Two people injured in suspected IED explosion at Latema junction near Odeon, Nairobi

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
24,941
Reaction score
28,869
January 26, 2019
Nairobi, Kenya

Two people have been injured in an explosion at Nairobi's Latema Road-Tom Mboya Street junction.

Reports say a man hired a trolley pusher to carry a box. It is suspected the box contained an Improvised Explosive Device which exploded.

According to Nairobi Police boss Philip Ndolo, the man who hired the trolley pusher ran away immediately after the explosion. Ndolo has asked the public to be on high alert and report any suspected terror activities.

Source : KTN news Kenya
=====

Shambulizi la bomu limetokea katikati ya jiji la Nairobi usiku huu na kujeruhi watu wawili, polisi wathibitisha.

Mlio mkubwa ulisikika katika eneo la Odeon, moja ya viunga vyenye shughuli nyingi na mikusanyiko ya watu wengi katikati ya jiji la Nairobi.

Bomu hilo lilikuwa limefichwa ndani ya begi na kusukumwa kwa mkokoteni.

Mkuu wa polisi wa jiji la Nairobi Philip Ndolo amewaambia wanahabari kuwa, bwana mmoja mwenye asili ya Kisomali alikodi mkokoteni na kupakia begi lake, na walipofika eneo la tukio, kwenye makutano ya barabara za Tom Mboya na Latema mmiliki huyo wa begi alitoweka.

"Alimhadaa mwenye mkokoteni kwa kumwambia amsubiri akafuate kitambulisho chake ambacho alikisahau...hakurudi na baada ya muda mfupi kilipuzi kilichokuwamo ndani ya begi hilo kililipuka,"amesema bwana Ndolo.

Mlipuko huo umewajeruhi mwendesha mkokoteni na mfanyabiashara ndogondogo aliyekuwepo karibu na mkokoteni. Mlio mkubwa wa bomu hilo ulizua taharuki kubwa kwenye eneo hilo lenye stendi nyingi za mabasi ya abiria.

Shambulio hilo linakuja siku chache toka viunga vya hoteli ya kifahari ya DusitD2 kushambuliwa na kupelekea vifo vya watu 21.

Tayari eneo hilo limefungwa na polisi na vikosi vya kutegua mabomu vimeshawasili eneo la tukio.
 
January 26, 2019
Nairobi, Kenya

Police official statement from the regional police commander Mr. Ndolo

Al shabab becoming desperate day by day. Hawa wajaribu Somalia ama Tz.
Yes very desperate!. After the blast, the only evidence to show that something had happened was the cordoned off road. But ironically just a few yards from the crime scene, people were busy going about their businesses as usual. Just perplexed by how the public is rapidly becoming hardened against the face of terrorism.
 
Shambulizi la bomu limetokea katikati ya jiji la Nairobi usiku huu na kujeruhi watu wawili, polisi wathibitisha.

Mlio mkubwa ulisikika katika eneo la Odeon, moja ya viunga vyenye shughuli nyingi na mikusanyiko ya watu wengi katikati ya jiji la Nairobi.

Bomu hilo lilikuwa limefichwa ndani ya begi na kusukumwa kwa mkokoteni.

Mkuu wa polisi wa jiji la Nairobi Philip Ndolo amewaambia wanahabari kuwa, bwana mmoja mwenye asili ya Kisomali alikodi mkokoteni na kupakia begi lake, na walipofika eneo la tukio, kwenye makutano ya barabara za Tom Mboya na Latema mmiliki huyo wa begi alitoweka.

"Alimhadaa mwenye mkokoteni kwa kumwambia amsubiri akafuate kitambulisho chake ambacho alikisahau...hakurudi na baada ya muda mfupi kilipuzi kilichokuwamo ndani ya begi hilo kililipuka,"amesema bwana Ndolo.

Mlipuko huo umewajeruhi mwendesha mkokoteni na mfanyabiashara ndogondogo aliyekuwepo karibu na mkokoteni. Mlio mkubwa wa bomu hilo ulizua taharuki kubwa kwenye eneo hilo lenye stendi nyingi za mabasi ya abiria.

Shambulio hilo linakuja siku chache toka viunga vya hoteli ya kifahari ya DusitD2 kushambuliwa na kupelekea vifo vya watu 21.

Tayari eneo hilo limefungwa na polisi na vikosi vya kutegua mabomu vimeshawasili eneo la tukio.

Chanzo cha habari ni BBC SWAHILI

Hawa alshabab watageuza kenya jangwa wasipotaka kuondoa unafiki somalia au kukaa round table.

Poleni,R.I.P waliouwawa.
 
hambulizi la bomu limetokea katikati ya jiji la Nairobi usiku huu na kujeruhi watu wawili, polisi wathibitisha.
Hawa alshabab watageuza kenya jangwa wasipotaka kuondoa unafiki somalia au kukaa round table.
Kwahiyo unashawishi Kenyan Government ikae round table na terrorists!?. Me sioni unafiki wa Kenya Somalia! n' those assholes should be sent to hell!!..
And even Gvt should sent an army there in hell to pursuit them too, wipe 'em clean!!..
 
Hawa wasomali washenzi sana, wanawaweka roho juu Wakenya na wageni kwamba wakati wowote kunaweza kuwa na shambulio la kigaidi.
 
Mlizipata zile silaha wanamgambo waliwanyang'ana jeshi la polisi pale Dar is Sluum? πŸ˜€πŸ˜€ kama walizipata nitag πŸ˜€πŸ˜€
Amani ya wasomali ni muhimu sana kuliko maisha ya waKenya, dah! kupanga ni kuchagua hayo ndio maisha mliochagua.
 
As long as hilo kambi ya wakimbizi kutoa Somalia hapo Kenya haitafungwa ,ugaidi wa Al shabab utaendelea. Hawa magaidi wa Alshabab wanatokea kwenye hiyo kambi kwenda kufundishwa na wakisha fuzu wanarudi kushambulia kwa kutumia kambi hiyo kwa kufanya maadaklizi yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…