Tuwe wakweli kocha Nabi hana mbinu za mechi za kimataifa. Rekodi zinaongea.

Kamgomoli

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2018
Posts
1,896
Reaction score
4,058
Baada ya mechi 2 za Yanga na Al hilal nikaona nisubiri mechi ya leo ili nifanye hitimisho km kweli Nabi ana uwezo wa kuiwezesha Yanga kufanya vzr kimataifa au laa. Nisema tu Yanga wasitarajie maajabu yoyote kutoka kwa huyu Profesa aliye-specialize kwenye kushinda mechi za ndani. Hebu tuache rekodi ziongee kwa kutazama mechi za kimataifa ambazo Nabi kaiongoza Yanga.
1.Yanga VS Rivers United 0:1 lose
2.Rivers United VS Yanga 1:0 lose
3.Yanga VS Al hilal 1:1 draw
4.Al hilal VS Yanga 1:0 lose
5.Yanga VS Club Africain 0:0 draw
Next.....??? Mimi Natabiri kipigo.

Mechi za kirafiki kimataifa Yanga Day.
6.Yanga VS Zanaco 1:2 lose
7.Yanga VS Vipers. 0:2 lose

Kati ya mechi saba Nabi kashinda mechi moja tu tena kwa mbinde. Hii ni rekodi mbaya kabisa kwa timu kubwa km Yanga.Mpaka hapo kwanini nisihitimishe kuwa huyu ni profesa wa mechi za ndani pekee?

Jana niliandika uzi kuonya km Yanga watacheza vile walivyocheza dhidi ya Al hilal kwa staili ya polepole( slow),hawatoweza kamwe kumfunga Club Africain. Cha ajabu leo wamecheza vile vile hali iliyofanya kutotengeneza shambulizi lolote la maana kwa dk zote 90.

Yanga wanacheza kwa kueleweka kuanzia kwa Diara hadi katikati ya uwanja. Baada ya hapo kila mtu anaanza kucheza anavyojua. Huoni timu ikicheza kwa mpangilio maalamu. Wakuamua kupiga chenga atapiga, wakuamua kukimbia na mpira atakimbia nao.Wa kupiga juu atapiga. Hapo ndipo nilipohitimisha kwa kusema Nabi hana uwezo wa mechi za kimataifa.

Sisemi afukuzwe ila Yanga waangalie malengo yao. Je malengo ni kuendelea kushinda ligi kuu pekee au wanataka kumfuata mtani wao kule aliko? Kazi ni kwao wenyewe wataamua.

Ni hayo tu kwa sasa.
 
Upo sahihi kabisa
Nabi mbinu za kimataifa Hana
Ila mkuu hujaweka mechi ya zalani .
Kwa nn Nabi anapenda kumuanzisha kisinda ,
Kisinda kaisha anatakiwa asugue banchi tuu
 
Bro umesema kila kitu cha kuongeza ni kwamba Mpira wa kocha Nabi unatabirika kirahisi. Hivyo makocha wa team pinzani wakishamsoma hana Plan B.
 
Kabisa mkuu hapo umepigilia msumali.
 
Uongozi wa yanga utamfukuza Nabi kabla ya mechi ya marudiano ili wapunguze lawama za mashabiki
 
Hawa utopolo ovyo kabisa, sasa tutaanza kuamini huku kwenye NBC league wanashinda kwa ujanja ujanja wa kuhonga marefa na wachezaji wa timu pinzani
 
Uongozi wa yanga utamfukuza Nabi kabla ya mechi ya marudiano ili wapunguze lawama za mashabiki
Kwa sasa anastaili kabisa kufukuzwa kwani hana jipya tena. Na sizani km hata yeye atalaumu. Uongozi umempa muda wa kutosha sana.
 
Baada ya mechi 2 za Yanga na Al hilal nikaona nisubiri mechi ya leo ili nifanye hitimisho km kweli Nabi ana uwezo wa kuiwezesha Yanga kufanya vzr kimataifa au laa. Nisema tu Yanga wasitarajie maajabu yoyote kutoka kwa huyu Profesa aliye-specialize kwenye kushinda mechi za ndani. Hebu tuache rekodi ziongee kwa kutazama mechi za kimataifa ambazo Nabi kaiongoza Yanga.
1.Yanga VS plateu 0:1 lose
2.Plateu VS Yanga 1:0 lose
3.Yanga VS Al hilal 1:1 draw
4.Al hilal VS Yanga 1:0 lose
5.Yanga VS Club Africain 0:0 draw
Next.....??? Mimi Natabiri kipigo.

Mechi za kirafiki kimataifa Yanga Day.
6.Yanga VS Zanaco 1:2 lose
7.Yanga VS Vipers. 0:2 lose

Kati ya mechi saba Nabi kashinda mechi moja tu tena kwa mbinde. Hii ni rekodi mbaya kabisa kwa timu kubwa km Yanga.Mpaka hapo kwanini nisihitimishe kuwa huyu ni profesa wa mechi za ndani pekee?

