Tuzungumze Kifamilia: Jinsi Kauli zetu Wazazi/Walezi zinavyokuwa Baraka au Laana kwa Mtoto

Lanlady

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2019
Posts
1,836
Reaction score
6,303
Nawasalimu nyote. Natumai mu wazima. Karibuni kwenye kikao cha familia tuimarishe mahusiano yetu.

Kwanza nianze kwa kusema, kwenye maisha yangu mimi binafsi, nimekuwa nikijifunza katika kila jambo ninaloliona au kusikia. Ninaamini kwamba, kila jambo huwa na sababu. Iwe nzuri au mbaya. Lazima tu kuna sababu ya jambo hilo kutokea.

Sasa nimeona katika familia nyingi, wazazi wengi hawajui au hawatambui kwamba vinywa vyao vimebeba baraka au laana kwa watoto wao. Baadhi ya wazazi hudhani kile kiumbe walichokileta duniani kitajiimarisha chenyewe na kujifunza chenyewe au kupokea baraka za moja kwa moja kutoka huko juu. La hasha!

Baraka za watoto ziko katika vinywa vya wazazi wao. Kila neno analotamka mzazi linaumba. Ni mara chache sana kukuta mzazi anamtakia mwanae mema au mabaya halafu yasimkute. Ni nadra sana.
Wengi kadri wanavyotamkiwa na wazazi wao ndivyo inavyokuwa.

Hivyo basi, ndugu mzazi uliye na watoto au mzazi tarajali, jitahidi kadri uwezavyo kuwatamkia watoto wako yaliyo mema. Ondoa kabisa chuki, hasira zinazotokana na msongo wa mawazo kwenye matamshi yako kwa watoto wako.

Nanyi walezi, mnayo fursa ya kusaidia kutoa mawaidha mema kwa watoto wengine mnaowalea. Hasa kwa wale wanaoishi na watoto wasio wa kuwazaa na wazazi wao hawako tena duniani.

Kuna watu wengi sana leo hii wanataabika kwenye safari ya mafanikio; si kwasababu ya matendo au mienendo yao, bali ni kwa sababu ya matamko ya laana kutoka kwa wazazi wao. Wamekosa kabisa muelekeo.
Wazazi wao ndio hasa kikwazo kwao.
Huenda ni kwasababu ya kutofautiana kiimani, mtazamo au mwenendo.

Mwenyezi Mungu atusaidie sana. Ili tuwatamkie watoto wetu baraka. Tuwasaidie kuishi pasipo majuto "kwanini hawa wamekuwa wazazi wangu?, kwanini nimezaliwa katika hii familia? "

Kumbuka haiwezekani mtoto kuchagua aina ya mzazi anayemtaka; bali ni rahisi kwa mzazi kutengeneza aina ya mtoto anayemtaka.

Hakuna mtoto anayechagua jina lake mwenyewe, bali wengi kama sio wote hupewa majina na wazazi/walezi wetu. Hakuna anayechagua kabila, wote tunarithi toka kwa wazazi.

Ndugu mzazi, chagua jina zuri la kumpa mtoto wako!
Asanteni kwa kunisoma!
 
Andiko zuri, wazazi na vijana Wana mengi ya kujifunza kuhusu malezi.

Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo, huwezi mlisha uchafu alafu utegemee mema.

tena wazazi wa uswahilini waji angalie mno, matusi siku nzima hapo mtaani. Sijui Wana tengeneza kamusi ya matusi

Nanyi wa kishua lindeni wanenu, wasiwe mlenda mlenda kuzidi, kidogo tu mommy, daddy
 
πŸ™
 
Siipendi tabia ya kurithisha majina kwa watoto, mengine yanabeba hadi tabia.....

Last born kwetu alipewa jina sijui la babu mzaa baba, basi huwa tunaambiwa alikuaga mkaliii afu anapotea tu nyumbani yani kama anatoroka hata mauti yalimkuta akiwa porini katoweka nyumbani.

Huyu last born sasa copy and paste jamaa mkali kama pilipili hata akikosa hataki kuulizwa yupo 30s ila hadi leo bado huwa anatoroka nyumbani.

Wazazi msiwape majina ya urithi watoto, heri ku gugu jina zuri mpe mtoto.
 
Kama namuona anavyosoma huu uzi huku amekasirika, ila miaka 30+ hatoroki, anakuwa ameondoka bila taarifa

 
Mzazi anaweza kumpa mtoto jina halafu akajikuta anamchukia kwasababu ya hilohilo jina
 
point to note
"Kumbuka haiwezekani mtoto kuchagua aina ya mzazi anayemtaka; bali ni rahisi kwa mzazi kutengeneza aina ya mtoto anayemtaka"
 
😳😳
 
Mtoto NI malezi.Tuwatamkie watoto mema Ili yaishi kwao.Hii issue ya majina hata sielewagi uhusiano wake wakati mwingine.Mbona kuna watotomajina ni mazuri Tu lakini watukutu balaa.Mfano ukamwita mtoto John kwa sababu lilikua ni jina la babako ndo mtoto anakua na tabia za babako.Mi naona cha msingi ni kumpa jina mtoto Bila kunuia tabia za mwenye jina.Sijui nimeelewaπŸ™†πŸ™†
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…