Tuweke kumbukumbu sawa: Serikali inaelekezwa na kusimamiwa na Katiba sio Chama!

Tuweke kumbukumbu sawa: Serikali inaelekezwa na kusimamiwa na Katiba sio Chama!

Hongera kwa kujirejeshea akili.

Angalau vile vioja vya viongozi wa CCM kuonekana wakiwakoromea watendaji wa serikali na kuwalazimisha kuzingatia ilani ya CCM vitaanza kutambulika kama ujinga usio kifani. Ilani ni bargaining tool ya chama bungeni. Basi. Si agizo la utekelezaji.

Nchi ya ajabu hii yenye viongozi wasiojua kiunganisho kati ya vyama-bunge-mahakama-serikali (executive). Hawajui kwamba serikali inatekeleza maazimio ya bunge, sheria na hukumu za mahakama tu; sio ilani ya chama cha siasa. Na chama hakiwasiliani na serikali moja kwa moja bali kupitia viongozi wa kisiasa serikalini. Sio ule ujinga wa mwenyekiti wa wilaya wa CCM kumhoji OCD wa polisi kuhusu ajali za barabarani au ujambazi wilayani.
Hizi zilikuwa ni sera za serikali ya Urusi ambazo nchi ya urusi ilitaka zitumike duniani kote.soma kitabu kiitwacho RISE AND FALL OF SOVIET EMPIRE kimetungwa na Brian Crozier.wakati mwingine lazima tukubali marekani na washilika wake wameikomboa dunia.
 
Usitudanganye bwana Jingalao, serikali ya awamu ya 6 mbona inaelekezwa kutokea Msoga? Hakuna cha katiba wala chama!
 
Matamko yetu kama viongozi ni muhimu yakawa na umakini wa hali ya juu
Unaona leo kwamba matamko lazima yadhibitiwe. Wakati wa magufuli alitaka chochote nawe unashangilia bila kujua athar zake. ( ulifunga kibwaya ukanengua) leo hali imegeuka unalia na matamko.
Ccm inapendwa na wajinga na waliosoma (Source: research data)
 
View attachment 2173553

Hii ni rejea muhimu kwetu sote na kwa manufaa ya Taifa letu.


KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!
Tatizo la Mi CCM inadhaniniko juu ya kila kitu katika Tanzania hii.
Ndio maana wanakiuka misingi ya Katiba na kuona ndio inaishauri Serikali.
Using wanarejesheana nafasi za uongozi! WaTanzania ni muda wa kuamka na kudai Katiba mpya sio swala la chama fulani pekee. Hii kujidai ina wenyewe ni uchwara tu.!

Sent from my SM-A115AZ using JamiiForums mobile app
 
Kipindi kile kichaa anafanya atakalo mlikua busy kumpongeza na kuimba mapambio sasa zamu yenu imeisha ndio mmeumia na kuanza kujisogeza kwa wapenda haki.
 
Tatizo hatuna vyombo imara vya kulinda katiba vyetu mfano polisi, TISS, n.k
Tatizo la Mi CCM inadhaniniko juu ya kila kitu katika Tanzania hii.
Ndio maana wanakiuka misingi ya Katiba na kuona ndio inaishauri Serikali.
Using wanarejesheana nafasi za uongozi! WaTanzania ni muda wa kuamka na kudai Katiba mpya sio swala la chama fulani pekee. Hii kujidai ina wenyewe ni uchwara tu.!

Sent from my SM-A115AZ using JamiiForums mobile app
 
Kwa kadri ninavyoelewa mimi, Nchi inaongozwa kwa maelekezo kutoka ndani ya Katiba; wakati Serikali inaongozwa kwa maelekezo yaliyomo ndani ya Ilani ya Uchaguzi ya Chama kilichopo madarakani.
Je, kwenye Katiba siku hizi kuna ilani za uchaguzi? Tuseme ilani za vyama kama CHADEMA, ICT, CCM......?
 
Wewe na wenzako ni propoganda au tumbo kilichowageuza kuwa msukule enzi za bwana yule?
 
Back
Top Bottom