Tuwe wawazi; hivi kimuziki tunaweza kuwafikia watu wa Afrika Magharibi kweli?

lugha haina mahusiano ya moja kwa moja na mafanikio ya kimuziki maana muziki wenyewe ni lugha ambayo mtu yoyote anaweza kuoilewa tatizo liko kwenye uwekezaji ie vipaji vipya, tekinologia,ubunifu n.k
 
lugha haina mahusiano ya moja kwa moja na mafanikio ya kimuziki maana muziki wenyewe ni lugha ambayo mtu yoyote anaweza kuoilewa tatizo liko kwenye uwekezaji ie vipaji vipya, tekinologia,ubunifu n.k
Fanani hawezi kuifikia hadhira bila matumizi ya lugha, hivyo binafsi naamini lugha ina mchango mkubwa tu. Japo nakubaliana pia na ulichokisema kwamba umahiri, ubunifu na matumizi ya teknolojia yana mchango mkubwa sana. Kuna watengenezaji muziki (Classical Composers) kama Mozart, Bach, Prokofiev, Enio Morricone na John Coltraine wao wanapiga vyombo tu na muziki wao bado unasikilizwa mpaka leo.

Kama unaimba kwa kutumia lugha yako ukitaka kutoka basi lazima utengenezaji wako wa muziki uwe umejaa ubunifu wa hali ya juu sana. Mfano Black Mambazo Lady Smith wana Grammy Awards kibao na wanaimba kwa lugha asilia, lakini aina ya uimbaji wao iko kitaalamu sana (Too Sophisticated), hata kama huelewi maneno lakini kama unafahamu muziki lazima utajua hawa jamaa ni wataalamu.

Watanzania utaalamu wa muziki hatuna, watengenezaji muziki asilia (Traditional Composers) hatuna. Sisi tumezoea muziki wa studio (FL) tu. Kiasi kwamba hata ukisikiliza hupati kitu cha ziada kabisa, hili limetugharimu sana hata kwenye kufanya Live Perfomance....
 
Kwa wanamuziki wetu ni poor management ndiyo huwaangusha...
 
tujiulize Kwanza
ilikuweje wakina Biti Siti muziki wao ulikubalika huko bara Hindi wakitumia kiswahili
ilikuweje wakina Bibi kidude waliweza kufanya matamasha hata huko ujerumani kwa kiswahili
vipi Jaguar waliwezaje kwenda mpaka huko japani kutumbuiza muziki wao kwa kiswahili
:N.B. hao waliwezaje kupeleka muziki wao duniani kwa kutumia lugha mama kwa teknologia ya zamani hawa wa leo wanakwama wapi na wana kila kitu teknologia(social media),pesa n.k
 
Muziki wa Bibi Kidude unaangukia kwenye genre ya Folk-Music, ukiusikiliza sana ulikuwa na utaalamu (Sophisticated) ambao hata leo hii wasanii wetu wengi hawana. Kuanzia kwenye sauti (vocals), upigaji wa vyombo ambapo alichanganya muziki wa mwambao na Afro-Jazz huku akifanya uimbaji wa papo kwa papo (Live Perfomance). Hiki cha kuchanganya muziki wa kiafrika na Jazz ndicho kiliwafanya watu kama Remmy Ongala kufika mbali kwasababu walifanya muziki kitaalamu.
 
Nafikiri sababu kuu ni wao kuandika kwa kiingereza. Lakini katika uandishi wote hao wako level moja au chini ya Kezilahabi na Shaaban Robert. Na kuna waandishi wengine bora sana wa kiswahili, lakini kwasababu ya lugha ndiyo maana tunawasikia sana hao wa nchi hizo.
 
Nimekua nikiangalia mashabiki wa mziki wa kwetu kwa muda mrefu, kuna wanaosema nchi yetu ina mwanamziki bora Afrika nzima!
Nasikitika lakini sina namna nabaki kushangaa tu.

Afrika Magharibi wanatuzidi ktk sehemu zote iwe ni burudani, elimu,Biashara, utamaduni,uigizaji,michezo,comedy nk!

Youssor N'Dor, salif Keita,Sekouba Bambino,Toumane Diabate, Amadou Balake,Coumba Gawlo,Habib Faye,Jimi Mbaye, Gnonas Pedro,Oumoh Sangare,Thione Sekh,Bonkana Maiga,Mbalou Kante na wengine wengi tu ukiwasikiliza unajua wanajua barabara zao, mziki wao unazungumza sehemu ipi barani Afrika wanatokea.

