This is...
JF-Expert Member
- Dec 28, 2014
- 5,050
- 5,204
Tumemsikia Mkurugenzi wa NEC akitoa tuhuma dhidi ya mgombea urais wa chadema kwamba anakiuka maadili ya uchaguzi, lakini hatujamsikia akiongelea upande wa pili wa Dkt. Magufuli. Sisi kama wananchi tumeshuhudia matendo yanayokiuka maadili ya uchaguzi yanayofanywa na Dkt. Magufuli kwa uchache nitaorodhesha machache:
1. Dkt. Magufuli kutumia hazina ya taifa kutoa fedha za miradi wakati akijua ana hadhi sawa na wagombea wengine,kurubuni wananchi. Hii Ni rushwa ya wazi. NEC mko wapi??
2. Dkt. Magufuli kuwatisha wananchi kuwa hatowaletea miradi ya maendeleo wasipochagua wagombea wa chama chake. Hapa Kuna mambo mawili Dkt. Magufuli amejuaje kwamba atachaguliwa tena, pili hivi ni vitisho na kuligawa taifa. NEC hamuoni?
3. Kassim Majaliwa kufanya kampeni nchi nzima na kutumia rasilimali za serikali wakati yeye si mgombea urais wala si mgombea mwenza. Yeye ni mgombea ubunge wa Ruangwa. NEC mmeziba masikio.
4. Polepole kumuita Lissu katuni, kuiagiza TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI kumuita Lissu katika Kamati ya Maadili. NEC hawaongei hili wala kukemea lakini Mkurugenzi anajinasibu wako huru na hawafanyi kazi kwa shinikizo.
5. Mkurugenzi wa Tume akiwa kama refa anaipigia CCM kampeni waziwazi lakini Tume haichukui hatua zozote.
ONGEZEA MENGINE ILI KUWEKA KUMBUKUMBU SAWA.