hata kuwaelezea watoto wetu. Ni vile hawa WALAFI wanatetea ulaji wao tu, sidhani kama kuna sababu yoyote ya msingi.

HASTA LA VICTORIA SIEMPRE!
 
Nikionacho mimi, huko tuendapo msijeshangaa Serikali ya tatu ikarudishwa lakini ikawa na hadhi ya Teritory tu huku wananchi wake wakiruhusuwa kuteuliwa na kugombea nafasi za Jamhuri lakini ikawekwa sheria ya kutoruhusu wananchi hao kushiriki kupuga kura ya kuchagua viongozi wa Jamhuri.
Kwa nini hamtaki kuheshimu mawazo ya Hayati Mzee wetu Karume? Mawazo ya kuwa na serikali Moja nchi Moja? Wazanzibar walitaka serikali Moja kupitia kwa Hayati Karume, Watanganyika kupitia Hayati Mwalimu Nyerere wakakataa na maelezo haya ni kwa mujibu wa Mwalimu Nyerere mwenyewe.

Kwa hiyo, ninashangaa sana kuona Kuna watu wanawasingizia Wazanzibar kuwa hawataki serikali Moja!!!

Tuheshimu mawazo ya Hayati Karume ya kuwa na serikali Moja nchi Moja. Muda wenyewe ni Sasa!
 
Ujumbe wako hautafika 2050 ni hapo mwaka 2027 tutakapoanza kutafuta mchakato wa kuandika Katiba mpya ndio yataibuka maana CCM hawajawahi kuwa na akili wanaona wanarekebisha kumbe bado wanakosea. Nchi iwe na rais mmoja, makamu wawili mmoja Tanganyika na mwingine Zanzibar (nafasi ya urais wa zanzibar ifutwe) na Waziri mkuu mmoja tu au Rais mmoja (CinC & Head of State) na Waziri Mkuu wawili wawe (Head of Government) alafu kila nchi ibakie na serikali zake hawa mawaziri wakuu watafanya kazi kama Head of Government ambapo kiuhalisia bado itakuwa Serikali 3. Pia ianzishwe tume ya pamoja ya fedha, makubaliano ya Muungano yapitie na yaandikwe upya na yatakelezwe kikamilifu hatutaki raia wa Zanzibar kuajiriwa Tanganyika kama DC, RC, DAS wala RAS .
Asante Una mwelekeo.... lakini bado. Serikali iwe moja nchi moja. Rais Mmoja, makamu mmoja Waziri Mkuu mmoja. Spika mmoja, Jaji Mkuu mmoja, Mwanasheria Mkuu mmoja, Jeshi moja, polisi Moja, Magereza moja nakadhalika na kadhalika moja. Ikiwa hivi kero zote za Muungano zitakwisha!
 
Kwa kifupi Zanzibar ifutwe!
 
lkn pia tuangalia chanzo cha `Tanganyika Nationalism``, ni nini?
 
huu Muungano, ulikuwa sahihi kwa miaka ya zamani
NATAMANI WAZEE WETU WAKUBALI KUWA, KUNA CHANGAMOTO ILI WAZIREKEBISHE, ILA WAKIENDELEA KUAMINISHANA KUWA CHANGAMOTO NI NDOGO NDOGO au HAZIPO; KIPO KIZAZI KITAKACHOKUJA NA KUZITATUA KWA NAMNA KINAONA INAFAA.....NA KUWAACHA WAZEE WATAOKUWEPO MIDOMO WAZI!
 
Issue ya Muungano ni existential risk both kwa Bara na Visiwani. Zanzibar akiumwa mafua lazima Bara tupige chafya. Bara wakikubali muungano ufe, ni a very short sighted political move. Visiwani wakikubali, ni suicide kwao.
Muungano ukivunjika ni hasara zipi watanganyika watapata? Nielimishe tafadhali.
 
Tujtayarishe kupokea wakimbizi kwa kuwa ikivunjika Tanzania basi na Zanzibar nayo haitakuwa na muda. Hakuna Unguja na Pemba nje ya Tanzania.

Chuki ya waPemba dhidi ya waUnguja ni kubwa kuliko ya Wazanzibari dhidi ya waTanganyika
 
Hoja yako ni ipi hasa.
Umetumia maneno meeengiii, lakini hoja haionekani.

Kwamba serikali ya Tanganyika iwepo ya maonyesho tu; ikiwa kivuli cha hiyo ya Tanzania; wakati serikali ya Zanzibar ikiendelea kuwa na hadhi kubwa hata kuizidi hiyo ya Tanzania?

Assumption yako (zenu) na hao wanaCCM wenzio ndiyo hiyo, mkidhani waTanzania wataendelea kuwavumilia milele.
Itakusaidia sana ukianza kujizoesha maisha bila ya CCM Tanzania.; kwsa maana hilo ndilo litakalofuata.

"Ili Tanzania Ipone, ni lazima CCM ife"

Ukweli huu hamtaki kuukubali, lakini itawabidi tu, maana hakuna namna nyingine.
IMG_20260615_130955.jpg

👆🏾 Painful truth
 
Tujtayarishe kupokea wakimbizi kwa kuwa ikivunjika Tanzania basi na Zanzibar nayo haitakuwa na muda. Hakuna Unguja na Pemba nje ya Tanzania.

Chuki ya waPemba dhidi ya waUnguja ni kubwa kuliko ya Wazanzibari dhidi ya waTanganyika
Nimekusoma na kukuelewa vizuri ulichoandika hapa, pamoja na kwamba sioni sababu ya kuendelea na kuinajisi Tanzania kwa kuogopa hayo matokeo unayoyaeleza wewe.

Tuogope "wakimbizi" kuliko kuliangamiza taifa zima?
 
Back
Top Bottom