Mziki umechanganywa na Siasa,tamaduni zao,imani zao,asili zao,uelewa wao,ukomavu wao na uzoefu wao!

West Africa wanafahamika sehemu nyingi zaidi ya dunia, wana tuzo zisizo na idadi, wana vipato vikubwa sana kulinganisha na wa kwetu.

Tanzania tumebarikiwa ujuaji mwingi,kujikweza kwingi,kujiona tunastahili kuheshimiwa kuliko wengine,tunahitaji tuonekane tuna pesa nyingi kuliko tulivyo!

Mfano rahisi ni Youssor N'Dor ana utajiri wa usd 145 milioni, lakini sisi hatuelewi hayo tunataka tutambulike tuko juu ya wote.
 
Kwenye uandishi tatizo siyo lugha peke yake, tatizo ni kwamba watanzania hawana utamaduni wa kupenda kujisomea.
Hivyo kama waandishi wetu hawatasomwa na kuanza kutambulika na sisi, unategemea nani atawatambua huko nje ??
 

Ki ukweli wanamuziki wetu wengi kama sio wote ni kama wamebahatisha tu kwa ajili ya maisha magumu kuwa wanamuziki, kwa maana hiyo muziki hawaujui zaidi ya kuganga njaa tu.
 
Hatari sana,baada ya kuona alichokifanya WizKid kule London juzi nikasema sasa basi tenaa...
 
Kuhusu lugha nakataa, miziki ya Congo Zaire iliimbwa Kwa lingala Kwa kiasi kikubwa na ikatamba sana. Nyimbo za kihindi watu wanaziimba na kuzipenda mfano Kuch Kuch hotae bila kuilewa lugha.

Kuna bendi ya mchiriku inaitwa jagwa , jamaa wanagonga shoo tena Kwa Kiswahili mpaka wazungu wanapagawa.
 
Lugha ina sehemu yake ambayo ni kubwa, japo kiukweli muziki wenyewe jinsi ulivyo ni lugha tosha ambayo inajitosheleza. Ndiyo maana nikasema kwamba wale waliosomea pindi wanaposikia muziki hufahamu tu kama huyu msanii ni mtaalamu au mbabaishaji.
 
Kuna hizi band zingefika mbali na kuutangaza mziki wa Tanzani lakini mpaka leo sijui nini sababu ya kupotea,

Kuna The Kilimanjaro band, Tatu nane, Chuchu Sound na nyimbo za Taarabu za mwambao hasa zenye mahadhi ya taratibu zingeendelezwa tungefika mbali na mziki wa asili ya Tanzania.

Nchi zilizofika mbali ki mziki zaidi waliegemea kwenye mziki asili na kuchanganya vionjo vipya!

Ukiangalia km walivyofanya Hugh Masekele na Simon Paul, Mahlathini & Mahotela queens, Soul Brothers,Chicco Twala,Pat Shange,Yvonne Chakachaka,Brenda Fassie, Black Mambazo nk mziki wao ulitembea nchi mbalimbali.

Tanzania hatutaki kujifunza bali tunachukua mziki wowote tuna copy na kuingiza sokoni basi.
 
Lakini pia kumbuka kuwa West Africans waliwahi kupata contact na Europeans. Shule kwao ziliwahi sana, walianza biashara na wazungu kabla yetu, miaka mingi kabla yetu.

Ni kama hapa kwetu, makabila ambayo yaliwahi kupata contact na wazungu yako mbele kielimu na kiuchumi.
 
Muziki wa Tanzania ulianza kuanguka pale ambapo tulianza kufanya biashara na kujikuta kwamba wanaoendesha muziki ni Media-Kubwa, Promoters, Labels na Managers na siyo msanii na kipaji chake. Hivyo hawa watu wasipoupenda muziki wako au kama wewe hutakubali kuwapa pesa wakunyonye basi huwezi kutoka.

Ndiyo hapa sasa unakutana na watu wakubwa wenye ushawishi kama Ruge Mutahaba, Saidi Fela, Clouds Media, Kiss-Fm ambao kiuhalisia wao hawana vipaji vyovyote vya muziki lakini wanakula, wanalala, wanavaa na kuendesha magari ya gharama kwa kunyonya vipaji vya wenzao. Wao ukiwauliza wanasema ni biashara na wasanii na watanzania bila hata kustuka tunakubali kabisa ni biashara.

