TV gani hapo nichukue 50 inch 4K solarmax au 43 inch FHD Hisense

TV gani hapo nichukue 50 inch 4K solarmax au 43 inch FHD Hisense

Nyamwage

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2020
Posts
760
Reaction score
1,875
Bei ziko sawa na zote ni smart
29459.jpg
29461.jpg
 
Achana nazo zote chukua Mewe. Usishtuke kisa jina baya, kwa sasa ndio TV ya low end yenye ubora. Hata hivyo low ends nyingi kina Solarmax, Alitop na wenzake huwa ni yale yale kwenye quality. Tofauti inakuja kwenye durability, ipi inachoma kadi mapema, ipi inahimili kudondoshwa au kutikiswa.

Hisense za siku hizi nyingi ni utapeli (sijawahi prove kama zipo fake au ni quality yao ndio mbovu) na hata hivyo ingekuwa ni genuine siikubali VIDAA kabisa.

Kwa soko la bongo ukishindwa Sony na Samsung inafuata TCL kisha ndio inakuja Haier na Hisense zinapambana hizi kila moja na mapungufu yake.
 
Nunua bidhaa kutokana na ubora badala ya mkumbo. Hisense kwa sasa wamebaki jina. Kwa experience ambayo ninayo, Solarmax inaweza kukupa uimara kuliko Hisense, mbali zaidi Solarmax ina Android.

Kwa hizo TV mbili, hakuna kitu Hisense atakuoffer ambacho Solarmax hatakupa, zaidi tu kuna vitu Solarmax atakupa ambapo Hisense hatoweza.
 
Umemaliza mzee
 
Nini kimetokea kwa Hisense? Naona kama inakataliwa.
 
Nini kimetokea kwa Hisense? Naona kama inakataliwa.
Durability imeshuka na kuzingua display bila sababu ya kueleweka kwa kesi nyingi wanavyo report watu.. japokua mi natumia mwaka wa 3 huu na iko ON kila siku zaidi ya masaa 12... Nafikiri matoleo ya sasa ni kimeo kama kweli zinawafia wadau..
 
Back
Top Bottom