Tuweni serious

Tuweni serious

Am not responsible for that. I got a family to take care of. Ila nnapoweza, nawasaidia kama nnavomsaidia mtu mwingine yeyote. Siwezi kuacha kulipa ada ya mwanangu ili nimtumie baba pesa ya kupaua kibanda chake. Thanks.
Sisi sio wazungu. Hata uige vipi. Africa tuna kitu kinaitwa Back Tax. Watu wamekupambania ufike ulipofika, you need to do your part kwa wazazi na wadogo zako. What do you think will happen to your kids siku ukifa ghafla na wazazi wako na ndugu zako umewachinjia baharini
 
Sio wajibu wa mtoto kumhudumia mzazi. Ni wajibu wa mzazi kumhudumia mtoto.

Iko hivi, kwa mambo yoote mema na mazuri waliyokutendea wazazi wako tangu unazaliwa, hakuna bei utaweza kuwalipa. Malipo yake ni kuwatendea vivyo hivyo wajukuu zao, au hata zaidi.

Kama baba yako alichakalika kutwa kucha kuhakikisha hamkosi kula, hakikisha watoto wako hawakosi kula under any circustance. Kama ulisoma na kila ulichohitaji ulipatiwa kwa wakati, tenda hivo hivo kwa wanao.

Kama mama alijinyima kula ili wewe ushibe tendea hivo wanao, kama ulianza kukengeuka, baba/mama akachukua bakora akakucharaza urudi kwenye reli, fanya hivo kwa wanao wanaojifunza utukutu. Sio kuanza kuleta uzungu akati kizazi kinaharibika.

Pamoja na changamoto za ndoa, ila kama baba/mama yako alimvumilia mwenzie ili wewe ukue ukiwa chini ya malezi ya wazazi wote wawili jitahidi kumaliza tofauti zenu huko ili mlee hao watoto hadi watakapo jitegemea mkiwa pamoja.

Kama hukuwahi kumwona baba yako akimfokea/akipmiga mama yako mbele yenu, usimfokee mkeo ama kumpiga mbele ya watoto. Hata kama uliwahi kushudia hicho kitu, just dont. Yaan my point is Just give your kids the best you got from your parents. Hapo utakuwa unalipa madeni ya yoote mazuri waliyokutendea wale wazee.

Niamini mimi, Furaha na mafanikio ya wajukuu zao ndiyo zawadi kubwa unaweza kuwapa wazazi wako. Sio hivi visenti.
This is my point of view too... Ani iko hivi

Sio jukumu la mtoto kumlea mzazi ... Ni jukumu la mzazi kumlea mtoto ... Mama yangu na baba yangu wamenilea nimefika hapa nilipo wamemaliza jukumu lao ... Ni jukumu langu kulea familia yangu(mke na watoto) nao niwafikishe level ya kujitegemea... Sasa ukisema nihangaike na familia yangu (mke na watoto) halafu nihangaike na mama na baba tena it's just not fair ...

BUT

Kama mama , baba na ndugu wako na hali mbaya ni vyema kuwasaidia kwa uwezo wako na kuna baraka ndani yake pia.
(Msaada huu uwe ndani ya uwezo wako ani usikupe stress)

Ukijaribu kuangalia the other side of the story ni kwamba mimi nimelelewa nimekuwa mkubwa then niwalee wazazi wangu afu wanangu wateseke then wanangu waje wanilee mimi wanao wateseke like wtf is that ... Ani nimzae mtoto afu nijiambie "huyu atakuja kunilea nikizeeka!" Hiyo Logic sio


So conclusion ni kwamba you need to start your own family na kuipa kipaumbele kwanza lakini Allah akikujaalia ukaweza kuhudumia familia yako vyema then ukawa na uwezo wa kuwasaidia ndugu na wazazi kama hawajiwezi hiyo inakuwa superb
 
Ndio wazazi ni Mungu wapili wa duniani
Mathayo 12:47-50
[47]Mtu mmoja akamwambia, Tazama, mama yako na ndugu zako wamesimama nje, wanataka kusema nawe.
[48]Akajibu, akamwambia yule aliyempasha habari, Mama yangu ni nani? Na ndugu zangu ni akina nani?
[49]Akawanyoshea mkono wanafunzi wake, akasema, Tazama, Mama yangu na ndugu zangu!
[50]Kwa maana ye yote atakayeyafanya mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni, huyu ndiye ndugu yangu, na umbu langu, na mama yangu.



Baba wa dunia hii utanisamee Tu. sina undugu na wewe usipo nielewa kwenye imani yangu binafsi
 
Mathayo 12:47-50
[47]Mtu mmoja akamwambia, Tazama, mama yako na ndugu zako wamesimama nje, wanataka kusema nawe.
[48]Akajibu, akamwambia yule aliyempasha habari, Mama yangu ni nani? Na ndugu zangu ni akina nani?
[49]Akawanyoshea mkono wanafunzi wake, akasema, Tazama, Mama yangu na ndugu zangu!
[50]Kwa maana ye yote atakayeyafanya mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni, huyu ndiye ndugu yangu, na umbu langu, na mama yangu.



Baba wa dunia hii utanisamee Tu. sina undugu na wewe usipo nielewa kwenye imani yangu binafsi
Sawa umeamua niwako sio wangu mie wangu nawatunza ni wezavyo
 
 
Back
Top Bottom