Tuwe wakweli kwa hali ya kimpira tuliyo nayo Tanzania, kuajiri kocha MGENI ni kumzawadia mihela ya bure tu

Tuwe wakweli kwa hali ya kimpira tuliyo nayo Tanzania, kuajiri kocha MGENI ni kumzawadia mihela ya bure tu

Ndugu mzabzab hawa tulio nao hata tungewajali vipi hata kama tukisema Kila mtu asafiri na jet yake na kiwango Cha kulipwa ajitajie mwenyewe haitasaidia Kwa sababu uwezo wao umeishia hapo walipofikia ndio maana tumeishia kuwa dalaja la kupandia wenzetu.

Ni uzwazwa uliopindukia kukazana kuingia gharama kubwa kuajiri makocha wenye CV kubwa na wanaolipwa hela nyingi waje wafundishe hapa.

Ni sawa na kununua mitambo mikubwa sana ya kisasa wakati una umeme hafifu alafu mitambo ikianza kusumbua uanze kulaumu mafundimitambo, nakuhakikishia utafukuza na kufukuza as long as hutatatua tatizo la udhaifu wa umeme wako hutatatua tatizo.

Naomba nieleweke siwalaumu wachezaji wetu naamini wanajituma na huenda wanatoa %100 ya uwezo wao but hivyo ndivyo tulivyowaandaa.

Kama tuna nia ya kuleta mabadiliko ya kweli ni lazima tubadilishe namna ya kuwaandaa watu wetu. Na hili linaihitaji wizara pamoja na TFF kukaa pamoja na kupeana majukumu ya namna ya kutengeneza kizazi kipya cha ushindani na weledi.
Naweza sema with full confidence kuwa wewe unajua mpira. Hongera.
Ishu ni sisi kushindwa kuanda wachezaji wetu.

Mkakati unataikwa kuwa endelevu sio ujinga wa taifa stars maboresho 🤣🤣🤣 wat a load of nonsense.

Shule zinatakiwa kuwa na qualified coaches ambao watafundisha mpira with the appropriate age category drills. So unafindisha mtoto wa miaka 14 kama unafundi jitu la miaka 26.

Kozi kila leo tunaona zinaendeshwa so makocha wapo so high time hao makocha ndio waende kufundisha huko mashuleni ili sasa tupate wachezaji wenye ubora. Haya na haya mambo ya kuchanguana kwa ajili ni mtoto wa mjomba tuache. Mara sijui mtoto atoe laki tatu ndio achaguliwe hapana
 
Kama mtu Kama Karia anawekwa kuongoza mpira unategemea nn? Mi nilishaacha kuangalia mpira WA Tanzania zamani Sana.

Mabadiliko yaanze Kwa Raisi WA shirikisho na yeye atoke waje watu wenye weledi WA kuongoza kile chombo, sio vibaya hata tukiajiri foreigner ambaye CV yake inajitosheleza au hata tukimpa kazi ya Consultancy kusaidia soka letu.

Toka jamaa Aingie madarakani hakuna kipya Taifa Starz ilichofanya. Wao wanakazana kufaidisha matumbo Yao Tu huku soka letu likididimia.
wewe tunafanana mtazamo. Tenga angalau alijitahidi huyu Karai hana upepo wa mafanikio kwa Taifa Stars wala weledi wa kuongoza mpira wetu sijui kwanini wadau wako kimya
 
Umeongea ukweli mkuu. Napenda kufuatilia mechi nyingi za Burkina Faso; mfano (CHAN & Africa cup); nakumbuka 2016 &2017 Tanzania tuliwafunga Home &Away.
Ila leo hii wapo mbali sana kwenye rank ya Afrika na Dunia kwa jumla.
Tufanye leo(2022) tucheze nao mechi yeyote matokeo yatakayotokea itakuwa aibu kwa taifa.
Tatizo Tanzania tunaishi kimazoea sana ndio maana hutupigi hatua kwenye soka.
Uwekezaji kwenye academy za soka na michezo ya mitashumta/umiseta huko kunamadudu balaa, ikitwa timu ya kata shida, timu ya mkoa shida( yaani watu wanaweka watoto na ndugu zao).

Ukweli kama taifa itachukua miongo ama karne kadhaa kusogea/ kufanya vizuri kwenye soka.
Ushauri; tuweke mambo wazi kama academy zichukue watoto wenye uwezo na si kuangalia huyu ni wanani na anatoka wapi.
Michezo ya mitashumta/ umiseta. Ifanyike kwa ufanisi na si ilimradi kutimiza ratiba, na watoto wachaguliwe kwa kigezo cha uwezo na si huyu ni Mtoto wa kiongozi au wamwalimu flani.
Hitimisho. Tukizingatia haya ndani ya miaka 5- 7. Tutapiga hatua kwenye soka.
 
Ndugu Gmarra inaumiza sana waliopewa dhamana wanatupiga porojo mwanzo mwisho wakati uhalisia unajieleza. Jana nilimsikia katibu mkuu wa wizara anasema tumefungwa na Uganda lakini hatujapoteza mashindano. Eti anajisifu hii ni jamhuri ya wapambanaji tutapambana mpaka kieleweke. Ukimsikiliza kishabiki ni maneno matamu sana ila ukimsikiliza kiuhalisia unakata tamaa, kama mwenye dhamana ya kuufanyia reform mpira wetu haoni tatizo tunaloona wakereketwa ata cjui nisemeje!
 
Back
Top Bottom