Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 17,005
- 20,425
Kuna upotoshaji mkubwa kwamba kilichopo sasa ni MoU na Mkataba wa Awali tu hivyo hatuwezi kujadili kwamba Serikali imeingia mkataba na Dubai. Nafikiri tuwekane sawa kidogo na tupate tafsiri ya hayo maneno yana maana gani hasa.
Maana na Tafsiri halisi ya MoU - Memorandum of Understanding au kwakiswahili fasaha "Mkataba wa Makubaliano", Ni msingi unaowekwa kwaajili ya kusimamia jambo halisi ama mkataba kamili. Au ni Mwongozo kwaajili ya mkataba.
Pili kuna Mkataba wa Kiserikali, Intergovernmental Agreement, haya ni Makubaliano ya kiserika ni mkataba halisi ambayo lengo lake halisi huwa ni kuandaa utekelezaji wa mkataba. Kwa lugha nyingine tukiwa site tunaita mobilization site. Intergovernme Agreement ikishasainiwa inahesabika ni mkataba, mfano hii Intergovernmental Agreement ya Tz na Dubai ni ya miezi 12 kama wao wanavyosema japo hakuna palipoandikwa, na kwa muda mkataba ulivyosainiwa 25 October 2022, inamaana kwamba uhai wa Intergovernmental Agreement hiyo imebaki miezi 4 tu, ndiomaana wanakimbizana kutaka bunge liidhinishe fasta ili wasaini mkataba halisi. Kuna hoja kwamba kwanini Intergovernmental Agreement imeanza kufanya kazi kabla bunge halijaridhia kama sheria na katiba inavyotaka. Hili niwaachie Wanasheria Mh Lissu na Mh Peter Kibatala watatusaidia.
Mambo yote mawili hapo juu, yaani MoU na Intergovernmental Agreement yana kazi moja tu kwamba mkataba halisi utakaosainiwa hautatoka nje ya kile mlichokubaliana kilichoandikwa kwenye MoU na Intergovernmental Agreement. Kwa lugha rahisi ni kuwa Mkataba halisi Kati ya Serikali na Dubai, hautatoka nje ya Yale tunayoyasoma kwenye MoU ya Serikali na Dubai kuhusu Bandari ya Dar. Kwahiyo ndio kusema MoU hii ni sawa na mkataba tu, tofauti yake ni kuwa hii inaweza kuhaririwa na kuondolewa yale yatakayobishaniwa na pande mbili kabla ya kusaini mkataba.
Kwahiyo ilimradi MoU na Mkataba wa Kiserikali viko Public, Umma una haki ya kujadili na kukosoa kwa nguvu zote kwa lengo la kushauri marekebisho ya msingi. Kukosoa MoU haina maana tunaingilia Bunge, kila mtu kwa sehemu yake akosoe ashauri apinge na asifie, Ilimradi MoU iko public kwa umma. Aliyeleta kwa Umma MoU ni serikali, hivyo isiogope ukosozi, ipokee na iingatie hisia na matakwa ya umma!
Tuendelee kujalidi tusiruhusu wahalifu watuondoe kwenye mjadala kwakufanya spinning za kwamba Mh Mbowe kataja Uzanzibar nk, Hawa kina Kibajaji ni sehemu ya kundi la watanzania wenzetu wajinga tusiwape muda wetu. Tukumbuke sheria mbovu ya TISS inapitishwa katikati ya sakata la Bandari.
Na Yericko Nyerere