Ukijaribu kufuatilia kwenye mitandao ya kijamii hususan kwenye kurasa mashuhuri kama ICC, The White House, UN, nk utakutana na comments nyingi mno za SOS 🇻🇪 (Save Our Souls) ikifuatiwa na bendera ya venezuela. Wananchi wa Venezuela walitumia mitandao ya kijamii kupaza sauti kwa njia hiyo, na hatimaye kilio chao kimesikika. Hivyo watanzania kwa umoja wetu tunaweza kufanya hivyo pia, tukaanzisha kampeni ya SOS 🇹🇿, Twendeni tukacomment kila mahala mpaka dunia nzima ifahamu ukandamizaji na uvunjifu mkubwa wa haki unaoendelea Tanzania, Dunia ijue tupate msaada. Kwa umoja wetu ninaamini tunaweza!