LGE2024 Twaha Mwaipaya atikisa Kilombero

LGE2024 Twaha Mwaipaya atikisa Kilombero

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Unaendelea kunitia huzuni mkuu 'Erytho', kwa taarifa yako kama hii.
Ni kichaa wa aina gani, asiye kuwa na akili kichwani anaye weza kuchezea halaiki ya aina hii, milioni 15.
Hii ni zaidi ya raia wote walioko kwenye nchi, kama Rwanda! Israel, kwani kuna watu wangapi?

Tunalo jeshi la polisi hapa, hata laki mbili hawafiki!

Na kumbuka, hakuna mtu anaye himiza hapa hiyo milioni 15 wakafanye vurugu! Tunasema hivi, kwa nini hiyo milioni 15 ikubali "UHALIFU", kuharibiwa kura zao na kuvurugiwa HAKI zao za kuwachagua viongozi wanao wataka wao?

Kwa nini tusijiulize haya maswali na kuyatafutia ufumbuzi? Kwa nini viongozi wa watu hawa, milioni 15 wasifanye kazi zao kwa karibu zaidi na watu hawa, ili matatizo yanayo wakabiri yashughulikiwe kwelikweli?

Binafsi ninge penda kupata jibu toka huko ndani ya CHADEMA, kuelezwa ugumu hasa upo wapi kutekeleza kazi hiyo.
Hawawezi kufikisha hao wanachama hata wanachama milioni 5 tu sidhani Kama wanao.

Wangekuwa na idadi kubwa hivyo ya wanachama wasingekuwa wanahangaishwa na polisi.

Wanachama milioni 15 maana yake kwa mwaka wangekusanya ada ya uanachama bilioni 15?
 
Hawawezi kufikisha hao wanachama hata wanachama milioni 5 tu sidhani Kama wanao.

Wangekuwa na idadi kubwa hivyo ya wanachama wasingekuwa wanahangaishwa na polisi.

Wanachama milioni 15 maana yake kwa mwaka wangekusanya ada ya uanachama bilioni 15?
Ukitaka kujuwa uzembe wa viongozi unaanzia wapi, hapa ndipo penye msingi wenyewe. Huenda hata wao hawajui wanao wanachama wangapi. Sitashangaa hilo.

Hata hao milioni 5 kama kweli wanao, na kuwa shirikisha vizuri kwenye maswala ya chama, hali ingekuwa ni tofauti na ilivyo sasa.

Inanisikitisha sana kama John John Mnyika atakuwa mhusika wa uzembe huu, kwa maana namwamini sana John, na kukubali uwezo wake mkubwa alio nao.

Kwa upande huu, kuna kitu hakiko sawa ndani ya CHADEMA.
 
Erythrocyte Jimboni la Kinondoni litazameni vizuri na leo nilitamani sana kuonana na Boni Yai lakini nilishindwa. Kinondoni na Kawe kuna viongozi wa hovyo mnoo, Mwenyekiti wa Wilaya na wa Mkoa kumbe wana kazi zao nje ya Mkoa, na wakati wote wa kufuatilia rufaa zetu pale Manispaa walikuwa hawaonekani.

Nashangaa leo naambiwa rufaa zetu za Kata ya Makumbusho zipo kwa Mtendaji wa Kata. Angalieni viongozi wa jimbo la Kinondoni ni hovyo mnooo. Mmoja nipo naye whatsaap nilimchana makavu.

Wamezingua sana.
Ni nyinyi wana chama mnao jitambua kutafuta njia ya kuondoa uozo wa viongozi kama hao. Hao ndio wanao kidhoofisha chama.
 
Back
Top Bottom