Tuweni serious

Tuweni serious

Sio wajibu wa mtoto kumhudumia mzazi. Ni wajibu wa mzazi kumhudumia mtoto.

Iko hivi, kwa mambo yoote mema na mazuri waliyokutendea wazazi wako tangu unazaliwa, hakuna bei utaweza kuwalipa. Malipo yake ni kuwatendea vivyo hivyo wajukuu zao, au hata zaidi.

Kama baba yako alichakalika kutwa kucha kuhakikisha hamkosi kula, hakikisha watoto wako hawakosi kula under any circustance. Kama ulisoma na kila ulichohitaji ulipatiwa kwa wakati, tenda hivo hivo kwa wanao.

Kama mama alijinyima kula ili wewe ushibe tendea hivo wanao, kama ulianza kukengeuka, baba/mama akachukua bakora akakucharaza urudi kwenye reli, fanya hivo kwa wanao wanaojifunza utukutu. Sio kuanza kuleta uzungu akati kizazi kinaharibika.

Pamoja na changamoto za ndoa, ila kama baba/mama yako alimvumilia mwenzie ili wewe ukue ukiwa chini ya malezi ya wazazi wote wawili jitahidi kumaliza tofauti zenu huko ili mlee hao watoto hadi watakapo jitegemea mkiwa pamoja.

Kama hukuwahi kumwona baba yako akimfokea/akipmiga mama yako mbele yenu, usimfokee mkeo ama kumpiga mbele ya watoto. Hata kama uliwahi kushudia hicho kitu, just dont. Yaan my point is Just give your kids the best you got from your parents. Hapo utakuwa unalipa madeni ya yoote mazuri waliyokutendea wale wazee.

Niamini mimi, Furaha na mafanikio ya wajukuu zao ndiyo zawadi kubwa unaweza kuwapa wazazi wako. Sio hivi visenti.
Brilliant
 
Msisitizo:
wao wameamua kuishi nao na ndio waislam walivyoo. Kijana wajue sana wazazi wako siku zako zipate kuwa nyingi hapa duniani.
Malaya, sio wakaaji ni maisha mafupi tu utakayofurahia nao. Mke au Mume hao hawanaga guarantee So only your mom anaguarantee maishani mwako na ndugu zako japo sio wote . Good Day
Kama baba yako angesema Mke hana guarantee usingekuwa naye huyo mama.
 
This is stupid. Wafanye wazazi wako waishi vizuri siku walizobakiza hapa duniani
Am not responsible for that. I got a family to take care of. Ila nnapoweza, nawasaidia kama nnavomsaidia mtu mwingine yeyote. Siwezi kuacha kulipa ada ya mwanangu ili nimtumie baba pesa ya kupaua kibanda chake. Thanks.
 
Hujaambiwa uache majukumu ya familia ili umpe baba nimekuambia mjumlishe humu kama mmoja wa familia yako
 
Hujaambiwa uache majukumu ya familia ili umpe baba nimekuambia mjumlishe humu kama mmoja wa familia yako
Sasa namjulishaje kama mmoja wa familia yangu akati nae anafamilia yake! Sababu yeye ana mke na watoto wake, na anawajibika kwa hao. Mimi nae nnamke na watoto wangu, nnawajibika kwa hao. My brother, usilegeze maisha kwa kutegemea watoto waje wakusaidie. Utakuwa unawapa mzigo usio wastahili. Hao watoto nao watakua na watakuwa na majukumu yao. Kila mtu ashinde mechi zake.
 
Mie ni mwanamke
 
Sikusemi vibaya ndugu mwandishi ila Kuna kila dalili wewe ni masikini kama Mimi tu. Au unanizidi kidogo umasikini.

Usiwape ndugu lawama za umasikini wako!! Pambana uvunje poverty circle.

Kwahiyo we ukisaidiwa na shemeji yako utakataa?

Hivi hujui msemo kuwa familia unayo iunda ndio yako kuliko uliyotoka?
 
Attachments

  • Screenshot_20230128-175818.png
    Screenshot_20230128-175818.png
    46.9 KB · Views: 4
Why my dear
Ni vigumu kumtenganisha mtoto wa kike na mzazi. Hata wanavosemaga kwenye ndoa pesa ya mwanamke haionekani uwa inarudishwa kwa wazazi. Na hiyo ni kwasababu mwanaume yupo atacovet kila kitu🙂
 
Sikusemi vibaya ndugu mwandishi ila Kuna kila dalili wewe ni masikini kama Mimi tu. Au unanizidi kidogo umasikini.

Usiwape ndugu lawama za umasikini wako!! Pambana uvunje poverty circle.

Kwahiyo we ukisaidiwa na shemeji yako utakataa?

Hivi hujui msemo kuwa familia unayo iunda ndio yako kuliko uliyotoka?
Duniani wote ni maskini tu ila kwenye kusaidia wote tunajitahidi
 
Ni vigumu kumtenganisha mtoto wa kike na mzazi. Hata wanavosemaga kwenye ndoa pesa ya mwanamke haionekani uwa inarudishwa kwa wazazi. Na hiyo ni kwasababu mwanaume yupo atacovet kila kitu🙂
Nikiolewa nitapenda wazazi wote nitawasadia sana sintoangalia yupi ni wangu wote ni wangu kadri ya uwezo wangu nitafangua milango yangu kwao ila Kwa ndugu mie wangu wote wazee wanalea vilembwe na Mshukuru Mungu Sina anayenitegemea labda wa Mume nao watachoose niwaangalie wazazi wao au nisikilize shida zao ila sipendi waniandame kweli
 
Are you single😉
 
Back
Top Bottom