Uchaguzi 2020 Twalib Kadege: Nitaanzisha Wizara ya Mikopo itakayokopesha fedha kwa Wanawake na Vijana

Uchaguzi 2020 Twalib Kadege: Nitaanzisha Wizara ya Mikopo itakayokopesha fedha kwa Wanawake na Vijana

Faith Luvanga

Member
Joined
Aug 21, 2018
Posts
14
Reaction score
15
Akizungumza katika Mahojiano Maalum na JamiiForums, Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha UPDP, Twalib Kadege amesema iwapo Watanzania watampa ridhaa ya kuongoza, Serikali yake itahakikisha Watanzania wote wanakuwa na hali nzuri kimaisha.

Ataanzisha Wizara ya Mikopo itakayowakopesha fedha Vijana na Wanawake ili kuwawezesha kufanya shughuli mbalimbali zitakazowaingizia kipato. Lakini, pia Serikali yake itawatafutia masoko ndani na nje ya nchi ili bidhaa wanazozalisha ziuzwe kwa bei nzuri na waweze kupata faida.

"Vijana ni nguvu kazi changa, tutawaundia Wizara ya Mikopo itakayojishughulisha na Wanawake na Vijana ili waweze kujishughulisha zaidi na waache kukaa vijiweni badala yake wafanye kazi za biashara, kilimo na nyingine yoyote kulingana na mtu atakavyopenda"

Kadege ameongeza kuwa, Serikali yake inataka kuwaweka Watanzania katika hali nzuri ambapo wananchi watanufaika na kodi zao, wananchi wawe na unafuu wa maisha wasiwaze watakula nini au wataishi vipi kwani Serikali yake itatengeneza mazingira rafiki wananchi wote na wafanyakazi wataongezewa mishahara ambapo kima cha chini cha mshahara kwa wafanyakazi itakuwa ni Tsh. 400,000.
 
Back
Top Bottom