Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
Kwa Sasa Rais wetu Mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania jasiri Muongoza Njia Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan,Ndio Kinara wa kupigania Nishati Safi ya kupikia Barani Afrika Na Duniani Kwote.
Ndio Sauti ya Wanawake wote ,ndio mkombozi wa wanawake ambao wamejikuta wakiathirika kiafya kutokana na matumizi ya nishati ya kuni na mkaa katika kupikia.Ndio Sauti pekee inayosikika na kusikilizwa juu ya nishati safi ya kupikia,ndio Sauti ambayo inaendelea kusikika masikioni kwa Mataifa tajiri na masikini,ndio mtetezi wa mwanamke na mtoto wa kike Duniani Kwote.
Rais wetu kipenzi anataka iwe mwisho wa machozi ya wanawake na mtoto wa kike kutokana na matumizi ya nishati hiyo hatarishi ya kuni na mkaa kupikia. Rais Samia Ameibuka na kuinuka kama nyota ya matumaini katikati ya giza kuwafuta machozi na kuwakomboa wanawake .
Kwa njia hiyo Rais Samia amefanya kazi ya kupiga ndege wawili kwa jiwe moja kishujaa na kihodari sana. Kwanza kwa kuhamasisha matumizi ya Nishati Safi ya kupikia kama vile gas, umeme n.k. maana yake anafanya kazi ya kuokoa mazingira yetu .kwa sababu kila mwaka maelfu kwa maelfu hadi mamilioni ya miti yamekuwa yakikatwa na kuteketezwa kwa ajili ya kuni na kuchoma mkaa. Hali ambayo imekuwa ikiacha jangwa Maeneo mbalimbali Duniani kwote hususani katika Nchi zinazoendelea.
hali ambayo kwa kiasi kikubwa imepelekea na kuchochea mabadiliko ya hali ya hewa maeneo mbalimbali Duniani kwote.kama vile ongezeko la joto kali pamoja na ukame mkali ambao umesababisha madhara mbalimbali kama vile kufa kwa wanyama,kukauka kwa mimea na hivyo kutokea kwa njaa,kukauka na kupungua kwa vyanzo vya maji na hivyo kuleta athari za upungufu wa umeme kwa wale wanaotegea maji kama chanzo kikuu cha uzalishaji umeme.
Lakini pia hali hiyo imekuwa ikigharimu serikali zote pesa nyingi sana katika kukabiliana na athari hizo. Pesa ambazo zingeweza kutumika katika shughuli nyinginezo za maendeleo kama vile ujenzi wa shule, zahanati,vituo vya afya, miundombinu ya barabara, usambazaji wa Maji na umeme kwa bei nafuu na mengine mengi.
Lakini vilevile kampeni ya Rais Samia inaokoa Maisha ya Mwanamke na mtoto wa kike kutokana na matumizi ya kuni na mkaa kupikia. pia inainua uchumi wa mwanamke kwa kutumia muda wake katika shughuli za kiuchumi badala ya kusafiri umbali mrefu kwenda porini kutafuta kuni.
jambo ambalo wakati mwingine limeleta madhara kama vile watoto wa kike kubakwa maporini,kuumwa na nyoka ,kuumwa na kuvamiwa na wanayama wakali wa msituni pamoja na kuumia kwa kudondoka kwenye miti au kuchomwa na vitu kama vile miiba,miti na ajali mbalimbali za porini.
Kuibuka kwa Rais Samia na kampeni hii ya matumizi ya Nishati safi ya kupikia kunamfanya Mama kuwa nuru na tumaini kwa wanawake na watoto wa kike ulimwenguni kwote. Jambo hilo la kuokoa Maisha ya mamilioni ya wanawake na watoto wa kike ulimwenguni pamoja na kuokoa mazingira kunamfanya Rais Samia kuwa na Nafasi kubwa ya kutwaa tuzo ya Nobel.
Sioni kinachoweza kumzuia kubeba tuzo hiyo ya heshima kabisa Duniani Kwote. Mama anastahili kabisa bila kipingamizi kupata heshima hiyo. Naamini waandaaji wa tuzo hiyo mpaka muda huu watakuwa wameshaona mchango chanya wa Mama na kusubiri wakati ufike tu ili waweze kumpatia Mama yetu Mpendwa na shujaa wa Afrika.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.