TV Mpya vs. Mtumba: Ipi ni Bora kwa Bajeti ya Milioni 1.5

Ngoja waje
Cc : Tumbili wa mjini
 
chief,vifaa vya mitumba ni sawa na mtu anaye andaa mkeka wa kubeti means una bahatisha kama kifaa kitakuwa kizuri au laa.
1.4 Mil ni parefu,au unaichezea shilingi kwenye tundu choo.

New brand ndo mpango mzima.
 
Zote ni bora. Je vipi wewe na kichanga nani mbora?
 
Mbona hujaweka kubwa lao Samsung? Mimi Tv kama sio Samsung basi Sony, nikikosa kabisa nitachukua LG kishingo upande.

Kwa hii case yako hapa ningechukia Sony, ila chukua sehemu ya kuaminika maana used kama imeshapigwa vyuma ni pasua kichwa.
Samsung ugonjwa wa vioo kuweka mistari kati na hatimaye kioo kizima kuwa giza hijawahi pata tiba.
 
Kwa brand ,hio mitumba miwili ni mizuri ila sasa je unauwezo wa kukagua spea moja moja kama haijawahi badilishwana kuweza kuona kama iko good au lah,Binafsi yangu mimi kwa bei ya 1.4m hapana wanauza bei juu sana,kama wanaweza shuka angalau 1m hapo sawa ila zingatia kuchunguza kwa makini (naimani hapa wauzaji wataleta utata),Mbali na hapo kaa na TCl tu ,kuhusu ulaji wa umeme soma spec utajua ni ulaji upi wa umeme upo kwa kifaa husika
 
Kwa 1.5M kama unanunua TV mtumba angalau iwe Oled, kutumia 1.5M kununua LED wakati at same price unapata LED mpya si wazo zuri.

Hisense U6/U6N series inakuwa considered kama best budget TV Kwa hio price point,

TCL Q651 series nazo nzuri kama mtu WA kucheza games.
 
TCL 65Q651 sio itakua zaidi ya 1.5M, maana naona model nyingi za kawaida ndo wanauza bei hio???
 
Chukua tcl au hisense mpya ila muhimu tu iwe kwa trusted dealer. Kuna tv copy nyingi sana sasa madukani tena nyingine zimekuwa assembled humu humu mitaani
 
Hivi mkuu wewe ukiambiwa uchague kati ya hisence na TCL zote zikiwa sawa Kwa kila kitu in terms of features na specifications.

Utachagua ipi mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…