May Day
JF-Expert Member
- May 18, 2018
- 6,367
- 9,119
Siku chache zilizopita niliwahi kuja na uzi humu kumlaumu Waziri wa habari, ambaye pia ni Dokta pale alipojaribu kumsifia hadharani Mama Mshirikina/Mchawi.
Niaminivyo mimi Mtu yeyote anayeogopa, kukubali au kusifia vitendo vya kishirikina naye pia ni mshirikina.
Hakuna maana yoyote Mtu kujiita muumini wa imani fulani huku kwa upande mwingine anaamini kuna mambo yanawezekana kwa ushirikina/uchawi.
Nimefadhaika zaidi baada ya kumsikia hata Kiongozi wetu Mkuu naye anathibitisha matukio ya kishirikina hadharani, kwamba eti kuna kazi zimewahi kukwamishwa kule Rukwa kwa matendo ya kishirikina.
Nachelea kutumia maneno yasiyo na staha kwa Viongozi, ila kiukweli inasikitisha na ni hatari sana.
Kuwa na taifa linaloamini ujinga na wakati huo huo tunataka kupambana na ujinga haitowezekana kamwe.
Tunaitaka scince na teknolojia huku tunaamini kwenye miujiza, tutabaki tunaimba tu miaka nenda rudi kwamba Wazungu wanatuonea ili hali tunaitegemea teknolojia yao kwa 99%, sijui ya kwetu itakuwa tayari lini.
Kama inatokea Kiongozi wetu ni Mshirikina basi aweke mambo yake hayo kando kwa kipindi chote anachotumikia nafasi yake.