Tuweke kumbukumbu sawa: Serikali inaelekezwa na kusimamiwa na Katiba sio Chama!

Tuweke kumbukumbu sawa: Serikali inaelekezwa na kusimamiwa na Katiba sio Chama!

jingalao

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2011
Posts
36,197
Reaction score
29,717
Screenshot_20220403-013237_Drive.jpg

Hii ni rejea muhimu kwetu sote na kwa manufaa ya Taifa letu.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!
 
Matamko yetu kama viongozi ni muhimu yakawa na umakini wa hali ya juu
 
Unahangaika sana naona jingalao .
Pole sana kwa yaliyokufika.
CCM ni nguzo ya uovu.
Hakuna cha serikali kusimamiwa na chama wala katiba.
Dawa ni katiba mpya tuu.
Mkigawana fito huko chamani kwenu ndio huwa mnakumbuka kuwa katiba ya nchi ndio "supremacy".
Huwa mnawakejeli wote wanaokosoa kwamba katiba lazima iwe juu ya kila kitu na ifuatwe,leo unaandika as if wewe ni mgeni nchini.
 
View attachment 2173553
hii ni rejea muhimu kwetu sote na kwa manufaa ya Taifa letu.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!
Leo umekuwa 'active' kwelikweli na mada hizi.

Ninakubaliana nawe, lakini kumbuka kama umesahau tu: CCM inajihesabu kwamba ndiyo chama pekee cha siasa nchini humu, hata baada ya vyama vingine kuruhusiwa kufanya siasa.

Hiyo ni 'relic' ya Chama kimoja, na kwa bahati mbaya sana tulivyo lala wananchi wa nchi hii, hakuna anyeuliza iweje, na kupinga kwa kutumia sheria mahakamani.

Tumelala sana, na CCM wanatumia usingizi wetu kufanya wanavyotaka wao.

Sasa bila shaka umesikia 'Maza Mizinguo, alivyoeleza jinsi walivyorekebisha katiba ya chama chao ili Mamea, na watendaji wengine wawajibike kwa chama; na sisi bado hatustuki chochote, tumo usingizini!

Ila naona kama wewe hapo umeanza kustuka..., lakini si kustuka kwa nia njema, maanake ingekuwa hivyo, maswali haya ungekuwa umeyauliza toka kitambo sana.

Tuipende Tanzania, achana na taka hizi za vyama vya wapiga dili.
 
Naona kapoteza matumaini yote ndani ya chama, sasa kaamua kutumia akili alizokuwa kazilaza maksudi kabisa.
 
View attachment 2173553
hii ni rejea muhimu kwetu sote na kwa manufaa ya Taifa letu.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!
EnHeeee, 'Jinga' imekuwaje leo? Mbona hutulii?

Nakushauri uwatafute watu kama 'Wajalalani', na wa aina hiyo katika kundi lenu mmyajadili haya yanayowasibu. Si wewe pekee unayeumia, unajua?

Huyo Mwanakijiji atakusaidia nini wakati huu. Huyu alishauza roho yake, hana ushawishi tena.
 
Mafisadi kushika hatamu kwa chama tawala nchi yetu itaangamia
 
Leo umekuwa 'active' kwelikweli na mada hizi.

Ninakubaliana nawe, lakini kumbuka kama umesahau tu: CCM inajihesabu kwamba ndiyo chama pekee cha siasa nchini humu, hata baada ya vyama vingine kuruhusiwa kufanya siasa.

Hiyo ni 'relic' ya Chama kimoja, na kwa bahati mbaya sana tulivyo lala wananchi wa nchi hii, hakuna anyeuliza iweje, na kupinga kwa kutumia sheria mahakamani.

Tumelala sana, na CCM wanatumia usingizi wetu kufanya wanavyotaka wao.

Sasa bila shaka umesikia 'Maza Mizinguo, alivyoeleza jinsi walivyorekebisha katiba ya chama chao ili Mamea, na watendaji wengine wawajibike kwa chama; na sisi bado hatustuki chochote, tumo usingizini!

Ila naona kama wewe hapo umeanza kustuka..., lakini si kustuka kwa nia njema, maanake ingekuwa hivyo, maswali haya ungekuwa umeyauliza toka kitambo sana.

Tuipende Tanzania, achana na taka hizi za vyama vya wapiga dili.
Tatizo huwa hatusomi hizi instruments tulizonazo.
 
Huwezi kudai katiba mpya wakati huo huo unalalama katiba kusiginwa!!!
Iliyopo inajitoshelezaje wakati hata kiongozi akiisigina hiyo katiba hauna/hatuna cha kumfanya!!?
Kama rais ndiye anayeteua majaji wa mahakama zote,unategemea unaweza hata kufungua kesi ya kikatiba na ikaendeshwa bila ya majaji kuwa biased kwa anayewateua!!!??
Yaelekea bado usingizi haujakuisha sawasawa jingalao .
Siwezi kudai Katiba mpya ...iliyopo inajitosheleza .wanaodai katiba Mpya hawajaisoma iliyopo
 
Tatizo huwa hatusomi hizi instruments tulizonazo.
Kuna watu wamezisoma na kuzielewa sana.
Tatizo si kusoma na kuzielewa.
Ninyi wafuasi wa JPM mlimsifia na mnamsifia sana kwamba kaibadilisha nchi. Kama kweli JPM angekuwa na nia njema na hii nchi,angetengeneza mifumo ambayo hata yeye kama ambavyo hayupo leo,nchi ingeendelea kwa mujibu wa mfumo (katiba) iliyo madhubuti.
Sasa jamaa yenu alifeli hata kuhakikisha anatengeneza utii wa katiba hii hii iliyopo,akaiweka pembeni na kujifanya yeye ndiye katiba,sheria,kanuni,taratibu na hakimu mkuu.
Hatukuona jingalao wala nani wakipiga kelele kuhusu katiba kusiginwa zaidi ya kufurahia upumbavu ule.
 
yeye alitekekeza Katiba kivitendo
 
Siwezi kudai Katiba mpya ...iliyopo inajitosheleza .wanaodai katiba Mpya hawajaisoma iliyopo

Hii katiba iliyopo ndio inamfanya rais kuwa juu ya katiba ma sheria, anaweza kufanya lolote na asiwajibike popote. Hii ndio sababu hasa ya mifumo ya nchi hii kuwa dhaifu. Sehemu kubwa unakuta katiba inatekelezwa kwa kufuata tabia binafsi za rais aliyeko madarakani. Mifano ya haya iko wazi.
 
View attachment 2173553

Hii ni rejea muhimu kwetu sote na kwa manufaa ya Taifa letu.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!

Hongera kwa kujirejeshea akili.

Angalau vile vioja vya viongozi wa CCM kuonekana wakiwakoromea watendaji wa serikali na kuwalazimisha kuzingatia ilani ya CCM vitaanza kutambulika kama ujinga usio kifani. Ilani ni bargaining tool ya chama bungeni. Basi. Si agizo la utekelezaji.

Nchi ya ajabu hii yenye viongozi wasiojua kiunganisho kati ya vyama-bunge-mahakama-serikali (executive). Hawajui kwamba serikali inatekeleza maazimio ya bunge, sheria na hukumu za mahakama tu; sio ilani ya chama cha siasa. Na chama hakiwasiliani na serikali moja kwa moja bali kupitia viongozi wa kisiasa serikalini. Sio ule ujinga wa mwenyekiti wa wilaya wa CCM kumhoji OCD wa polisi kuhusu ajali za barabarani au ujambazi wilayani.
 
Back
Top Bottom