Tuwe wakweli Ikulu ya Dodoma haipendezi, Ukame na hali ya jangwa kunaifanya isiwe na mvuto wa kimuonekano

Tuwe wakweli Ikulu ya Dodoma haipendezi, Ukame na hali ya jangwa kunaifanya isiwe na mvuto wa kimuonekano

Nimeangalia picha na video za Kikao cha Mwisho cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika leo Ikulu cha Chamwino, Dodoma. Picha na video hizo zipo ukurasa rasmi wa Ofisi ya Rais Ikulu IG.

Niseme tu ukweli Ikulu na Chamwino haipendekezi. Ukame wa Dodoma hasa miezi hii unaifanya isiwe na mvuto na muonekano mzuri. Mazingira yake hayavutii.

Sijui wafanye nini. Ila kwa sie wapenda mazingira mazuri tunaziona ikulu za Dar na Arusha ( Ikulu Ndogo) zina mvuto sana tofauti na Ikulu ya Dodoma kutokana na Kijani kingi na miti mizuri kunakopendekezesha sana maeneo yake.

No Reform No Election ✊️ ✌️
View attachment 3405802View attachment 3405803View attachment 3405804View attachment 3405805
Ni ujinga tuu wa Wizara ya Mazingira na Maji pamoja na taasisi zao.

Yaani Saudia Jangwani wanapanda Miti Kwa nini ishindikane Dodoma?

Harafu kule City Centre Kuna Miti safi kabisa iwaje huko Ikulu na Nje ya Mji wasipande Miti?

Kwa nini isiwe lazima Kila mwenye nyumba iliyopangwa apande moto hata 5?

Uzembe wa kimamlaka hasa ofisi ya VP inayosimamia mazingira.

Pia soma hapa (1) Saudia Kupanda Miti Bilioni 100 Jangwani .Je Kupanda Miti Dodoma tunahitaji wafadhili? | JamiiForums Saudia Kupanda Miti Bilioni 100 Jangwani .Je Kupanda Miti Dodoma tunahitaji wafadhili?
 
unajua usidhanie kuwa uwazavyo wewe ni sahihi,na wala hujui kuwa hapo ikulu kuna mipango ipi ya upandaji miti na maua,jifunze kutafiti kwanza
Mipango sio uhalisia na matumizi.

Sie tunataka kuona.

Ikulu imejengwa lini?

Kwa nini miti haikuoandwa na kukuzwa wakati ikulu inajengwa?
 
Kwa akili za kipumbavu kama zako na mleta uzi msingeweza kuibadili Dubai iwe ilivyo hivi sasa. Dodoma ina ukame kama wa Dubai? Mngeshauri serikali iongeze nguvu kwenye kupanda miti na kubadili mazingira badala ya kuandika uzi wa kulalamika kama vile nyie ni warundi. Wewe kama msomi unaandika mavi hapa JF vipi wasiokuwa wasomi?
Dubai UAE hawajabadili Dodoma yao, Dubai UAE wameiendeleza Dar es salaam yao kuwa bora zaidi.

Mfano wako unaonesha huelewi unachoandika.
 
Hizo safari zilianza zamani tuu

Bunge -Dodoma
Wizara- Dar

Sasa tukaamua vyote vikae pamoja Dodoma.

Dodoma haiwezikuwa white elephant, na mpaka sasahivi sio
Kwani ujinga ukiwa umeanza zamani ndiyo unakuwa si ujinga?

Bunge liliwahi kuwa Dodoma kabla mji mkuu haujahamishwa kwenda Dodoma?
 
I can bet a mortgage vyoo vya humo ndani vinanuka sijui navyo watasema ukame? Uchafu na kutozingatia mazingira ni tabia ya watanzania. Ikulu za arabuni huko ambako ni jangwani kabisa zina kijani kuliko hiyo ya DOM.

Aliyechora ramani ya hii ikulu anahitaji viboko 100 hadharani ikulu gani ka gereza.
 
Hoja yangu ni zaidi ya kupendeza.

Zoezi zima la kuhamisha mji mkuu ilikuwa ni kutumia pesa nyingi kutatua tatizo ambalo halipo kwa nchi yenye matatizo mengi yaliyopo ambayo hayajatatuliwa.
Sio kila jambo lazima lifuate formalities mambo mengine inabidi yafanyike bila kubembelezana kuhamia dodoma kwa staili ya magufuli alikuwa sahii
 
Dar es salaam tayari ukishakuwa mji mkuu mzuri tu.

Kulikuwa hakuna sababu ya kuhamisha mji mkuu.

Kama kulikiwa na congestion wangepanga mji mpya wa serikali Kigamboni.

Sasa hivi safari nyingi za Dar Dodoma zimetugharimu sana.

..wamlaumu Mzee Hafizi kwa muonekano mbaya wa ikulu yetu.

..mbona fest ledi Melania anajituma kuhakikisha White House inapendeza?

..wamuandalie Mzee Hafizi ziara akajifunze.

Cc Gagnija
 
I can bet a mortgage vyoo vya humo ndani vinanuka sijui navyo watasema ukame? Uchafu na kutozingatia mazingira ni tabia ya watanzania. Ikulu za arabuni huko ambako ni jangwani kabisa zina kijani kuliko hiyo ya DOM.

Aliyechora ramani ya hii ikulu anahitaji viboko 100 hadharani ikulu gani ka gereza.
Kwanza wake copy na ku paste ikulu ya Wakoloni kana kwamba hatuna wabunifu na wasanifu wa majengo,hovyo kabisa.
 
Sio kila jambo lazima lifuate formalities mambo mengine inabidi yafanyike bila kubembelezana kuhamia dodoma kwa staili ya magufuli alikuwa sahii
Kwanza siongelei formalities, naongelea logic. Naongelea uchumi. Naongelea efficiency. Naongelea oportunity cost.

Halafu siongelei kuhamia Dodoma alikofanya Magufuli, naongwlea wazo oroginal tangu utawala wa Nyerere.

Au hujui kuhamia Dodoma hakuanzisha Magufuli?
 
JPM angekuwepo, maji ya ziwa Victoria yangekuwa tayari yameshaibadilisha Dodoma kuwa ya kijani, na huenda kungekuwa na ziwa la maji Baridi la Kutengenezwa Dodoma.
Huyo ndio alijenga iku ya kukopi na kupaste.

Hiyo huyo ndio aliweka ikulu katikati a makazi ya watu

Hovyo kabisa,onyesha hata sentimita 1 ya maji kwamba mradi ulianza.

By the way inakuaje VP anashindwa kuacha ligacy ya Wizara anazosimamia za mazingira?
 
Kwanza wake copy na ku paste ikulu ya Wakoloni kana kwamba hatuna wabunifu na wasanifu wa majengo,hovyo kabisa.

..hata mimi hili suala lilinizingua.

..kwanini walifanya ikulu ya Dodoma kuwa copy ya Dar Es Salaam?

..pale walikosa ubunifu kwa kweli.
 
..hata mimi hili suala lilinizingua.

..kwanini walifanya ikulu ya Dodoma kuwa copy ya Dar Es Salaam?

..pale walikosa ubunifu kwa kweli.
Ujinga tuu wa kina Mwendazake wa kutoshirikisha mawazo ya wengine

Kwanza Bora tujenge ikulu nyingine Mpya yenye ramani yetu sio hiyo ya kukopi.
 
Back
Top Bottom