Ni offer maana hata wateja wapya pia wanapewa offer kuangalia bure kifurushi cha compact bure mwezi mzmaExactly mkubwa!
Hata mimi kwa kuwa msimu wa ligi kuu hasa za Spain na England haujanza, niliamua kulipia kifurushi kidogo kabisa cha ACCESS/DSTV BOMBA na nimeshangaa wametuachia na channels tatu za sports (SS5, SS7 na SS12) wakati kabla ya hapo channels hizi zilikuwa zinapatikana kuanzia kifurushi cha Compact, Compact Plus na Premium tu ambayo monthly subs fee zake ni kubwa zaidi inayo range kuanzia 84,500 - 216,000!!
Kwenye kifurushi hiki i.e ACCESS/DSTV BOMBA, channels za sports zilikuwa tatu tu; SS BLITZ, SS select33 na SS Select34. Kama wameongeza na hizi, niwapongeze DSTV na Multchoice kwa ujumla kwa kutujali na kutupenda wateja wao.
Hata hivyo, naona SS12 ni maalumu kwa habari na matukio ya Olympic Games huko Rio De Janeiro, Brazil
All in all nadhani wameamua kuboresha vifurushi vyao na mimi nasema wamefanya jambo jema. Kumbu kumbu zangu zinaniambia kuwa SS5 huwa wanarusha mechi nyingi tu za EPL kwa wiki na SS7 huwa ni maalumu kwa mechi za La Liga.
Natumaini hata subscribers wa DSTV BOMBA/ACCESS nao wataweza sasa kuona mechi zaidi nyingi za EPL na La Liga kwa msimu huu na misimu ijayo
Gtv walifilisika kipindi kile kwny anguko la uchumi halafu dstv walivyo wajanja waka inunua maana iliwaletea ushindani sana ndo sasa inaitwa gotvMaana yangu, tulikimbilia kununua dish na visimbusi vya GTV,ambayo nayo haikudumu hata miezi Minne.
Gtv walifilisika kipindi kile kwny anguko la uchumi halafu dstv walivyo wajanja waka inunua maana iliwaletea ushindani sana ndo sasa inaitwa gotv
Ya saa ngapi? Coz mechi ya SAA 11 tinaangaliaga CRTVHakuna kitu no metch moja kwa wiki
Hii CRTV unaipataje azam tv kaka?Ya saa ngapi? Coz mechi ya SAA 11 tinaangaliaga CRTV
Dah, kwenye king'amuzi changu hiyo others siioni kakaYes
Azamtv "other channels"
BURE
Inapatikana kule OTHER TV CHANNELS ni kwenye menu ya OK zen unapeleka kulia unakuta RADIO LIST halafu unaenda tena kulia unazikuta OTHER CHANNELSDah, kwenye king'amuzi changu hiyo others siioni kaka
Wengi wanafikiri kuwa sasa TV1 inaenda kurusha mechi zote za epl kama supersports.Haki ya matangazo yakulipia kwa ukanda wa jangwa la sahara bado dstv wana exclusive right.Njia hii ya kununua ili kuuza ndiyo pekee inampa muuzaji haki yakurusha mechi zote kwa wateja wake kupitia chaneli atakazozichagua.Hapa sasa ndo unaona dstv wanarusha kupitia supresports channels.
Njia nyingine ni kununua mechi moja ya jumamosi itakayochezwa kati ya saa nane mchana mpaka saa kumi za uingereza.Mnunuaji wa haki hii yeye analazimika kutouza hizo mechi,anatakiwa kuzirusha kupitia free to air channels(FTA) ambazo atakuwa ameingia nazo makubaliano ya kibiashara.Hapa sasa unawakuta ECOMAT wa Zimbabwe ambao wamepewa haki hizo mpaka msimu wa 2018/19.Wao watarusha hiyo mechi moja ndani ya muda huo tajwa siku ya jumamosi kupitia hizo TVs.Moja ya hizo TV ni TV1 ambao wamekubaliana na ecomat kurusha mechi moja siku ya jumamosi kwa hapa Tanzania na popote inapofika TV1 ndani ya kusini mwa jangwa la sahara.
Kwahiyo sio kama watu wengi walivyoelewa.Ukiangalia ratiba ya epl mechi nyingi kali hazichezwi jumamosi.Na hata zile kali chache zilizopangwa jumamosi hazichezwi muda huo ulioruhusiwa kwa tv za FTA.Hii inafanywa makusudi ili kuto wakosesha wateja watu wa pay TV kama dstv ambao wanalipa pesa nyingi kununua hizo haki.
Kwa hiyo umuhimu wa dstv kwa hapa bongo bado hauwezi kupunguzwa hata kidogo na hili suala la TV1.Kuna jumamosi zitakuwa hazina mechi hata moja kwa watu wa FTA kwakuwa tu mechi siku hiyo zinaanza late,zaidi ya ule uliokuwa stated kwenye mkataba wao na epl board.
Kwa makadirio ya mechi moja kila wiki tv1 wangerusha mechi 33 tu kwa msimu mmoja.Lakini kwa sababu ya limitation ya muda ni dhahiri zitakuwa chini ya 33.Sasa unawezaje kuibana dstv mwenye mechi 330 kwa season za epl huku wewe unapewa mechi chini ya asilimia 10 tena za kuchaguliwa kimkakati?