Tuzungumze kuhusu oil za automatic gearbox, huenda siku ikakuokoa gharama

Tuzungumze kuhusu oil za automatic gearbox, huenda siku ikakuokoa gharama

Toyota zote zenye gearbox za A type au U type. Siyo CVT kama Rumion.

So far kujua gearbox yako kwa toyota huwa kuna kibati kinakuwa kwenye frame ya mlango wa dereva au abiria wa mbele. Kwenye frame kuna kibati huwa kinaandikwa taarifa mbalimbali za gari na moja ya taarifa huandikwa Trans/Axle. Ukisoma hapo ndio utajua kama ni A au U au CVT. Kama ni CVT huwa inaanza na herufi K.

Pia kwa gari zingine hicho kibati kinakuwa upande wa engine huko ila kwenye frame ya gari kama kawaida.

Cc: Bavaria
 

Attachments

  • IMG_20210219_220118_619.jpg
    IMG_20210219_220118_619.jpg
    90.4 KB · Views: 103
Kwa ninachokijua carina Ti inapokea T-IV. Na Lubex ni Dexron II.

Gearbox ina moving parts nyingi sana hivyo maeneo mengi kunakuwa na friction. Kuweka mafuta sahihi kunakufanya upunguze friction na hivyo kuongeza uhai wa gearbox yako.
Nissan Xtrail NT30 niweke gearbox oil gani?
 
Hizi nyuzi za magari ukizifuatilia utagundua kuwa mafundi badala ya kutengeneza magari huwa wanaharibu magari na madereva badala ya kuendesha magari, kazi kubwa wanayofanya ni kuua magari!
Sikuizi madereva ni wajuaji sana kuliko mafundi,na wanapenda kusikia wanachowaza wao. Kuna dokta niliona kaandika mlangoni mwake "Majibu ya google yaache hapa mlangoni kabla hujaingia chumbani" nikajua wagonjwa wameshaanza kujiona wajuaji kuliko madokta 🤣 🤣 . Kazi za Fundi aachiwe fundi. Fundi wakati mwingine ukimwonyesha ujuaji nakumlazimisha afanye anachotaka dereva,lazima afanye ampendezeshe kama anavyotaka sababu dereva ndiyo anayetaka hela na hapa ndo magari huanza kuaribika.
 
Toyota zote zenye gearbox za A type au U type. Siyo CVT kama Rumion.

So far kujua gearbox yako kwa toyota huwa kuna kibati kinakuwa kwenye frame ya mlango wa dereva au abiria wa mbele. Kwenye frame kuna kibati huwa kinaandikwa taarifa mbalimbali za gari na moja ya taarifa huandikwa Trans/Axle. Ukisoma hapo ndio utajua kama ni A au U au CVT. Kama ni CVT huwa inaanza na herufi K.

Pia kwa gari zingine hicho kibati kinakuwa upande wa engine huko ila kwenye frame ya gari kama kawaida.

Cc: Bavaria

Sasa Giant

Mi yangu imeandikwa K310 ni toyota Axio

Unaeza nipa list ya oil nzuri za gearbox ?
 
Tuzungumze kidogo kuhusu Oil za Automatic Gearbox.

Kuna makundi makubwa mawili ya Oil za Automatic Gearbox(ATF).

1. Standalone ATF

2. Universal ATF

Hebu tunagalie moja baada ya nyingine.

Universal ATF

Hizi ni zile ATF ambazo kopo lake linaandikwa msururu wa magari ambayo hiyo ATF inaweza kuwekwa. Yaani unaweza kukuta kopo lake limeandikwa gari hata 20 tofauti tofauti ambazo zinaweza tumia hiyo ATF. Hizi ndio ATF ambazo watu wengi sana wanazipenda, Hasa kwa sababu wanaona bei yake ipo chini. Haikatazwi kutumia hizi ATF lakini hata ukisoma katika baadhi ya manual za magari wameweka wazi kwamba tumia Universal ATF kwa muda mfupi wakati ukitafuta ATF sahihi(Standalone) kwa gearbox yako.

Asilimia kubwa ya watu wanaolalamika matatizo ya Gearbox, Shida huwa zinaanzia hapa kwenye kuweka Universal ATF. Unaweka Lubex ya Shilingi elfu 7 halafu ukitoka hapo unaenda kununua gearbox ya 2M.

Asilimia kubwa ya watu ambao gari zao zina gearbox za kisasa kama DSG(Vw), CVT(Nissan, Subaru, Honda, Baadhi ya toyota, n.k.), Tronic(Benz, Audi, Jeep n.k.) wameharibiwa sana Gearboxes zao kwa sababu gearbox hizo haziwezi kukuvumilia hata kwa siku moja.


Standalone ATF

Hizi ni Gearbox Oils ambazo OEM amerecommend zitumike katika gearbox Husika. Mara nyingi hizi huwa zinatumika kwa ajili ya aina fulani tu ya Gearbox. Kwa mfano ATF za Toyota kama T-II, T-III na T-IV ni standalone na zimetengenezwa kutumika kwa ajili ya Gearbox za toyota, Ni ngumu kukutana na gearbox ya G-tronic ya Mercedes eti inawekwa T-IV. Asilimia kubwa Standalone nyingi tunazifahamu kupitia Service Manual za magari au Dipstick ya Gearbox.


Kama unajali uhai wa gearbox ya gari lako basi Standalone ATF ndio njia pekee ya wewe kwenda. Weka hiyo ATF halafu tembea 50,000Km ambazo OEM wengi wanazitaja, Gearbox yako haitawahi kukusumbua. Kitu cha msingi tu uwe unaangalia kama Oil ya gearbox inapungua.
Car Diagnosis, Engine service, Repair, Check engine, na mengine mengi.

Karibu Ofisini kwetu Dar es salaam, Sinza Kijiweni.

0688 758 625 au 0621 221 606
 
Back
Top Bottom