Tuzuie upotoshaji wa kiserikali kuhusu MoU na Mkataba wa Awali

Upotoshaji wa kiserikali upo sehemu moja tu.

Kama MoU na Preliminary Agreement zimeshakosewa, maana yake hata mkataba rasmi ukiandikwa, ambao lazima utokane na hayo makubaliano mawili ya mwanzo nao utakuwa umeshakosewa, kwasababu serikali yetu tayari ilishajifunga.

Tuna hasara sana kuwa na Rais asiyejielewa.
 
Hayo yote yasingekuepo kama tungekua na bunge thabiti, haya yote ni matokeo ya kua na Raisi kama JPM. Kaua mihimili yote sasa tumeanza kupata matokeo ya hilo.
Nakubaliana naww kbs ✔️ haiwezekan unajinasibu mzalendo na Rais wa wanyonge ambae unapambana na mafisadi lkn huwataki wapinzani bungeni ambao wamesaidia san watanzania kujua ufisadi unaofanyika nchini. Hata mikataba ya hovyo mingi walipinga sana, je lengo lilikua ni lipi la kuwaondoa wanaopinga mikataba mibovu na kuibua kashfa za kifisadi? Majibu nayataka toka kwa walinda legacy...
 
Mkataba sio porojo, ili uitwe mkataba mahakamani; lazima uthibitishe test tano.

1. Offer
2. Acceptance
3. Consideration
4. Mutual obligation
5. Capacity to enter the contract

Bila ya kuonyesha mahakama ivyo vitu vitano huo sio mkataba wa biashara.

Hapo kwenye 2 na 5 hiyo agreement ipo wazi ili serikali iweze fanya majadiliano lazima kwanza hayo maelewano yapitishwe na bunge sasa kuna mkataba hapo.

Kuna mambo mengi hapo ukifanyia test huo auwezi ita mkataba.
 
Hayo yote yasingekuepo kama tungekua na bunge thabiti, haya yote ni matokeo ya kua na Raisi kama JPM. Kaua mihimili yote sasa tumeanza kupata matokeo ya hilo.
Huwezi kumeza maji bila kumtaja JPM?

Mwaka gani hii nchi imefanya hicho unachokitaka?
 
Hivi serikali ya Dubai ni fully sovereign? Inatambulika kimataifa kama serikali inayomiliki territory? Dubai inamiliki territory? Sio kwamba ipo ndani ya territory ya UAE? Je, Dubai inatambulika kidiplomasia?
 
[emoji38][emoji38][emoji38] Safi sana !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…