JituMirabaMinne
JF-Expert Member
- May 4, 2020
- 3,381
- 9,744
Tuzungumze kidogo kuhusu Oil za Automatic Gearbox.
Kuna makundi makubwa mawili ya Oil za Automatic Gearbox(ATF).
1. Standalone ATF
2. Universal ATF
Hebu tunagalie moja baada ya nyingine.
Universal ATF
Hizi ni zile ATF ambazo kopo lake linaandikwa msururu wa magari ambayo hiyo ATF inaweza kuwekwa. Yaani unaweza kukuta kopo lake limeandikwa gari hata 20 tofauti tofauti ambazo zinaweza tumia hiyo ATF. Hizi ndio ATF ambazo watu wengi sana wanazipenda, Hasa kwa sababu wanaona bei yake ipo chini. Haikatazwi kutumia hizi ATF lakini hata ukisoma katika baadhi ya manual za magari wameweka wazi kwamba tumia Universal ATF kwa muda mfupi wakati ukitafuta ATF sahihi(Standalone) kwa gearbox yako.
Asilimia kubwa ya watu wanaolalamika matatizo ya Gearbox, Shida huwa zinaanzia hapa kwenye kuweka Universal ATF. Unaweka Lubex ya Shilingi elfu 7 halafu ukitoka hapo unaenda kununua gearbox ya 2M.
Asilimia kubwa ya watu ambao gari zao zina gearbox za kisasa kama DSG(Vw), CVT(Nissan, Subaru, Honda, Baadhi ya toyota, n.k.), Tronic(Benz, Audi, Jeep n.k.) wameharibiwa sana Gearboxes zao kwa sababu gearbox hizo haziwezi kukuvumilia hata kwa siku moja.
Standalone ATF
Hizi ni Gearbox Oils ambazo OEM amerecommend zitumike katika gearbox Husika. Mara nyingi hizi huwa zinatumika kwa ajili ya aina fulani tu ya Gearbox. Kwa mfano ATF za Toyota kama T-II, T-III na T-IV ni standalone na zimetengenezwa kutumika kwa ajili ya Gearbox za toyota, Ni ngumu kukutana na gearbox ya G-tronic ya Mercedes eti inawekwa T-IV. Asilimia kubwa Standalone nyingi tunazifahamu kupitia Service Manual za magari au Dipstick ya Gearbox.
Kama unajali uhai wa gearbox ya gari lako basi Standalone ATF ndio njia pekee ya wewe kwenda. Weka hiyo ATF halafu tembea 50,000Km ambazo OEM wengi wanazitaja, Gearbox yako haitawahi kukusumbua. Kitu cha msingi tu uwe unaangalia kama Oil ya gearbox inapungua.