Jana niliandika uzi kuonya km Yanga watacheza vile walivyocheza dhidi ya Al hilal kwa staili ya polepole( slow),hawatoweza kamwe kumfunga Club Africain. Cha ajabu leo wamecheza vile vile hali iliyofanya kutotengeneza shambulizi lolote la maana kwa dk zote 90.

Yanga wanacheza kwa kueleweka kuanzia kwa Diara hadi katikati ya uwanja. Baada ya hapo kila mtu anaanza kucheza anavyojua. Huoni timu ikicheza kwa mpangilio maalamu. Wakuamua kupiga chenga atapiga, wakuamua kukimbia na mpira atakimbia nao.Wa kupiga juu atapiga. Hapo ndipo nilipohitimisha kwa kusema Nabi hana uwezo wa mechi za kimataifa.

Sisemi afukuzwe ila Yanga waangalie malengo yao. Je malengo ni kuendelea kushinda ligi kuu pekee au wanataka kumfuata mtani wao kule aliko? Kazi ni kwao wenyewe wataamua.

Ni hayo tu kwa sasa.
Sio kimataifa tu,hata hapa ndani kama si bahasha na jopo la wachawi kama wote mngeumbuka tu hata mbele ya KMC
 
Simba ni mwanaume aliyeanua kutafuta furaha nje ya nyumba yakw yaani michepuko,na yanga kaamua kutafuta furaha ndani ya ndoa
 
Baada ya mechi 2 za Yanga na Al hilal nikaona nisubiri mechi ya leo ili nifanye hitimisho km kweli Nabi ana uwezo wa kuiwezesha Yanga kufanya vzr kimataifa au laa. Nisema tu Yanga wasitarajie maajabu yoyote kutoka kwa huyu Profesa aliye-specialize kwenye kushinda mechi za ndani. Hebu tuache rekodi ziongee kwa kutazama mechi za kimataifa ambazo Nabi kaiongoza Yanga.
1.Yanga VS plateu 0:1 lose
2.Plateu VS Yanga 1:0 lose
3.Yanga VS Al hilal 1:1 draw
4.Al hilal VS Yanga 1:0 lose
5.Yanga VS Club Africain 0:0 draw
Next.....??? Mimi Natabiri kipigo.

Mechi za kirafiki kimataifa Yanga Day.
6.Yanga VS Zanaco 1:2 lose
7.Yanga VS Vipers. 0:2 lose

Kati ya mechi saba Nabi kashinda mechi moja tu tena kwa mbinde. Hii ni rekodi mbaya kabisa kwa timu kubwa km Yanga.Mpaka hapo kwanini nisihitimishe kuwa huyu ni profesa wa mechi za ndani pekee?

Jana niliandika uzi kuonya km Yanga watacheza vile walivyocheza dhidi ya Al hilal kwa staili ya polepole( slow),hawatoweza kamwe kumfunga Club Africain. Cha ajabu leo wamecheza vile vile hali iliyofanya kutotengeneza shambulizi lolote la maana kwa dk zote 90.

Yanga wanacheza kwa kueleweka kuanzia kwa Diara hadi katikati ya uwanja. Baada ya hapo kila mtu anaanza kucheza anavyojua. Huoni timu ikicheza kwa mpangilio maalamu. Wakuamua kupiga chenga atapiga, wakuamua kukimbia na mpira atakimbia nao.Wa kupiga juu atapiga. Hapo ndipo nilipohitimisha kwa kusema Nabi hana uwezo wa mechi za kimataifa.

Sisemi afukuzwe ila Yanga waangalie malengo yao. Je malengo ni kuendelea kushinda ligi kuu pekee au wanataka kumfuata mtani wao kule aliko? Kazi ni kwao wenyewe wataamua.

Ni hayo tu kwa sasa.
Hoja yako ina mashiko! Ila umechemka sehemu ndogo sana, kwa kutoweka matokeo ya mechi zake mbili dhidi ya Zalan! Baada ya kuchapia hapo kwenye Rivers United (wewe ukaweka Plateu), ulitakiwa pia uitaje hiyo timu ya Zalan!

Hivyo usiwe na double standard.
 
Amekujibu kuwa zalan sii timu ni kikundi cha wakimbizi
 
Hizo ni hasira tu na zote mnamuangushia Nabi... Bado ana nafasi ya kuunda kikosi next time kwa mechi za kimataifa. Kosa lake ni kuwaanzisha kina Kisinda... akiambiwa atajirekebisha.
 
Mashabiki wa Yanga mnatoa lawama sasa hivi, lakini wakati ule uongozi ulipovunja pre season tour mlishangilia bila ya kujua athari ya kuzikosa mechi za kirafiki katika mazingira tofauti.

Mnacheza na Mbuni Fc mkitegemea kupata nini hapo..? Mnashinda katika mazingira yenye utata, badala ya kukemea mnapita kifua mbele kujitapa. Madhara yake ndo haya sasa, ndo mnalia sasa kimataifa..

Sasa mmemsajili Aziz Ki kwa gharama kubwa, ili aje kucheza Ihefu..?
 
Back
Top Bottom