May Day
JF-Expert Member
- May 18, 2018
- 6,311
- 9,027
Tengeneza picha umeamka siku moja na kujikuta kati kati ya jangwa saa sita mchana jua lipo utosini, ukizunguka pande zote huoni Mmea wala Mbu zaidi ya miale (mirage) inayotokana na kuakisiwa kwa jua juu ya uso wa Dunia.
Hicho ndio kifo, na iwapo ghafla mbele yako itafumuka chemu chemu ya maji baridi basi huo ndio uhai....Maji ndio uhai.
Niliposikia kuwa tumetumia karibia bilioni mia sita kwenye sensa nilijaribu kufikiria mambo mengi sana.
Kwa mfano nilijiuliza ni kwa nini tusingejenga maabara moja kubwa pale Kigamboni na Wanasayansi wetu wa kileo na hata wale wa Mtaani wakakutana na kufanya kazi usiku na mchana hata kama itawachukua miaka mitano ili hatimaye wapate suluhu ya kuyageuza maji ya bahari kuwa maji baridi?.
Hakuna linaloshindikana chini ya jua ndio maana Wengine walifikiria kwenda kufika na kuangalia Mwezini kuna nini na wakafanya kazi kwa bidii mpaka wakafanikiwa.
Kutoa tu jibu kuwa kusafisha maji ya bahari ni teknolojia ngumu ni jibu la kinyonge sana...ni kama vile hatuna matumaini ya kuendeleza pale 'Wazungu' wanapotuachia...yaani Mtu atasoma na kusimikwa ma PHD yao lakini bado hana faida sana kwa jamii yake zaidi ya kutegemea ajira Chuoni akawe Mhadhiri...na baadae atimkie kwenye Siasa kana kwamba ndicho haswa kilichompeleka huko Vyuoni Ulaya.
Nafahamu changamoto ya kuishi Dunia ambayo kuna Wengine wanafanya zaidi ya asilimia tisini ya suluhu za changamoto zinazoikabili Dunia ili hali sisi wa Dunia ya tatu tunabakl kama wapokeaji...sawa hatukuweza kwenye kuunda Boeng, TV au simu za mikononi lakini bahari tunayo...ni ya kwetu.
Itafika mahali tutahitaji bomba la kutoa maji baharini kuja Bara/mikoani badala ya kufikiria kufanya hivyo kwa mafuta au gesi tu.
.........Maji ni Uhai.....