TUWE NA UWAZI KWENYE KILA KITU TUNACHOFANYA KUELEKEA UCHAGUZI 2025

koryo1952

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2023
Posts
1,289
Reaction score
2,199
Ninaomb a sana tuwe na uwazi katika kila jambo tunalolifanya kuelekea uchaguzi wa 2025. Tuige nchi ya jirani yetu ya Kenya ilivyo na uwazi kwenye masuala ya uchaguzi. Leo kule Kenya waombaji wote walioomba nafasi ya Mwenyekiti wa IEBC wanahojiwa mubashara (Live) kupitia luninga ya Citizen. Wananchi wote wanashuhudia maswali wanayoulizwa na majibu yao yanafanyika mubashara sasa hivi.

Naomba tuige mfano wa Kenya. Kila kitu kiwe wazi kwenye masuala ya uchaguzi. Kwa yeyote anayetaka kuangalia usaili wao fungua Citizen TV sasa hivi.
 
Ccm ingekuwa na uwezo wa kushinda kihalali hilo lingewezekana hapa.
 
Mfumo wa vyama vingi CCM walilazimishwa,hawapo tayari kushindana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…