TV Mpya vs. Mtumba: Ipi ni Bora kwa Bajeti ya Milioni 1.5

TV Mpya vs. Mtumba: Ipi ni Bora kwa Bajeti ya Milioni 1.5

Mlume ndagu

Member
Joined
Aug 12, 2018
Posts
64
Reaction score
75
Wataalamu wa mambo naomba msaada wenu katika uamuzi huu. Nina bajeti ya milioni 1.5 kwa ajili ya kununua TV, na leo nimezunguka madukani kutafuta chaguo bora.

Katika maduka ya bidhaa mpya, nimepata TV mbili zinazovutia:

  1. Hisense 65A6K/N – UHD Smart 4K
  2. TCL UHD Smart 4K
Zote zinauzwa kwa milioni 1.5, na zinakuja na zawadi za HDMI cable, Wall bracket, na delivery ya bure. Pia, zinakuwa na warranty ya mwaka mmoja.

Baada ya hapo, niliamua kutembelea maduka ya bidhaa za mtumba. Huko, nilipata chaguo mbili za kuvutia zaidi:

  1. Sony Bravia 65XE7002 – UHD Smart 4K, Made in Japan (2017)
  2. AVA FFalcon 65UF1 – UHD Smart 4K, Made in Australia
TV hizi za mtumba zinauzwa kwa milioni 1.4, lakini hazina miguu (stand), remote, wall bracket, HDMI cable, wala delivery ya bure. Pia, warranty inayotolewa ni ya miezi 6 pekee.

Sasa, nimebaki nikitafakari kama nichukue TV mpya za Kichina (Hisense ama TCL) ambazo zinakuja na warrant ndefu na vifaa vya ziada, au nichukue Sony ya mtumba, ambayo ni brand kubwa na inajulikana kwa kudumu muda mrefu, licha ya kuwa na warranty fupi.

Kwa kuzingatia ubora wa picha, uimara wa TV, na faida za kila chaguo, je, wadau mnanishauri nichague ipi? Nipo tayari kupokea ushauri kutoka kwa wenye uzoefu wa vifaa hivi.

Asanteni sana!
 
Wewe akili yako inakwambiaje kwani?

Ukikaa chini na kutathmini thamani ya pesa yako na uhitaji wa unachotaka unapata jibu gani??

Ukanunue kitu used chenye bei sawa na kipya kikiwa na mapungufu bila ya uhakika huko kilikotumika kilitumikaje ama ununue kitu kipya unachokibikiri mwenyewe, kikiwa kimetimia kila kikorombwezo chake na unapewa na warranty ya uhakika.
Akili mumkichwa bwashee.
 
Wewe akili yako inakwambiaje kwani?

Ukikaa chini na kutathmini thamani ya pesa yako na uhitaji wa unachotaka unapata jibu gani??

Ukanunue kitu used chenye bei sawa na kipya kikiwa na mapungufu bila ya uhakika huko kilikotumika kilitumikaje ama ununue kitu kipya unachokibikiri mwenyewe, kikiwa kimetimia kila kikorombwezo chake na chances are unapewa na warranty.
Akili mumkichwa bwashee.
N A K A Z I A
 
Mbona hujaweka kubwa lao Samsung? Mimi Tv kama sio Samsung basi Sony, nikikosa kabisa nitachukua LG kishingo upande.

Kwa hii case yako hapa ningechukia Sony, ila chukua sehemu ya kuaminika maana used kama imeshapigwa vyuma ni pasua kichwa.
 
Wewe akili yako inakwambiaje kwani?

Ukikaa chini na kutathmini thamani ya pesa yako na uhitaji wa unachotaka unapata jibu gani??

Ukanunue kitu used chenye bei sawa na kipya kikiwa na mapungufu bila ya uhakika huko kilikotumika kilitumikaje ama ununue kitu kipya unachokibikiri mwenyewe, kikiwa kimetimia kila kikorombwezo chake na chances are unapewa na warranty.
Akili mumkichwa bwashee.
Na mara nyingi used zinakuwa zinakula umeme sana isitoshe kuungua ni dakika 0
 
Wewe akili yako inakwambiaje kwani?

Ukikaa chini na kutathmini thamani ya pesa yako na uhitaji wa unachotaka unapata jibu gani??

Ukanunue kitu used chenye bei sawa na kipya kikiwa na mapungufu bila ya uhakika huko kilikotumika kilitumikaje ama ununue kitu kipya unachokibikiri mwenyewe, kikiwa kimetimia kila kikorombwezo chake na unapewa na warranty ya uhakika.
Akili mumkichwa bwashee.
Usikariri Mkuu. Binafsi nina jamaa zangu mmoja alichukua Hisense mpya mwingine Samsung used.

Hisense ilirudishwa dukani, ikatengenezwa ikaja kufa kabisa ikarudishwa tena kwa ugomvi mkubwa kidogo wapelekane polisi!
 
Hayo ma sony mara nyingi yanakuwa ya kizamani, yashapigika kisawa sawa huko yalipotoka, yakisumbua spare hupati mpaka aje juha mwenzio alienunua used ikamfia mbadilishane parts.
Kabisa hii kuna dada angu alinunua LG now ipo tu iliungua kashindwa tengeneza mafundi wanakula pesa wanasepa tv haipon
 
Usikariri Mkuu. Binafsi nina jamaa zangu mmoja alichukua Hisense mpya mwingine Samsung used.

Hisense ilirudishwa dukani, ikatengenezwa ikaja kufa kabisa ikarudishwa tena kwa ugomvi mkubwa kidogo wapelekane polisi!
Acha bas Hisense hii au nyinge
 
Usikariri Mkuu. Binafsi nina jamaa zangu mmoja alichukua Hisense mpya mwingine Samsung used.

Hisense ilirudishwa dukani, ikatengenezwa ikaja kufa kabisa ikarudishwa tena kwa ugomvi mkubwa kidogo wapelekane polisi!
Ok.
 
Wewe akili yako inakwambiaje kwani?

Ukikaa chini na kutathmini thamani ya pesa yako na uhitaji wa unachotaka unapata jibu gani??

Ukanunue kitu used chenye bei sawa na kipya kikiwa na mapungufu bila ya uhakika huko kilikotumika kilitumikaje ama ununue kitu kipya unachokibikiri mwenyewe, kikiwa kimetimia kila kikorombwezo chake na unapewa na warranty ya uhakika.
Akili mumkichwa bwashee.
Mimi Kama Afisa Mtendaji wa Kata ya Jamii Forum

Napiga na muhuri kabisa! Na elfu mbili ya muhuri sitawadai

Samaleko
 
Kwa Kutumia uzoefu wangu na kwa usalama wa matumizi Yako ya umeme naomba niandike kwa herufi kubwa
NUNUA TV MPYAAAAAAAAAAAA na uwe wa kwanza Kutumia
Tv used itakutesa hadi useme poo
 
Issue sio used au mpya issue ni ubora na uimara wa bidhaa husika, SONY ni imara hasa ukipata mtumba wa uhakika kwa kuwa ina warranty uhakika mkuu
NB: Kuwa makini 1.4M ni parefu
 
Kununua vifaa vya elektroniki vya mtumba ni risk. Wachache huwa wanafanikiwa kununua na visiwaletee songombingo za Kaboka Mchizi.
Ushauri kwa aliyeanzisha thread ni bora ununue TV mpya.
NB: Kwa ushauri wa kitaalamu uliokwenda shule wasiliana na mjukuu wa Mkwawa ndugu, Chief-Mkwawa
 
Back
Top Bottom