Clouds Fm na Ruge Mutahaba wamechangia sana kudorora kwa muziki wa Tanzania, yaani wana sehemu kubwa sana. Kuna wasanii wengi sana, na miziki ya aina nyingi (traditional genres) imepotezwa kwenye ramani. Iko kama Marekani na Uingereza, ambako miaka ya zamani kama 50's, 60's na 70's ilikuwa rahisi sana kwa wasanii kutoka kimuziki.

Ilikuwa ni suala la uhusiano baina ya msanii na kipaji chake pamoja na mtengeneza muziki (Producer), media zilikuwa haziingilii sana. Record Labels kama Motown chini Berry Goldy ndiyo ilisaidia sana muziki wa watu weusi kama Jazz, Soul and Blues kupata mafanikio makubwa sana nchini marekani. Berry Goldy alipigia sana muziki huu debe na kuhakikisha unasikiwa Marekani yote. Motown ndiyo iliwatoa wakina Marvin Gaye, Smokie Robinson, The Jackson 5, Diana Rose na wengine.

Lakini sasa watu walivyoona kwamba muziki unatengeneza pesa ndefu ndiyo mambo yakageuka juu chini, media zikaingilia, siaza za kibaguzi zikaingilia, promoters wakaingialia, lebels zikabadilika na managers wakawa na nguvu kuliko msanii. Hivyo msanii akawa anafanya kama wao wanavyotaka, na vipaji vingi vikaanza kuzimwa.

Ndiyo maana leo hii unabaki unashangaa inakuwaje msanii mkali wa Jazz, Soul na Blues kama Jeniffer Hudson anafunikwa na watu Adele ambao kimsingi ni wazungu. Au msanii mwenye uwezo mkubwa kama Keri Hilson anapotezwa kabisa kwenye ramani kwasababu tu ameshindana na Beyonce, ilhali Keri Hilson ana kipaji sana kuliko Beyonce. Jibu ni rahisi Media zina nguvu kuliko msanii na ndizo zinaongoza mwelekeo mzima wa muziki.

Tanzania nasisi tulikutwa na kitu cha namna hiyo kwamba media zimekuwa na nguvu kuliko msanii. Ukaanza udalali kwamba muziki wa aina fulani fulani ndiyo upigwe, na ili wasanii wapigwe ni lazima kuwe na mkataba wa kulipana baina ya msanii na media. Sasa ukiangalia Tanzania tulikuwa na media kubwa ngapi kipindi hicho, utafahamu jinsi gani muziki wetu uliangushwa.

SOCIAL MEDIA is the best thing to ever happen in Africa, naamini bila mtandao sidhani kama wasanii kama Diamond Platnumz angeweza hata kushinda vita yake dhidi ya Ruge Mutahaba na Clouds Media. Binafsi kuna wasanii wengi ambao niliwafahamu kupitia Kiss-Fm African Beats, lakini kwenye Clouds walikuwa hawapigwi kabisa.

Hili inabidi tulitazame kwa undani, na tulifanyie utafiti mkubwa,.........
 
Kaka asante kwa andiko lako hili zuri sana. Mimi napenda sana muziki, lakini pia napenda kuchimbua muziki. Hoja zako zote nakubaliana nazo humo.

Kwanini sisi tumepigwa gap?

—Kuna sababu za Kihistoria ulizozieleza hapo [utumwa, na uwekezaji wa wazungu maeneo hayo] yalichangia mambo mawili, moja ni ubepari, hii ilichangia Hakimiliki kushamiri mapema sana maeneo hayo [kinyume kabisa na hapa kwetu], pili uwekezaji na biashara kati ya west afrika na ulaya imechangia jambo kubwa sana—WEST AFRICANS DIASPORA. Hili ni gap kubwa sana walilotupiga hawa jamaa. Diaspora ndio inatoa connections ya wanaijeria kuingia huko Ulaya, kupata deals na hatimaye muziki wao kuzidi kupenya mainstream and international.

