Tuzingatie kitu gani tunapokwenda kununua simu ili tupate simu bora?

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251
Huu wakati ambao asilimia kubwa ya vitu tunategemea simu aidha kama njia ya mawasiliano, wengine simu ndio ofisi yaani wanatumia kuingizia kipato au wengine kama vifaa vya kujiburudisha kwa kuchezea magemu inahitaji ujuzi na akili kubwa kuweza kufanya machaguo ya wakati wa kuingia sokoni.

Sasa kwenye masoko ya simu kuna upigaji sana, unaweza uziwa simu kwa bei ghali kumbe haikufaa kuuzwa hivyo ila utanunua sababu huna ujuzi au hujui vitu gani utazame ili uweze kupata simu kulingana na mahitaji.

Wataalamu wa haya mambo tupeni ABC ya namna ya kuyaendea masoko ya simu hasa kwa sisi ambao hatuwezi kwenda kwenye maduka kama Mliman City ambayo yanasifika kwa kuzingatia ubora tunaishia Kariakoo ambako inasifika kuwa wajanja wengi.

Tutajiaje kuwa hii simu ina ubora, usalama, betri liko vizuri, ni mpya kweli na si kanjanja, camera nk ni mbinu gani tutumie?
 
Batterry Cappacity -5000+mah
Kioo kiwe na Super Amoled
Chipset iwe SnapDragon au exynos
Iwe na muonekano wa kuvutia.
Ram 6 , Rom 260+

Njia nazotumia,kwanza huwa naingia GSM kuangalia simu za bei rahisi ambazo zimetoka miezi michache iliyopita, nakagua sifa zake ,namna ikiwa haijafunguliwa kabisa, siku ambayo simu imetengenezwa, imetengenezwa nchi gani? Mfano samsung za A zinatoka China,India,Vietmnan n.k

Ukitaka upate original jitahidi ununue simu pale pale zikiachiwa sokoni bado za moto , mfano mimi nimenunua galalxy A17 5g mwezi January 2026 lakinii kwenye boksi siku ya matengenezo ilikuwa 23 november2025. Lakini pia pale kariakoo sio kwamba simu original hakuna , zipo nyingi tu, na hata hao wa mlimani city wanapokelea hapo au hutumwa mtu kuzifuata hapo wanazipeleka mall.

Kwahiyo kabla hujanunua simu ichunguze, ichambue, weukifika unahakiki tu wala huitaji maelezo. Hakikisha unaifungua mwenyewe iwe haijafunguliwa boksi
 
Asante Mkuu
 
Safi Sana mkuu
 
China plaza kumekaa kitapeli sana mul asee kwa kina zahor
 
Samsung A17 4g ya 380k wale wadada wanauza 600k? Wanarembesha ofisi wa mabango na vimeza vya kioo na kuvaa suti ili utetemeke, nilizunguka pza yote ile nawachora tu🤣🤣. Hamna kitu pale...
Nikawaambia nataka A17 5g wakawa hawaifahamu wanaijua hiyo ya 4g. Kimoyo moyo nikasema pumbavu zenu..
 
Ukiona umegoogle Simu ya miaka 2 afu bongo wanakwambia full box kimbia mbio usiangalie nyuma
 
je 350,000 naweza kupata simu aina ya Nokia na je zinafaa
Umelenga kununu nokia gani?🤔

Nokia mostly zilizopo sokoni ni za button ila hizi smart zipo but sio nyingi kivile. Nokia zipo sijajua kwa sasa no Nokia ipi inakimbiza sokoni kwa hiyo bajeti yako ya 350K ila Samsung unapata.

Usije ukanunua simu za chini ya mwaka 2023. Kama MUNGU atakujalia bajeti zaidi ujikaze ununue simu ya kuanzia mwaka 2025, latest.

Ram isiwe chini ya GB 6 ( simu nzuri ram ni GB 12). Avoid Tecno , Infinix na Itel,kaa nazo mbali hizi brands kama upo serious na kununua sim.
Battery 🔋 make sure inaanza 5000 mAh apps za kisasa zina run sana in the background so kwa simu yenye battery ya mashaka utakuwa unachaji sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…