Tuweke historia sawa- Viongozi waliowahi kujiuzulu Tanzania

Tuweke historia sawa- Viongozi waliowahi kujiuzulu Tanzania

Black cap

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2023
Posts
1,004
Reaction score
1,353
1) Mwaka 1962- Mwalimu Julius Nyerere
- Mwalimu Alijiuzulu nafasi yake ya "Waziri mkuu wa Tanganyika" miezi michache tu baada ya uhuru. Alimwachia kijiti Rashid Mfaume Kawawa na kurudi vijijini kujenga na kuimarisha chama cha TANU.
Kabla ya muungano

2) Mwaka 1977- Ali Hassan Mwinyi
- Alijiuzulu nafasi yake ya "waziri wa mambo ya ndani" kwa sababu maafisa wa usalama waliua vikongwe huko Mwanza na Shinyanga.

3) Mwaka 1990- mawaziri wote Tanzania walijiuzulu kwa sababu ya kashfa ya rushwa na malalamiko ya wananchi.
Waziri mkuu Sinde Warioba pia alijiuzulu.
Rais wakati huo alikuwa Ali Hassan Mwinyi

4) Mwaka 2015- Edward Lowasa
- Alijiuzulu nafasi yake ya "Waziri Mkuu wa Tanzania" kwa sababu ya kashfa ya kodi ya kampuni ya kufua umeme ya Richmond.

5) Mwaka 2015- Sospeter Muhongo
-Alijiuzulu nafasi yake ya "Waziri wa Nishati na Madini" kwa sababu ya kashfa ya uchotaji wa fedha katika Akaunti ya Tegeta Escrow.

6) Mwaka 2025- Humphrey Polepole
- Alijiuzulu nafasi yake ya "ubalozi nchini Cuba" kwa sababu ya kutoridhishwa na mienendo na taratibu za chama tawala (CCM) pamoja na kupinga vitendo vya utekaji wa watu.

7) Mwaka 2026- Dr. Emmanuel Nchimbi
-Amejiuzulu nafasi yake ya " umakamu wa Rais" ..........

N:B
Mwaka 1984-Abdul Jumbe
Alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Zanzibar. Alilazimika kujiuzulu nyadhifa zake zote kufuatia kile kilichoitwa "uchafuzi wa hali ya hewa ya kisiasa," baada ya kutaka mabadiliko ya muundo wa muungano kuelekea serikali tatu, jambo lililopingana na msimamo wa Nyerere na CCM.


 
Back
Top Bottom