Tuzo za Trace Music Awards zilikatishwa kutokana na maji kujaa karibu na Jukwaa

Tuzo za Trace Music Awards zilikatishwa kutokana na maji kujaa karibu na Jukwaa

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
378
Reaction score
766
Ninachojiuliza ni kwamba hawakujua au hawakufanya Survey ya eneo kabla ya kuweka Jukwaa
—————————————

Tuzo za Trace kwa wasanii wa Afrika zilizofanyika usiku wa kuamkia leo Visiwani Zanzibar, Tanzania, zilikatishwa kutokana na maji kujaa karibu na jukwaa.

Tuzo hizo zilizoonekana kuchelewa kuanza kutokana na uwepo wa upepo mkali na mawimbi ya maji, ikawalazimu waandaaji kusogeza mbele kuanza kwa tuzo hizo, zilizoanza muda wa saa 4 usiku badala ya saa mbili.

Kwa mujibu wa mashuhuda, tamasha hilo lililoanza kwa wasanii mbalimbali kuburudisha na lilikatishwa muda wa saa 9:20 usiku, ikiwa katika hatua za mwanzo za kutangaza tuzo hizo.

Source: BBC Africa
 
Issue hakuna ARENA.. Serikali imepigiwa sana kelele Ila bado ipo busy na viwanja vya mpira.

Ni aibu kwa Dar ambayo ni mji mkuu wa burudani Afrika mashariki kukosa Arena. Tunazidiwa hata na Kigali 🙌🏾
 
Back
Top Bottom