Tuwe wakweli kwamba Nyerere alifanya vibaya kuua Uhuru wa Tanganyika na kugawa rasilimali za Watanganyika kwa Wazanzibari wasiotaka vyao kuguswa

Huo si muungano ni uvamizi wa Tanganyika kwa Zanzibar chini ya Laanatullahi Nyerere
Zanzibar hakuna Madini, Mazao ya Chakula, Mifugo ya Chakula, Viwanda vya kuzalisha huwa tunawang'ang'ania Nini? Na kuwapa Stahiki za Watanganyika?
 
Mbona Kenya iko salama na Pemba iko karibu.
Mkuu hivi huwa unasoma majibu yangu kabla ya wewe kujibu?
Rejea basi walau aya ya kwanza tu

“…Si kweli mkuu, unaona havina kitisho cha usalama kutokana na hali tulivu ya kisiasa ya sasa. Lakini unapojiandaa na vita basi wakati wa amani ndiyo wakati sahihi kupanga mipango yote…”
 
Nilisoma. Tuseme sijaelewa.
 
Mkuu nimemsikiliza huyu bwana, ila kuna mahali kati ya dakika ya 3:30-4:00 anasema ati kodi ya VAT imepewa jina lake kutokana na kufupisha jina la kanisa katoliki yaani VATICAN. Jambo ambalo halina ukweli.
 
Sikiliza vitabu vya kanisa katoliki vinasema kitu gani


Madai ya huyu bwana nimebaini hayana mashiko japo kwa kiasi kidogo sana nimekubaliana nae.

Amedai Tanzania imejitumbukiza kwenye Ujamaa ili kuwanyima Waislam mali- ni kweli kuwa wakati wa uhuru wengi wa matajiri walikuwa ni waislam sababu waliishi mwambao na shughuli nyingi na mtandao wa kibiashara ulipanuka zaidi mwambao.

Lakini kwa hoja hiyo utaelezeaje ujamaa ulioingizwa kwenye nchi zenye waislam wengi? Na zile zenye Wakristo wengi?

Je, huko kwenye Wakristo wengi ‘Kanisa’ lilitaka kumpora nani mali?


Nchi iliyowahi kuwa ya kijamaaIdadi ya Waislam
Algeria 🇩🇿
98%
Misri 🇪🇬
90%
Libya 🇱🇾
97%

Achilia mbali hapo, vipi kuhusu nchi zenye wakristo wengi? Waliweka ujamaa ili kumkomoa nani?


Nchi iliyowahi kuwa ya kijamaa Idadi ya Wakristo
Angola 🇦🇴
95%
Zimbabwe 🇿🇼 84%
Zambia 🇿🇲
87%


Tafadhali nipe majibu.
 
Nilisoma. Tuseme sijaelewa.
Vizuri.

Nadhani unafahamu hali ya kisiasa ilivyokuwa miaka ya ‘60.

Zanzibar walikuwa wametoka kupata uhuru wa bendera na punde tu Karume akapindua serikali na kujipatia uhuru kamili. Mapinduzi yake yalikumbwa ni vitisho vya kupinduliwa tena toka kwa maadui zake.

Mwaka huohuo Nyerere almanusura apinduliwe katika kile tunachokiita “Dar Army mutiny” na bila usaidizi wa jeshi la Malkia Nyerere asingeendelea kukaa madarakani.

Kwahiyo Nyerere na Karume kila mmoja aliona utawala wake hauko salama hivyo ikaonekana kuwa Muungano ndiyo suluhu.

Kivipi?

Zanzibar ni nchi ndogo sana hivyo ni rahisi kwa anaetaka kuipindua kutimiza azma yake, hivyo waliiunganisha na Tanganyika ili anaetaka kuipindua basi ni lazima akabiliane na Tanganyika (nchi kubwa na yenye uwezo kijeshi).

Kwa Tanganyika mwalimu kuona askari wamemuasi moja ya suluhu ni kuungana na Zanzibar ili waasi wasijeitumia Zanzibar kama ‘stepping stone’ katika mashambulizi yao dhidi ya serikali na ikulu yake.

