Madai ya huyu bwana nimebaini hayana mashiko japo kwa kiasi kidogo sana nimekubaliana nae.
Amedai Tanzania imejitumbukiza kwenye Ujamaa ili kuwanyima Waislam mali- ni kweli kuwa wakati wa uhuru wengi wa matajiri walikuwa ni waislam sababu waliishi mwambao na shughuli nyingi na mtandao wa kibiashara ulipanuka zaidi mwambao.
Lakini kwa hoja hiyo utaelezeaje ujamaa ulioingizwa kwenye nchi zenye waislam wengi? Na zile zenye Wakristo wengi?
Je, huko kwenye Wakristo wengi ‘Kanisa’ lilitaka kumpora nani mali?
| Nchi iliyowahi kuwa ya kijamaa | Idadi ya Waislam |
| Algeria 🇩🇿 | |
| Misri 🇪🇬 | |
| Libya 🇱🇾 | |
Achilia mbali hapo, vipi kuhusu nchi zenye wakristo wengi? Waliweka ujamaa ili kumkomoa nani?
| Nchi iliyowahi kuwa ya kijamaa | Idadi ya Wakristo |
| Angola 🇦🇴 | |
| Zimbabwe 🇿🇼 | 84% |
| Zambia 🇿🇲 | |
Tafadhali nipe majibu.