TV E inakuja kubamba,mawingu hamna chenu

TV E inakuja kubamba,mawingu hamna chenu

Sioni chochote kipya kutoka ETV, TV yenyewe mara siku nyingine ikate, mara giza. Kuhusu kushindana bado sana nahisi baada ya miaka mitano ndio tuanze kuwafikiria kuwapita clouds, TV ambayo ni nzuri ni EATV kuanzia vipindi, graphics ila clouds kwa mwaka huu wetoa upinzani mkubwa kwa EATV hasa upande wa vipindi (take one, clouds 360,the weekend chart show au shilawadu, kambi popote, siz kitaa). Ila clouds upande wa graphics bado EATV wapo vizuri, hao ETV wafanye kazi sana na wawe wabunifu mwisho wa siku watabaki kama wenzao TV 1 wapo wapo tu vipindi hawana ingawa upande wa graphics wapo vizuri.
 
EATV ni noma ...hapo Kenya tu wamewashindwa na inafunika mbaya ....Bongo ndio kabisaaa akina Clouds tv sauti tu shida ...
 
TVE inakipindi gani cha maana!?
Binafsi sijaona lolote la maana zaidi ya muziki 24/7 atleast Clouds wanajitahidi kidogo kwenye vipindi ingawa na yenyewe bado.

Hiyo TvE bado changa sana labda miaka saba mbele wanaweza niimpress.
Bado bro ipo kwenye majaribio.....
 
Wadau me natumia cable Tv hiyo channel 1 imeunganishwa ndani ya Decoder ya CTV sasa hakuna kinachoangalika humo yaani ni kama uchafu vile one day channel ya basketball iligoma kuonesha nikasema nitizame Channel 1 Dah inamuonekano mbovu sana kupita maelezo... Why Why Why hizi Tv kwanini zinalemaa hawajiungi na mambo ya HD picha murua... nilikuwa naiona star Tv ovyo japo bado ni ovyo ila Channel 1 ni kundi moja ila wamezidi... Ningekuwa nina mamlaka TCRA ningeondosha hizi channel zenye quality mbovu alaa! kama haujingi na HD ondoka hewani... mnatuharibia macho yetu ebo!
 
Najiuliza swali moja tu clouds pesa hawana au vp tv kuwa na graphics mbaya vile
Majjizo ana miaka mitatu ila balaa lake kila mtu anakaa
kuwa na pesa ni kitu kingine na kuwa na watu wenye uwezo ni kitu kingine....pesa si kila kitu
 
Claouds wanapotea sokoni soon! TV E wapo hot sana
Tatizo kubwa la tv stations za tz ni contents, kwa hiyo binafsi nitasubiri nione vipindi vyao na contents zake, unahitajika ubunifu! La sivyo wawe wanapiga mziki tu, kwa station yao kiwa clear nawapa heko.
 
TVE inakipindi gani cha maana!?
Binafsi sijaona lolote la maana zaidi ya muziki 24/7 atleast Clouds wanajitahidi kidogo kwenye vipindi ingawa na yenyewe bado.

Hiyo TvE bado changa sana labda miaka saba mbele wanaweza niimpress.
Acha wivu wa kikeee mtoa mada hajazungumzia vipindi mapovu yanakutoka tuu Tv haina hata mwezi wala haijaanza kurusha vipindi unaanza kuleta wivu wako wa kike Hata Radio mlisema hivyo iko wapi sasa ndio Radio no 1 Dar so na Tv kaa mkao wa kula na ujue ndio Tv pekee ya Tz iko Afrika nzima na uchanga wake futa povuuu sasa jifunze kukubali cha mwenzio
 
Kwa wiki sasa nimekuwa nikiitazama hii Tv stesheni ya TV E.Kiukweli niseme nawapa sifa zifutazo:-
1. Logo yao ni nzuri sana na waliodesign hii logo nawapa credit za kutosha.Ukiangalia logo ya Clouds fm haina mvuto na hata waliodesign hawakuwatendea haki clouds.

2. Graphics zo ni nzuri sana hata muonekano wake ikiwemo mpangilio wa rangi ni mzuri sana, kwa hili nawapongeza sana na nahisi wana timu ya watu makini sana.Clouds graphics zao ni mbovu sana na hata mpangilio wa rangi ni mbovu pia sijawahi kupenda muonekano wa Clouds

Mwisho niseme CLOUDS TV mjipange sana kwasababu soon mtakwenda kupoteza watazamaji kutokana na mpangili mbovu wa vipindi vyenu,muonekano mbaya wa Tv.TV E nawapa pongezi kwa mwanzo huu mzuri na nawatakia muendelezo mzuri ili mtoe changamoto kwa EATV kwani Clouds TV si mshindani kabisa.
TV E mmiliki wake ni nani vile
 
Kawaiida sana Azam wangeingiza SBC 1,2,3 malipo yangu yangekuwa Mubasharaaaa!!!!
 
Kwa wiki sasa nimekuwa nikiitazama hii Tv stesheni ya TV E.Kiukweli niseme nawapa sifa zifutazo:-
1. Logo yao ni nzuri sana na waliodesign hii logo nawapa credit za kutosha.Ukiangalia logo ya Clouds fm haina mvuto na hata waliodesign hawakuwatendea haki clouds.

2. Graphics zo ni nzuri sana hata muonekano wake ikiwemo mpangilio wa rangi ni mzuri sana, kwa hili nawapongeza sana na nahisi wana timu ya watu makini sana.Clouds graphics zao ni mbovu sana na hata mpangilio wa rangi ni mbovu pia sijawahi kupenda muonekano wa Clouds

Mwisho niseme CLOUDS TV mjipange sana kwasababu soon mtakwenda kupoteza watazamaji kutokana na mpangili mbovu wa vipindi vyenu,muonekano mbaya wa Tv.TV E nawapa pongezi kwa mwanzo huu mzuri na nawatakia muendelezo mzuri ili mtoe changamoto kwa EATV kwani Clouds TV si mshindani kabisa.
Ulosema yote ni sahihi hasa logo wametisha
 
TV-E ina muonekano mzuri sana na pia inasikika vizuri. ukichunguza utaona kuna stations chache za tv ambazo zina picha nzuri na sauti nzuri hapa Tanzania. hivi sasa wana kama segment moja ya kuomba nyimbo.
 
Back
Top Bottom