Wadau tunawashukuru kwa maoni yenu, kama ilivyoandikwa ktk thread hii Tuzo hizi bado ni changa, na mapungufu hayakosekani ila tutajitahidi kwa kadiri ya uwezo wetu kuziboresha mwaka hadi mwaka. Kutokana na hali ya kiuchumi mwaka huu tumeamua kuwa na categories 11 tu, lakini uwezekano wa ku-zibadilisha/ongeza/punguza/boresha upo.
Kwanza kabisa tungependa kuwafahamisha kwamba Bongo5 Media Group Ltd ni kampuni inayojitegemea na haina uhusiano na kampuni wala media house nyingine yoyote hapa nchini, wenye kampuni ni Luca Neghesti na Nancy Sumari.
Mchakato wa wananchi kupiga kura kupitia tovuti ya
Tanzania People Choice Awards na SMS ulianza February 2014, lakini kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wetu tulilazimika kuusitisha na kuanza tena April 29, ukidumu kwa wiki 3 tu.
Katika kila kipengele tumechukua majina matano yenye kura nyingi zaidi (baada ya kujumlisha SMS na online votes) kisha kuwatangaza top 5 nominees May 20.
Kwa kweli hata sisi tulishangazwa kidogo na baadhi ya kura zilizopigwa lakini tusingeweza kuingilia mchakato kwa vile mashabiki ndio waliyojitolea kupiga kura. Pia ni muhimu kuzingatia muda mchache na mifumo ya upigaji kura.
Tumeshaanza kupanga mikakati ya kuhakikisha tuwafikie watanzania wengi zaidi mwakani, tunakaribisha mawazo yenu pia. Katika uandaaji wa tuzo siyo rahisi kuwaridhisha wadau wote kila mara, ni kazi ngumu, ila maoni yenu ni muhimu sana na feedback inafanyiwa kazi.
Tunawasihi wadau wote wa JF wapige kura mwakani kuhakikisha their favorite matangazaji na kipindi are represented, tunawashukuru kutuunga mkono na kutumia muda wenu kujadili tuzo zetu changa.