Kwahiyo kwenye suala hili ilikua ni ‘win-win’ kwamba Zanzibar italinda mapinduzi yake na bara itajihakikishia kuwa waasi hawataitumia Zanzibar kama kichaka chao cha kujifichia.
 
Zanzibar hakuna Madini, Mazao ya Chakula, Mifugo ya Chakula, Viwanda vya kuzalisha huwa tunawang'ang'ania Nini? Na kuwapa Stahiki za Watanganyika?
Sielewi kwa nini mnakuja kutuuwa kila uchaguzi ili kumweka kibaraka wenu?
 
Hajatoa lake moja kichwani mwake yote yametoka kitabu cha kanisa Katoliki. Itakuwa unamsikiliza kwa jaziba au umetumwa
 
Mkuu nimemsikiliza huyu bwana, ila kuna mahali kati ya dakika ya 3:30-4:00 anasema ati kodi ya VAT imepewa jina lake kutokana na kufupisha jina la kanisa katoliki yaani VATICAN. Jambo ambalo halina ukweli.
Tupe ukweli
 
Sijaona faida ya Muungano.....siku nkiwa Rais ntaufutilia mbaaaaliiiiij......!! Jina pendwa la Tanganyika rirudi kwenye raman
 
Ni chuki tu kwa waislamu hakuna chengine
 
Unajua wewe unaropokwa sana. Ili update kitambulisho cha uzanzibari lazima ukao miaka 3 mfululizo. Na wako wengi sana watanganyika wanavyo. Na wanamiliki ardhi na wameajiriwa serikalini wacha zako. Inawezekana unawachukua wazanzibar either wamekutoa bikra na wakakuacha. Tembelea mitaa ya mwakaje, mfenesini, mwache alale utakuta wapo wamanyema, wayao na wamakonde wengi sana. Kiboje, miwani, ndagaa, bumwlbwisudi waruguru wandengereko ndiyo majority kwa 90% vile vile kiboje, kitumba, kidimni, dunga basi majority ni wandengreko, wapogoro, wanyamwezi. Na kuna lsehemu kibao. Mahotelini 90 ni watu wa tanganyika, ukienda beach wamasai kama upo loliondo, wachole wamejaa katikabidara nyeti za ZNZ na.muungano. watu wa kusini ndiyo wamejaa katika biashara za umachinga.Sasa wewe mpuuzi sijui utaka nini unakuja kila leo.na maada za kipuuzi. Muunganobis here to stay kama unakerekera basi tafuta basha
 
Mtu asiyejua kuwaachia urithi hata wanae unamteegemea akuachie nchi salama.
 
Huiwezekani nchi yenye watu 60m ikaungana na nchi yenye watu 1m alafu ikawepo haki sawa kwa wote lazima nchi yenye watu 1m ipate upendeleo na haswa ikiwa nchi hiyo ni kisiwa.
 
Dah umeongea ukweli mtupu saivi Zanzibar watanganyika tele Machinga wote waliofurushwa dar wamehamia zenji na vile vile wapo wale waliohamia wakaishi zenji zaidi ya miaka mitatu wakapata kitambulisho cha mzanzibari wapo tele kuanzia serikalini mpaka huku mitaani na tunaishi nao sijawahi kusikia mtanganyika kabaguliwa.
 
Huiwezekani nchi yenye watu 60m ikaungana na nchi yenye watu 1m alafu ikawepo haki sawa kwa wote lazima nchi yenye watu 1m ipate upendeleo na haswa ikiwa nchi hiyo ni kisiwa.
Ndivyo mnavyodanganyana Kanisani?
 
Rasilimali gani hizo za hao unaowaita Watanganyila zilizogawiwa Zanzibar? Hivi unafahamu kwamba >60% ya Watalii wanaokuja Tanzania wanakuja sababu ya Zanzibar na siyo Bara ? Unajua utalii unachangia kiasi pato la Taifa kwa ujumla?
Watalii wengi wanakuja Tanzania kwa ajili ya Serengeti, Ngorongoro na Mlima Kilimanjaro na sio kwa ajili ya hicho kijiji cha maghofu yaliyopakwa chokaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…