Nyerere na sokoine ndio waliowaletea umasikini watz weusi kwa kuwaaminisha umasikini ndio uzalendo na utajiri ni dhambi utajiri ni unyonyaji,akataifisha Mali zao nyingi wengi wakatupa magunia ya pesa wengine wanakimbia Kenya, zambia kukwepa kuwekwa jela sababu ni matajiri.Wachaga wakakimbilia Kenya, Wahindi wakakimbia uingereza, USA,canada nk.Waliobaki wakafilisiwa na kutakiwa waishi kishetani ukikutwa na colgate,sabuni,dola,radio,ukinywa bia nyingi kwa siku,ukila vizuri,ukinunua gari uhujumu uchumi ulikuhusu.
Ashukuriwe mzee ruksa ndie aliyewarudisha wengi nchini na waswahili ndo wakaanza kuchomoza tena kwenye utajiri mfano kina Mengi, matajiri wa mabasi,malori,mahoteli nk.Mkoloni hakuwa na shida kabisa na mweusi kumiliki Mali na utajiri maadamu tu ulipe Kodi,thus walikuwepo matajiri wengi tu weusi ambao baada ya Uhuru Nyerere aliwashusha wakaishi kishetani.
Yaliyomo yalikuwepo hakuna jipya.
Anayofanya mwanafunzi alishayafanya Mwalimu na alishindwa.