TV1 Kurusha Live ligi kuu ya Uingereza(EPL)

TV1 Kurusha Live ligi kuu ya Uingereza(EPL)

Hapi no mwendo wa game moja kwa wiki kama wanahuakika wataonyedhs game yote watoe ratiba kbs
 
Ngoja tusubiri tuone, usiwaamini sana wabongo kwa ishu kama hizi
 
Exactly mkubwa!

Hata mimi kwa kuwa msimu wa ligi kuu hasa za Spain na England haujanza, niliamua kulipia kifurushi kidogo kabisa cha ACCESS/DSTV BOMBA na nimeshangaa wametuachia na channels tatu za sports (SS5, SS7 na SS12) wakati kabla ya hapo channels hizi zilikuwa zinapatikana kuanzia kifurushi cha Compact, Compact Plus na Premium tu ambayo monthly subs fee zake ni kubwa zaidi inayo range kuanzia 84,500 - 216,000!!

Kwenye kifurushi hiki i.e ACCESS/DSTV BOMBA, channels za sports zilikuwa tatu tu; SS BLITZ, SS select33 na SS Select34. Kama wameongeza na hizi, niwapongeze DSTV na Multchoice kwa ujumla kwa kutujali na kutupenda wateja wao.

Hata hivyo, naona SS12 ni maalumu kwa habari na matukio ya Olympic Games huko Rio De Janeiro, Brazil

All in all nadhani wameamua kuboresha vifurushi vyao na mimi nasema wamefanya jambo jema. Kumbu kumbu zangu zinaniambia kuwa SS5 huwa wanarusha mechi nyingi tu za EPL kwa wiki na SS7 huwa ni maalumu kwa mechi za La Liga.

Natumaini hata subscribers wa DSTV BOMBA/ACCESS nao wataweza sasa kuona mechi zaidi nyingi za EPL na La Liga kwa msimu huu na misimu ijayo
Ni offer maana hata wateja wapya pia wanapewa offer kuangalia bure kifurushi cha compact bure mwezi mzma
Halafu ss5 n home of la liga sema wanaonyeshaga pia mechi za epl
Ss3 ndo epl
 
Maana yangu, tulikimbilia kununua dish na visimbusi vya GTV,ambayo nayo haikudumu hata miezi Minne.
Gtv walifilisika kipindi kile kwny anguko la uchumi halafu dstv walivyo wajanja waka inunua maana iliwaletea ushindani sana ndo sasa inaitwa gotv
 
Gtv walifilisika kipindi kile kwny anguko la uchumi halafu dstv walivyo wajanja waka inunua maana iliwaletea ushindani sana ndo sasa inaitwa gotv

Nawakumbuka sana GTV.

Hawakuwaga strict sana kama walivyo DSTV hasa ktk malipo ya ada ya kila mwezi

Nakumbuka, kama trh yako ya kulipa imefika na ukashindwa kulipa, hawatakukatia matangazo hata kwa wiki mbili au zaidi mbele.

Hii ni tofauti kabisa na DSTV, kwani hawa jamaa kama huwa unalipa kila trh 5 ya kila mwezi ni sharti ifikapo trh hiyo uwe umelipa kinyume chake ukichelewa tu, wanaanza kukuondolea channel moja baada ya nyingine!!
 
TV1 si ni channel moja...kwa hiyo watazamaji hatutakuwa na uamuzi wa kuchagua mechi gani tuangalie wakati mechi tatu zinachezwa wakati mmoja. Au wamenunua na channels nyingine za star times kwa ajili ya kuonyesha mechi zote za epl bure?
 
Na la liga vipi aisee wataonyesha?..maana ndio ligi bora duniani,
 
Tv 1 acheni kukatisha katisha vipindi kwa kuweka matangazo Mara kwa mara


Sent from my iPad using JamiiForums
 
Utapeli mwingine mjini...watu waaingia kichwakichwa na kuishia kuangalia game moja kwa wiki
 
Wadau,mtaalamu wa uchambuzi wa masuala ya mpira yupo live sasa hivi ndani ya TV1.Huyu mzee anajua sana.
 
Ni habari njemba sana kwa ss wapenzi wa soka...lkn nafikiria kuhusu ishu ya match selection na idadi ya match kwa siku ..
 
Kwa dunia ya kibepari hakuna kitu cha bure.
 
Wengi wanafikiri kuwa sasa TV1 inaenda kurusha mechi zote za epl kama supersports.Haki ya matangazo yakulipia kwa ukanda wa jangwa la sahara bado dstv wana exclusive right.Njia hii ya kununua ili kuuza ndiyo pekee inampa muuzaji haki yakurusha mechi zote kwa wateja wake kupitia chaneli atakazozichagua.Hapa sasa ndo unaona dstv wanarusha kupitia supresports channels.

Njia nyingine ni kununua mechi moja ya jumamosi itakayochezwa kati ya saa nane mchana mpaka saa kumi za uingereza.Mnunuaji wa haki hii yeye analazimika kutouza hizo mechi,anatakiwa kuzirusha kupitia free to air channels(FTA) ambazo atakuwa ameingia nazo makubaliano ya kibiashara.Hapa sasa unawakuta ECOMAT wa Zimbabwe ambao wamepewa haki hizo mpaka msimu wa 2018/19.Wao watarusha hiyo mechi moja ndani ya muda huo tajwa siku ya jumamosi kupitia hizo TVs.Moja ya hizo TV ni TV1 ambao wamekubaliana na ecomat kurusha mechi moja siku ya jumamosi kwa hapa Tanzania na popote inapofika TV1 ndani ya kusini mwa jangwa la sahara.

Kwahiyo sio kama watu wengi walivyoelewa.Ukiangalia ratiba ya epl mechi nyingi kali hazichezwi jumamosi.Na hata zile kali chache zilizopangwa jumamosi hazichezwi muda huo ulioruhusiwa kwa tv za FTA.Hii inafanywa makusudi ili kuto wakosesha wateja watu wa pay TV kama dstv ambao wanalipa pesa nyingi kununua hizo haki.

Kwa hiyo umuhimu wa dstv kwa hapa bongo bado hauwezi kupunguzwa hata kidogo na hili suala la TV1.Kuna jumamosi zitakuwa hazina mechi hata moja kwa watu wa FTA kwakuwa tu mechi siku hiyo zinaanza late,zaidi ya ule uliokuwa stated kwenye mkataba wao na epl board.

Kwa makadirio ya mechi moja kila wiki tv1 wangerusha mechi 33 tu kwa msimu mmoja.Lakini kwa sababu ya limitation ya muda ni dhahiri zitakuwa chini ya 33.Sasa unawezaje kuibana dstv mwenye mechi 330 kwa season za epl huku wewe unapewa mechi chini ya asilimia 10 tena za kuchaguliwa kimkakati?

Mkuu nimekuelewa inakuwaje Zanzibar wanaona zote na Dstv IPO kwa 10000 tu kupitia Zanzibar cable na coconut
 
Back
Top Bottom