—Pili, sisi Tanzania hapa hatuna muziki wetu. Hatuna muziki wetu kwa sababu za kijiografia na kihistoria. Muziki wote barani afrika, umetokana na traditional music na kupelekwa mainstream. Ukitazama nchi kama Congo au Nigeria utagundua Aina zao za muziki zimetokana na kabila fulani kuwa kubwa and dominant, kitu ambacho kwetu vilizimwa enzi za Nyerere, mbaya zaidi sera za ujamaa, ziliathiri sana muziki, zilizuia ubunifu, zilididimiza mahusiano ya kimuziki ya Tanzania na Dunia na kubwa zaidi sera za ujamaa zilidumaza sana Diaspora yetu. Hivyo hatua na mazingira ya asili ya kupeleka muziki wetu duniani na mbaya zaidi hakuna juhudi za makusudi zilizofanywa za kupeleka muziki huu duniani kama alivyofanya Mobutu kwa muziki wa Rumba, kiasi cha kufanya matamasha maalumu kwenye Rumble of the jungle fight, kwa kuwaleta hadi kina James brown, ili tu kuutangaza muziki wa Kongo.

Kwa sasa ndio tunaamka, lakini ukitazama, hakuna juhudi zenye mkakati wenye maono ya kuipeleka sanaa yetu katika level hizo. Kila msanii unaona anapambana anavyoweza. Hivyo, sidhani kama kuna siku muziki wetu utakuwa na hadhi yoyote duniani.
 
Wewe jamaa una akili nyingi sana na zile za ziada, kuanzia leo ntaanza kukufuatilia kwa ukaribu. Hoja zako zote mbili zimebeba hoja zote ambazo tumezichangia kwenye mjadala huu na kuongezea mambo muhimu kama siasa za kijamaa. Kiufupi Mzee Nyerere alileta The Cultural Revolution hapa nchini Tanzania ambapo tamaduni zilionekana kitu kiovu kabisa na mbaya zaidi ujamaa ulikataza kabisa muziki wa nje ya Afrika kupigwa Tanzania, hivyo tasnia iliganda kabisa.

Lakini umeongelea kitu kikubwa sana cha hakimiliki (Intellectual Property Rights), ambapo nchi za wenzetu kimekuwa na nguvu sana huku serikali zikifanya jitihada za ziada kabisa. Tanzania umiliki binafsi wa mali lilikuwa ni jambo haramu na tumetunga The Copyright and Neighbouring Act mwaka 1999, sheria ambayo inasimamia hakimiliki. Hii sheria nayo ina walakini na mpaka sasa hatuna wataalamu wengi wa sheria za hakimiliki nchini Tanzania.

Wasanii wanakwama sana, wananyonywa na kuibiwa bila kupewa stahiki zao (Proper Incentives) ambazo zitatoa motisha kwa sanaa yetu kukua. Hili halipo tu kwenye muziki, hata kwenye mpira lipo, angalia jinsi timu zinavyojiendesha zikijiita za wananchi. Hivi kweli bado watu wanaamini kabisa mpira unaweza kukua kwa namna ambavyo Simba SC na Yanga zimekuwa zikiendeshwa kwa miaka mingi ???

Yaani SIASA ZA UJAMAA zimeleta laana kubwa sana nchini, huwa nashangaa sana kuona watu bado wanakuwa wanazikumbuka na kuzitamani.....
 
Tazama video hii ya Ferre Gola.

Modernization of traditional music. Na hii ndio inafanya muziki wa Kongo, au Afrika Magharibi, uzidi kuwa bidhaa pendwa duniani.
Your browser is not able to display this video.
 
Nazidi kupata vitu vipya vya kwa nini tuko nyuma sana?
Ktk thread no 38,39 mmeandika vitu mhimu mno.

Siasa za awamu ya kwanza zimeturudisha nyuma mno ktk mambo mengi.

Sijajua Mw Nyerere aliona utamaduni utamkwamisha vipi ktk kutawala nchi.

Sijui pia mawasiliano na Watanzania waliokua nje ya nchi aliyahofia sababu kwa nia ipi.

Nchi ilifungwa kwenye kila kitu.
Wafanyabiashara walifirisiwa kwa maagizo tu. Na ndio maana makampuni makubwa mengi pia ya kurekodi yalihamishia shughuri zao nchini jirani.ì

Wengi wanamsoma Mwl kwenye maandishi lakini tulioyaishi maisha ya kipindi chake tunajua ni siasa zilizompamba kuliko uhalisia!

Kakwamisha mno Watanzania kujua habari zozote za nje ya nchi kasoro Habari za Uchina zinazohusu ujamaa basi.

Hii ndio imeathiri kila kitu, Watanzania walio wengi ni miaka 20 tu iliyopita ndio wameanza kupata habari na kusafiri nje ya nchi.

Mziki wowote bila utamaduni hauwezi kueleweka umetoka wapi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…