Sio wajibu wa mtoto kumhudumia mzazi. Ni wajibu wa mzazi kumhudumia mtoto.
Iko hivi, kwa mambo yoote mema na mazuri waliyokutendea wazazi wako tangu unazaliwa, hakuna bei utaweza kuwalipa. Malipo yake ni kuwatendea vivyo hivyo wajukuu zao, au hata zaidi.
Kama baba yako alichakalika kutwa kucha kuhakikisha hamkosi kula, hakikisha watoto wako hawakosi kula under any circustance. Kama ulisoma na kila ulichohitaji ulipatiwa kwa wakati, tenda hivo hivo kwa wanao.
Kama mama alijinyima kula ili wewe ushibe tendea hivo wanao, kama ulianza kukengeuka, baba/mama akachukua bakora akakucharaza urudi kwenye reli, fanya hivo kwa wanao wanaojifunza utukutu. Sio kuanza kuleta uzungu akati kizazi kinaharibika.
Pamoja na changamoto za ndoa, ila kama baba/mama yako alimvumilia mwenzie ili wewe ukue ukiwa chini ya malezi ya wazazi wote wawili jitahidi kumaliza tofauti zenu huko ili mlee hao watoto hadi watakapo jitegemea mkiwa pamoja.
Kama hukuwahi kumwona baba yako akimfokea/akipmiga mama yako mbele yenu, usimfokee mkeo ama kumpiga mbele ya watoto. Hata kama uliwahi kushudia hicho kitu, just dont. Yaan my point is Just give your kids the best you got from your parents. Hapo utakuwa unalipa madeni ya yoote mazuri waliyokutendea wale wazee.
Niamini mimi, Furaha na mafanikio ya wajukuu zao ndiyo zawadi kubwa unaweza kuwapa wazazi wako. Sio hivi visenti.