Huu wakati ambao asilimia kubwa ya vitu tunategemea simu aidha kama njia ya mawasiliano, wengine simu ndio ofisi yaani wanatumia kuingizia kipato au wengine kama vifaa vya kujiburudisha kwa kuchezea magemu inahitaji ujuzi na akili kubwa kuweza kufanya machaguo ya wakati wa kuingia sokoni.
Sasa kwenye masoko ya simu kuna upigaji sana, unaweza uziwa simu kwa bei ghali kumbe haikufaa kuuzwa hivyo ila utanunua sababu huna ujuzi au hujui vitu gani utazame ili uweze kupata simu kulingana na mahitaji.
Wataalamu wa haya mambo tupeni ABC ya namna ya kuyaendea masoko ya simu hasa kwa sisi ambao hatuwezi kwenda kwenye maduka kama Mliman City ambayo yanasifika kwa kuzingatia ubora tunaishia Kariakoo ambako inasifika kuwa wajanja wengi.
Tutajiaje kuwa hii simu ina ubora, usalama, betri liko vizuri, ni mpya kweli na si kanjanja, camera nk ni mbinu gani tutumie?