Twende mbele, turudi nyuma: Nchi za wenzetu zilizoendelea wanapiga kazi

Twende mbele, turudi nyuma: Nchi za wenzetu zilizoendelea wanapiga kazi

Sasa kwa saa analipwa let say dollar 50 kwanini usikomae masaa 15 utakua umechota dollars ngapi

Njoo huku saa 1
Mkuu, achana na kulipwa,
Mtu kwenye biashara yake tu hafanyi kazi muda huo, anachelewa fungua, anawahi funga, excuse nyingi
 
Uongo watanzania wanapenda sana kufanya kazi ili kuingiza kipato ila sere za serikali ni mbovu
Wapo wanaopenda kufanya kazi, na wapo wengi tu wavivu,

Wavivu wao wanailaumu serikali kwa kitu
 
Wapo wanaopenda kufanya kazi, na wapo wengi tu wavivu,

Wavivu wao wanailaumu serikali kwa kitu
Malipo ya nje na malipo ya hii Nchi yako ni tofauti na utendaji kazi lazima uwe tofauti hata kulipwa nje wanalipwa kwa wakati Nchi yako watu wanapigwa pass ndefu
 
Binafsi Japanese ndio walinishangaza wanajituma wale jamaa Site Eng na yeye anakunja Nondo....sema wanalipwa vizuri
 
Kila eneo lina value for money yake .unakuta huko unalipwa buk4 ila unaweza kula milo mi4...huku pia mishahara mikubwa ila expensive life ingawa huko kumezidi..mnanyonywa sana
Tatizo kubwa la hapa kwetu ni tija ndogo kwenye kazi tunazofanya. Mtu anaingia kiwandani saa 12 asubuhi hadi saa 12 jioni analipwa elfu 5 tu. Mkulima na familia nzima wanashindia shambani kutwa kwa jembe la mkono, kumaliza ekari moja inawachukua hadi siku 5, wakija kuvuna wanapigwa za uso mpaka hawajielewe. Kwenye mashamba ya chai ulipwa sh 300 kwa kilo moja, ukichuma kilo 20 kwa siku una elfu 6 tu.

Kiufupi mfumo wetu wa kiuchumi hautoi tija kwa kazi watu wafanyazo, vinginevyo wakulima wangekuwa na maisha bora kuliko hata watumishi waishio mijini. Wewe babu zetu wanalima miaka nenda rudi tena mazao ya biashara, na hawana starehe zozote za kuwapotezea pesa, lakini utawakuta pale pale kiuchumi, akijitahidi sana ana ngo'ombe zake na mifugo wengine kidogo. Huku madalali waliokaa vijiweni wakipata mamilioni kila wakati wa msimu.
 
Mwafrika hasa mtanzania anataka apige kazi masaa nane tena hayo bado anaona ni mengi,

Awahi kutoka kazini apitie baa amwagilie moyo na nyama choma huku akibishana simba na yanga.

Wanawake wanataka wawahi kutoka kazini wapitie saluni wakajirembe huku wakipiga soga na umbea.

Halafu jumapili wakajazane makanisani wakipayuka kama mbayuwayu kumuomba Mungu wapate mafanikio.

Hawa ndio waafrika..!!
😁😁😁😁😁😁😁
 
Mkuu, achana na kulipwa,
Mtu kwenye biashara yake tu hafanyi kazi muda huo, anachelewa fungua, anawahi funga, excuse nyingi
Huwa nasahanga sana unakuta mtu anafungua duka la mahitaji saa tatu!
Unakuta sehemu ya kuuza supu saa tatu bado supu haijawa tayari!
 
Back
Top Bottom