TV 15 zaibwa hospitalini Njombe. Mkuu wa mkoa azunguka mitaani kuzisaka

Kuna vitu vingine vinashangaza sana unaiba tv za nini! Hii nchi uzalendo ulishakufa kabisa sijui tunarudije enzi za mwalimu
Ifike muda ofisi na taasisi zote za serikali kufungwe cctv cameras.
 
Nimewahi kufika hapo mpaka sasa najiuliza zimeibiwaje kwanza ni hospital ina utulivu sana na kila kitu wamejitahidi sana kukipangilia vizuri.
 
Ifike muda ofisi na taasisi zote za serikali kufungwe cctv cameras.
Wakifanya hivyo itasaidia sana kupunguza rushwa, wizi, uonevu, ufisadi na kuongeza uwajibikaji.

Receptions za vituo polisi, TRA, mahakama, halmashauri, wizara, serikali za mtaa, reception za hospitali, shule zote ziwekee camera, polisi, polisi wa barabarani wavae camera.
 
Kwanza TV 15 zote za nini kwa hospitali moja?
Na huyo mkuu wa mkoa naye hamnazo, Tv zimeibiwa Julai, yeye anaenda kuzurura madukani leo, miezi minne baada ya kuibiwa. Siku zote alikuwa wapi? Bora apigwe chini, akalime nyanya kama mwenzake Hapi
 
Kazi rahisi tuu,wapenzi siku hao staff wa Hospital kama hawajamtaja mwizi Kata salary zao tuu kufidia.

Hii iende Hadi kwenye wizi wa dawa.
 
Nchi imejaa majangili tupu, 15 TV zinaibwaje?
 
Sanaa zinaendelea kama kawaida kwenye kichaka cha wapigaji...🀣
Huyu baba ebu atulie, mwishowe atatenguliwa na asipangiwe tena kituo cha kazi...πŸ˜‚
Hii nchi wanasiasa wana nguvu kuliko watendaji....tehπŸ€—
Mkuu hii ni sanaa kama ulivyosema. Tena ni sanaa ya uonevu. Huko juu wanapiga mabilioni ije kuwa hivyo vi-TV? Hawa watu wanadhani wana hati miliki ya kuiba wenyewe na ngazi za chini hawaruhusiwi kuiba?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…