Comoros, Mauritius, Cape Verde na Sao Tome vyote ni visiwa huru na havina kitisho cha usalama kwa mataifa yaliyo karibu yake.
Si kweli mkuu, unaona havina kitisho cha usalama kutokana na hali tulivu ya kisiasa ya sasa. Lakini unapojiandaa na vita basi wakati wa amani ndiyo wakati sahihi kupanga mipango yote.
Hivyo unavyoviona salama hii leo vinaweza tumika na kuwa kuwa ‘decisive factor’ wakati wa vita.
Leo hii Ufaransa ana kisiwa cha Mayotte, ambacho kii karibu na visiwa ulivyovitaja hiyo ina maana ya kuwa lolote likitokea Ufaransa ana pa kuanzia.
Kwa kulijua hilo Comoro wanadai kisiwa hiko kila leo.
Hapo Madagascar India wanajenga moja ya kambi kubwa ya kijeshi, vipi hilo bado halikai kama tishio mkuu?
Uchina mbali na kuwa na nchi kubwa lakini bado anadai Taiwan, na anajenga visiwa kwenye bahari ya kusini ya china suala ambalo linazua mgogoro na nchi zote ambazo bahari hiyo inapita. yote ni kwa sababu za kiusalama.
Urusi walitaka eneo la Kalinigrad toka kwa Ujerumani ilhali limejitenga kabisa zaidi ya maili 400 toka Urusi (achilia mbali Zanzibar iliyo maili 65 tu toka Dar es salaam) na nchi yao hawakuwa wajinga, walilitaka kimkakati na moja ya mkakati huo ni kupata ‘access’ ya Bahari ya Baltic na kuwa karibu na Ulaya Magharibi.
Ikumbuke ‘Monroe Doctrine’ ya Marekani iliyoweka wazi hawataki taifa lolote kujenga ushawishi katika amerika kusini, kati na visiwa vya Caribbean.
Ukitaka upate picha sahihi usiangalia kwa jicho la sasa tengeneza “worst case scenario”.
Turudi hapa nyumbani
Zanzibar ingekuwa huru na katika hali ya kisiasa ilivyokuwa hatari ingekuwa kwetu sisi waTanganyika.
Uwepo wa Zanzibar maili 65 toka kwenye fukwe za jiji letu kuu la kibiashara na ikulu ya rais wetu (ilivyokuwa) si suala dogo kiusalama.
Pata picha tungekuwa na adui na nchi nyingine, adui angepata urahisi kuitumia Zanzibar kama sehemu ya kuanzisha mashambulizi yake kwetu (umbali ni kitu muhimu sana).
Vilevile wale ambao hawakukubaliana na serikali ingelikuwa ni rahisi wao kufanya Oparesheni zao tokea Zanzibar.
Ni kama tulivyoratibu Oparesheni ya kumtoa nduli Iddi Amini Kwa kushirikiana na Waganda wenyewe wakiwa hapa nchini.