Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Na ww unaamini jigga hamuwez langa au swag?Kuna mstari anasema "na rap kwa kingereza,na rap kiswahili,,hata jigga haniwezi,,.me na rap kwa Lugha Mbili"
Umepiga cha arusha nini mkuu? Sifikirii hata kenya aliweza kuikamataSure jay z kwa langa ni mweupe kama CCM bila police
a mama yake ndo alikuwa mfadhili wake kwenye unga???Lakini langa kwani ni mboga 7 alikuwa kawekewa bili ya ngada na mother ake sio kama chid
Ndyoina maan
a mama yake ndo alikuwa mfadhili wake kwenye unga???
Aseee kweli, now vipi One The Incredible
"Sio Yule atakaye kimbia na kugeuka mwanariadha na adui wakivamia km Bou na da hustler"Song: Rafiki wa kweli
Artist: Langa
(verse 1🙂
Chakwake chakwako,chakwako cha kwake
Pamoja wakati wote kama kidole na pete
Sio lazima awe ndugu hata mtu wa mbali
Ukiumia anaskia uchungu anajali kwa kila hali
Tenda wema nenda zako,atayekulipa Mungu
Sio unawekeza ulipwe usipolipwa majungu
Unanichekea usoni unananipondea kisogoni
Kuwa mkweli na mwazi keep it real wit your homies
Sio yule atayekuficha kama demu wako hajatulia
Kisa siku zilizopita yeye pia alimpitia
Sio yule atayekimbia na kugeuka mwanariadha
Maadui wakivamia kama Bou na Da hustler
Rafiki batili,hawezi tunza siri
Kilemba cha ukoka nyoka ndumilakuwili
Sio tu kunywa na kumoka urafiki kupeana dili
Namna gani nizalishe 50 iwe 200
(Chorus)
Rafiki wa kweli,akufaaye kwa dhiki
Sio tu kwenye riziki au unapozimeki
Rafiki wa kweli, Kama mwili na kivuli
kwa mabaya au mazuri
Kwenye mvua ye mwamvuli
(verse 2)
Rafiki wa kweli sio tu kwenye riziki
Maana baada ya faraja unaweza rudi kwenye dhiki
Sio tu hali ngumu hakuna upendo wa kweli
That’s why makundi hayadumu waulize 2 berry
Nachotaka maishani mwangu namtakia mwanangu
Nachomtakia mama yangu ndo namtakia mke wangu
Nikimiliki range mwana namsusia pajero
Nikiwa na buku ana haki ya kuniomba jero
Tunagombana tunapatana tunaangalia mbele
Hatukumbushii ya jana yaliyopita si ndwele
Atakuwa glass ya maji ushikwapo na kiu
Katikati ya jangwa lisilo na mazao
Atakuwa asali na utamu kati ya limao
Wakati wa vita,atakulinda kama ngao
Na atakayekugusa,atamwinda mpaka kwao
Kushinda ama kushindwa ama zenu ama zao
(chorus)
(verse 3)
Marafiki zangu wa kweli sitowaacha milele
Ufukara au utajiri tutashirikiana kama nyenyele
Kwa miguu au usafiri,tutapiga misele
Majungu sitojali,we chonga sisi tutasonga mbele
Ukimgusa mwanangu umenigusa mimi
Ukimgusa mama yangu jua hatima yako kaburini
Nitakusaka uraiani kama nyoka wa kijani
Nafata miiko ya kitaani sikimbilii umwelani
Sitojali wewe nani haki itendeke mwishoni
Hata nikifa mbioni, nitakuibukia ndotoni
Kwa ajili ya rafiki zangu nipo tayari kuanzisha msala
Tayari kupata hasara kula mtaji wa biashara
Ukirukiwa na mamwela sitokubali ulale jela
Nina upendo wa ajabu unaozidi thamani hela
Najua wanangu masela watu wa mikasa na msala
Wanangu siwadai centi, noti, wala dala
Asikilizae hii track ajiulize kama yeye rafiki
Na kama ni mnafiki usinipe hata tano street
Roho saba huyu sasa hivi ni Captain wa jeshi. Anajua zaid ya tunavyojua maana ya kujua. Natafuta ngoma zake maana naonaga waite polisi na nakupenda hip hop tu
Wao wakimwaga ugali sie tunamwaga mboga amani kwa kaka voda - Babuu Kitaa ft Langa , Mchizi Mox - KimbiaKaka voda wambie wadogo zako waache kula poda watumie mmea.......
Ova
Asante mkuu umemalizaMan to man chidi benzi langa dimbani....
Nambie kama refarii record hii ya forty one....
Ado ado mdogo mdogo..........
............ ............ ........... .........
........... ............ ........... ..........
Nna mashuti zaidi ya Wayne rooney....
Km DJ nyimbo yako weka kaapunii.....
hautochezwa tena no kiwango weka kaapuni....
Chi chi chidi goo mtoto wa ilala komandoo love kwa wanangu wa ilala ...............
Chorus....
Nnaposimama hawasimami
Nnapochana hawachani
Nnavofanya hawafanyi......
......... ............ ...........
Bonge moja la colabo
Bonge moja la beat
enzi hizo bongo crank ndo imeingia.....
Daaaaah!!!!!!
Ngoma hiyo ya jay moe inaitwa jipange..kingo'ko ni mikocheni kwa kina babuu,langa,..na voda millionaire ni drug dealer mitaa hiyo..tena Don..hayo yanatosha tusije kutaftana..